Imefika wakati serikali iangalie mishahara ya watumishi wa "Local government" maana hali zao za mishahara ni ngumu na mbovu sana

Imefika wakati serikali iangalie mishahara ya watumishi wa "Local government" maana hali zao za mishahara ni ngumu na mbovu sana

Nadhani Kila Taasisi ya Serikali imeundwa kwa taratibu zake na mishahara Yao.
Muhimu kupambania nafasi za hizo Taasisi zenye salary kubwa.
Badala kila mtu wa Halmashauri apambane kuhama, kwanini serikali isi "balance" mishahara yake?

#YNWA
 
Umenena vizuri. Alafu ndio wanalalamikiwa sana, tuna demand delivery kubwa sana kutoka kwao, lakini ni watu wanaodhulumiwa. OR-TAMISEMI ni majanga. Kuna kipindi walitaka kuboresha, nadhani siasa tu. Ikaishia hewani.
Mawaziri hutupiga sanaa mikwara ila huwa hawajali "Maslahi yetu"

#YNWA
 
Popote pale utakapo kuwa kwenye hii serikali usipokula rushwa na kuiba hutoboi.msiseme nimewafundisha ukishikwa shauri yako.
Kwa serikali hii ya CCM kula rushwa ni ""Lazima""

#YNWA
 
Salaam ndugu Wana JF,

Naambiwa "Mama" yetu raisi wetu huwa anasoma humu JF.

Kwa heshima na taadhima naomba asome na hii.

Twende kwenye hoja..

Leo hii Kuna jamaa yangu kutoka halmashauri ya jirani kapata uhamisho kutoka halmashuri yake kwenda chuo cha Mandela (Arusha) yaani kwa huo mshahara anaoendea mpaka nimeshangaa.

Huyu jamaa basic analipwa TGS D = 745k ukitoa makota inayoingia mfukoni ni 500k and something.

Ila sasa huko aendako atakuwa analipwa basic 1.8Mil.

Hili limenifanya nijiulize ""KWANINI HALMASHAURI WANALIPWA KIDOGO KULIKO WATU WOTE SERIKALINI?""

Sometimes naonaga kama kufanya Kazi serikalini ukiwa chini ya TAMISEMI kama ni "laana/Majanga" maana kwenye mshahara huku ni dah "Ashukuriwe Mungu"

Hivi jiulize...
Tax Officer TRA Kazi yake ni kukusanya kodi, ada na tozo na Afisa mapato Halmashauri kaz yake nae ni kukusanya kodi na ushuru. Mbona sasa huyu Tax Officer (accounts) analipwa zaidi ya Afisa mapato wa Halmashauri (accounts)?

Hawa wawili, wamesoma course moja, chuo kimoja, wakaajiriwa na serikali moja ila tu kwasababu ya huyu yupo taasisi na huyu yupo "Local government" basi huyu anashavu zaidi ya huyu..!!
Why this, ikiwa wote wapo chini ya serikali moja?

Mishahara ya halmashauri inachekesha hasaa.
Ukiachana na afya ambao kidogo wao "alhamdulilahi ila"
1. Ukisoma diploma mshahara ni TGS C = 500k take home 400k
2. Ukisoma Bachelor ya miaka 3
TGS D = 700K take home 500k
3. Ukisoma Bachelor ya miaka mi4 ni TGS E = 900K take home 700k

(Mishahara hii nime approximate kwa kukaribisha zeros at the end)

Na kengine huku Halmashauri hizi masters na short course hazina hata maana ki-mshahara zaidi ya kwamba ni "Added advantage" ila sio ki-financial aspect HAKUNA LOLOTEE. Unakuta wewe una masters na mwenzio bachelor ila mshahara mnafanana.

Huwa nawaambia madogo ""Njoo halmashauri tafuta cheki namba halafu sepa huko kwenye mishahara minono"". Kwani nani asiyependa kufanya Kazi kwenye mshahara mkubwa?

Haiwezekani uliosoma nao wote mpo serikalini ila wao wana mishahara na maposho zaidi yako kisa wewe upo local government!

Kwa upande mwengine. Ukiangalia bungeni wanatupa sanaa lawama kwa Halmashauri huku wanasahau kuwa watumishi wao bungeni wana mishahara mikubwa kuliko wa halmashauri.

Yaani halmashauri inasemwa sanaa juu ya wizi ila HAKUNA MTU YEYOTE ANAYEONGEA KUHUSU UDOGO WA MISHAHARA YA HALMASHAURI.

Sijawahi hata siku moja kusikia taasisi yoyotee nchini ikiongelea maslahi ya watumishi wa Halmashauri zaidi ya kuwalaumu.

