Imefika wakati watu tujikite kwenye biashara ya kununua HISA

Imefika wakati watu tujikite kwenye biashara ya kununua HISA

inabidi huu Uzi niuzungukie Mara kwa Mara ...... Hapa lazima ntapata kitu
 
Mbona UTT,wao wanasema muwekezaji hatoathirika na kufilisika kwa kampuni!maana wao ndio wanakuwa kama dhamana,kwa kumnunulia mwachama wake hisa!kwa kampuni wanazoona zina faida nzuri.
 
Mbona UTT,wao wanasema muwekezaji hatoathirika na kufilisika kwa kampuni!maana wao ndio wanakuwa kama dhamana,kwa kumnunulia mwachama wake hisa!kwa kampuni wanazoona zina faida nzuri.
Kuna uzi humu jamaa analalamika hajapata gawio la faida kuanzia 2012.
 
Kuna kitu.kinaitwa UTT ...nahitaji kikifahamu
UTT ni mfuko wa pamoja wa uwekezaji. Katika hali ya kawaida ni vigumu kwa mtu mmoja mmoja kuwa na uwezo wa kununua hisa za kutosha kwenye kampuni zitakazomwezesha kupata faida ya kutosha kutokana na kupata gawio. Wanachokifanya UTT ni kukusanya hela hizi kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi na kutengeneza mfuko mmoja mkubwa ambao utakuwa na uwezo wa kuwekeza kwenye makampuni tofauti tofauti. Hawa wawekezaji wadogo wadogo wengi ndo watakaokuwa wanagawiwa faida itakayokuwa inapatikana kutokana na uwekezaji huo wa UTT.

Hawa jamaa wana mifuko tofauti tofauti kama umoja, mfuko wa watoto, mfuko wa kujikimu na mingineyo ambayo kila mmoja una malengo yake kwa hiyo ni uamuzi wako wewe unayetaka kuwekeza kuchagua mfuko unaoutaka katika hiyo kutegemeana na malengo yako.
 
Mkuu hizi biashara zinawafaa ma angel investors wana pesa mingi mpaka zinawashinda kwa sisi wapambanaji kuwekeza kwene soko la hisa ni vigumu kidogo, kwanza watu hawana elimu ya uwekezaji katika hisa, mtu hajui hata waraka wa mafanikio wa kampuni lakini anawaza hisa. Vilevile biashara ya hisa ina mambo kadhaa ya gawio ambayo kabla hujanunua hisa inabidi ujue kitu ambacho wengi hatuelimishwi. Hisa ni biashara nzuri kwa wenye kipato cha ziada.
 
Mbona UTT,wao wanasema muwekezaji hatoathirika na kufilisika kwa kampuni!maana wao ndio wanakuwa kama dhamana,kwa kumnunulia mwachama wake hisa!kwa kampuni wanazoona zina faida nzuri.
Hamna kampuni ambayo muwekezaji anaweza athirika kwa kufilisika kwa kampuni.
Labda kama kampuni haijasajiliwa.
 
UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaoendeshwa kwa kukusanya rasilimali (fedha) kutoka kwa wawekezaji na kuwekeza fedha hizo kwa mujibu wa malengo ya mfuko husika ili kupata faida. Umiliki wa uwekezaji wa mwekezaji unajulikana kama kipande au vipande. Kipande ni sehemu aliyonayo mwekezaji katika mfuko wa pamoja. Mfuko unapoongezeka thamani ndivyo vipande vinavyoongezeka thamani.

Sijaona tofauti iliyopo kati ya Hisa tulizozea na hii ya UTT.
UTT ni rahisi kujitoa ukihitaji.pesa zako ndani ya siku 7 lakini hisa lazima upate mnunuzi wa hisa zako. Mfuko wa UTT unanunua vipande vyako ukitaka kujitoa muda wowote kulingana na bei ya kununulia.
 
ntajihusisha na hisa baada ya magufuli kuondoka madarakani wacha niendelee kuuza ubuyu wa znz maana huyu jamaa uchumi unayumba na haeleweki
 
Kweli hisa ni nzuri sana. Kuna wakati nilikuwa nasoma mafanikio ya Warren buffet pamoja na kuanza kwa kuuza magazeti mtaan, kila kidogo alichikuwa akipata ktk kuuza magazine akikipeleka katka hisa. Na kweli mojawapo ya kilichomnyanyua ni hisa.
 
UTT ni rahisi kujitoa ukihitaji.pesa zako ndani ya siku 7 lakini hisa lazima upate mnunuzi wa hisa zako. Mfuko wa UTT unanunua vipande vyako ukitaka kujitoa muda wowote kulingana na bei ya kununulia.

UTT wao wanasimama kama mtu wa kati, wao wakishachukua hela wanaenda pia kununua hisa.
 
Wakuu msaada hivi kwa huko utt ukinunua his a MF ya 20000 baada ya miezi sita waweza pata faida ya kiasi gani?
 
Back
Top Bottom