Habari wana jukwaa,
Hapa nahitaji ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu masuala ya hisa za kampuni. Mimi nipo katika mchakato wa kuanzisha startup - lakini nahitaji kupata ufahamu juu ya masuala kadhaa, ikiwemo hili la hisa. Kuna
uzi huu niliuliza kuhusu mgawanyo wa hisa. Lakini sijapata mtu ambaye yupo deep ambae ameweza kujibu kwa uhakika. Sasa ninachohitaji kufahamu ni:
- Kwa kuzingatia utofauti wa AUTHORIZED SHARES, ISSUED SHARES na OUTSTANDING SHARES; Kuna uhusiano gani kati ya ISSUED SHARES na MTAJI WA KAMPUNI. I mean kwa mfano; Issued shares tuseme ni 10,000 zenye value ya TZS 20,000 each, Je; ni lazima kwenye vitabu vya mahesabu vya kampuni ionekane hiyo TZS 200,000,000.00? Au unaweza ukawa na issued shares zenye thamani kubwa kwenye MEMART, wakati mtaji halisi ulionao ni aslimia 10 tu ya mtaji ulioonesha kwenye MEMART?
In case swali lipo complicated; ngoja tujaribu hivi...
- MEMART na TRA kuna mahali hivi vitu viwili vinakutana? Let's say ume-indicate kwenye MEMART kwamba una mtaji (Issued shares) wa TZS 1,000,000,000.00; Je, katika ukaguzi wa mahesabu hiyo itatazamwa pia?
Nikiamini nimeeleweka, naomba kuwasilisha.
#Virus