KUHUSU POSHO.
Watu wanakwambia "Halmashauri wanajilipa posho sana"

Wanasahau kuwa, posho ni mapato ya ndani "own source" na kuna Halmashauri hayo mapato ya ndani HAKUNA.

Hivi halmashauri kama Ukerewe, Tanganyika, Momba, Mpimbwe, Ileje WANAJILIPA MAPOSHO kwa mapato gani?
Ikiwatu makusanyo yao hat Bil 2 kwa mwaka hakuna (maana vyanzo vya kukusanyia hakuna).
Sasa Hawa hizo posho wanapata wapi?

MAMA HALI NI MBAYA.
Watumishi wa Halmashauri Wana hali mbaya. Achana na hizi Halmashauri za mjini, ila hizi Halmashauri za vijijni watu Wana hali mbaya na ""Asilimia 90 ya watumishi wanapigana na kuhangaika ili wahame"" maana hakuna anayekubali mshahara mdogo huku kwenye mkubwa panaonekana.

Imefika wakati hii mishahara ya Halmashauri iangaliwe. Inakuaje mtu mwenye bachelor yake ya uhasibu kaajiriwa tokea 2015 mpaka leo mshahara ni 745,000/= yaani ukitoa kodi kinachobaki ndio aendeshee maisha.

Walimu nao wanateseka.
Hizo TGTS C, D, E, F ukizisoma utadhani ni pesa nyingi.
Sasa ngoja uandikiwe ni kiasi gani UTABAKI KUSHANGAA.

Unakuta mwalimu kasoma na mwenzake Bach. Ed
Huyu kawa mwalimu wa sekondary huyu kaajiriwa assistant tutor.
Sasa ukitaka kuona ""maajabu cheki mishahara yao""

Tutor ana mshahara kuliko mwalimu. Bila kusahau Tutor anaposho za vipindi na vitu vyengine ila yeye mwalimu kwanini asiwe na posho za vipindi?

Kuna Watu wapo taasisi huko WANALIPWA mishahara mara tatu ya halmashauri.

Madereva katika fani nayoonea huruma ni walimu na madereva.

Kwani Kuna utofauti gani wa dereva wa BOT, Wizara na Halmashauri?

Hivi V8/gari si ileile na gia si zilezile na lami si ileile, KWANINI Dereva wa Halmashauri ana TGS B na wengine WANALIPWA mara mbili yake? Au magari yao wao yanapaa na ya halmashauri yanatembea kwenye lami?

HII SI AFYA KABISA.

Nina mengi ya kuongea NAOMBA NIISHIE HAPO.

Mama Niko chini ya miguu yako NAOMBA HILI LITAZAMWE.

Mishahara ya Halmashauri ni nomaaa Raisi wangu.

Asante.

#YNWA
Mkuu unaongoza kwa kulalamikia kazi za halmashauri, tatizo Tamisemi ina watumishi wengi sana, wakilipa kila mmoja mamilioni, serikali itafilisika. Hao watumishi wa taasisi ni wachache, ndomaana ni rahisi kuwalipa pesa nyingi, na kupata kazi zao siyo rahisi, interview, GPA kubwa etc, hawazoi zoi watumishi wengi kama kumbikumbi, kama ilivyo ktk halmashauri.

Huko halmashauri ukipandishwa madaraja hata mawili tu, mshahara unakuwa mkubwa, ila ktk taasisi sina hakika kama wako spidi ktk kupandisha watu mishahara.
 
Issue siyo TAMISEMI tu.

Hata serikali kuu na Mahakama Kuna mishahara ya kipumbavu tu.

Wenye mishahara yenye Afadhali ni Mashirika ya umma, ambayo huwa wanasingizia wanazalisha.

Lakini Halmashauri hata mzalishe vipi, watajilipa posho madiwani, Wakurugenzi na wakuu wa Idara. Wewe hata pesa ya likizo iliyopo kisheria hupati.
Naomba niulize kwan tgs d si ni moja kwa watumish wote? Na kinachoratibu ni utumish. Kwanin uwapige mawe wa serikal kuu kama wao wana hela sana. ? Wakat lawson sijui ndio hio hio.
 
Mkuu unaongoza kwa kulalamikia kazi za halmashauri, tatizo Tamisemi ina watumishi wengi sana, wakilipa kila mmoja mamilioni, serikali itafilisika. Hao watumishi wa taasisi ni wachache, ndomaana ni rahisi kuwalipa pesa nyingi, na kupata kazi zao siyo rahisi, interview, GPA kubwa etc, hawazoi zoi watumishi wengi kama kumbikumbi, kama ilivyo ktk halmashauri.

Huko halmashauri ukipandishwa madaraja hata mawili tu, mshahara unakuwa mkubwa, ila ktk taasisi sina hakika kama wako spidi ktk kupandisha watu mishahara.
Ndio mana nimeshangaa.kwa sabab kuna wat halmashaur wana magar makal hata wizara hagusi. Na kila siku vikao.weingine mcc sijui vikao gan.kamat za ujenz yan full full
 
Halafu Kazi ni kubwaa Sanaa,taasisi wanajipangia mishahara Huku wizara tofauti
Ujue hata malecturer salaries zinatofautiana
Hakuna USAWA kwenye hii nchi ila Halmashauri KUMEZIDI.

#YNWA
 
Naomba niulize kwan tgs d si ni moja kwa watumish wote? Na kinachoratibu ni utumish. Kwanin uwapige mawe wa serikal kuu kama wao wana hela sana. ? Wakat lawson sijui ndio hio hio.
Hapana.
Kila Taasisi ina mishahara yake.
Halmashauri ndio ina level za TGS D.

Mfano:-
Nilianza Kazi nashahara wa 745K Basic halmashauri, wakati huohuo niliajiriwa na jamaa angu. Jamaa angu alienda BRELA alikuwa analipa 1.6 Mil Basic
Huyu jamaa tulisoma wotee kuanzia primary, secondary tukaenda science, advance science, chuo kimoja na course moja, ila ajira zilikuja kututengenisha kimatabaka..!!

Ila wote ni
1. Watumishi wa serikali
2. Chini ya chama kimoja
3. Raisi mmoja
4. Mlipa mshahara ni mmoja

#YNWA
 
Mkuu unaongoza kwa kulalamikia kazi za halmashauri, tatizo Tamisemi ina watumishi wengi sana, wakilipa kila mmoja mamilioni, serikali itafilisika. Hao watumishi wa taasisi ni wachache, ndomaana ni rahisi kuwalipa pesa nyingi, na kupata kazi zao siyo rahisi, interview, GPA kubwa etc, hawazoi zoi watumishi wengi kama kumbikumbi, kama ilivyo ktk halmashauri.

Huko halmashauri ukipandishwa madaraja hata mawili tu, mshahara unakuwa mkubwa, ila ktk taasisi sina hakika kama wako spidi ktk kupandisha watu mishahara.

""..... interview, GPA kubwa etc.. ""

Labda huelewi ila Taasisi vilaza wapo kibao.
Nina GPA ya 3.9 nimeajiriwa Halmashauri, nilifanya interview na jamaa angu mwenye GPA ya 2.2 kaajiriwa Taasisi.

#YNWA
 
Ndio mana nimeshangaa.kwa sabab kuna wat halmashaur wana magar makal hata wizara hagusi. Na kila siku vikao.weingine mcc sijui vikao gan.kamat za ujenz yan full full
Watu wengi wanaotajirikia serikalini ni wezi au side hustle.
Mada yangu hailengi hizo factor.

Mada yangu inalenga financial equality and equity makazini.

Haya ya side hustle zinazokufanya umiliki "mali" Kali na za gharama "KILA MTU ANA AKILI ZAKE"

Tuzungumzie kile kipatikanacho cha haki makazini.

#YNWA
 
Naomba niulize kwan tgs d si ni moja kwa watumish wote? Na kinachoratibu ni utumish. Kwanin uwapige mawe wa serikal kuu kama wao wana hela sana. ? Wakat lawson sijui ndio hio hio.
TGS D ni moja. Ila mashirika hawalipani TGS
 
Hapana.
Kila Taasisi ina mishahara yake.
Halmashauri ndio ina level za TGS D.

Mfano:-
Nilianza Kazi nashahara wa 745K Basic halmashauri, wakati huohuo niliajiriwa na jamaa angu. Jamaa angu alienda BRELA alikuwa analipa 1.6 Mil Basic
Huyu jamaa tulisoma wotee kuanzia primary, secondary tukaenda science, advance science, chuo kimoja na course moja, ila ajira zilikuja kututengenisha kimatabaka..!!

Ila wote ni
1. Watumishi wa serikali
2. Chini ya chama kimoja
3. Raisi mmoja
4. Mlipa mshahara ni mmoja

#YNWA
Sasa nduguyangu kwanini nawewe usingeapply Brela? Na unajua kabisa taasisi zina mishahara mikubwa halafu unaombaje Tamisemi?
 
""..... interview, GPA kubwa etc.. ""

Labda huelewi ila Taasisi vilaza wapo kibao.
Nina GPA ya 3.9 nimeajiriwa Halmashauri, nilifanya interview na jamaa angu mwenye GPA ya 2.2 kaajiriwa Taasisi.

#YNWA
Basi kama siyo kujuana, ulihujumiwa.
 
Back
Top Bottom