Imefikia mahali kunywa juice za dukani ni hatarishi kwa afya yako kuliko kunywa soda!

Imefikia mahali kunywa juice za dukani ni hatarishi kwa afya yako kuliko kunywa soda!

Additives kibao, kuanzia rangi, ladha na sukari. Kwenye ladha huwekwa ladha ya tunda husika mf. embe, ukwaji, chungwa nk. Rangi huwekwa kutegemea na aina ya tunda lengwa. Shangaa juice nyingi za matunda aina ya embe zinaingizwa nchini toka huko Dubai na bei yake ni karibu sawa na bure. Tafakati na uchukue hatua.
Umesema jambo la maana sana. Kimsingi, juice nyingi sana za matunda zinazouzwa madukani hazitokani na matunda, bali artificial flavors za hayo matunda. Juzi hapa niliona mafuriko ya Juice za Makomamanga madukani, nikawa nawauliza watu, hebu niambieni hapa Tanzania mmeona wapi mashamba ya makomamanga mengi ya kuweza kutosheleza juice za ku-supply Tanzania nzima!

Juice za embe nyingi zinatoka Dubai, lakini Dubai hawana embe! Chemistry tu inachezewa hapa. Ndio maana leo tuna nyama ya ngombe isiyotokana na ng'ombe!
 
Kama ilikua sumu mkuu mbona hadi Leo wana waliokua wanaitumia kwa kulamba bado wanapeta na afya zao zipo strong kabisa hakuna cha ugonĵwa ini wala Figo sema watu waliamua kuharibu biashara ya watu
Unapokunywa sumu sio lazima ufe baada ya miaka mitano au kumi. Athari za hiyo sumu katika mambo fulani unaweza kuzipata baada ya miaka 20 hadi 30. Na pia kuna athari zisizo wazi. Unaweza ukawa unazaa watoto wenye matatizo bila kuchua chanzo ni majuice uliyofakamia huko nyuma. Watoto wanazaliwa na medical issues za ajabu hujui hata zimetoka wapi
 
Kuna chapa hapo limebandikwa
Fruit pure 😄

Ova
Halafu kitu cha ajabu sana kuhusu nchi zetu hizi, unakuta waziri amekomalia kukataa msaada wa chakula kutoka nje eti kwa sababu chakula kimewekewa virutubishi (fortified), wakati wale wanaoweka additives za ajabu kwenye juice na vyakula vingine ndani ya nchi, ambazo ni hatari kuliko hata hicho chakula toka nje wanapeta tu!

Hizi juice zinazotengenezwa nchini nchi za EU na USA hawawezi kame kukupa kibali cha kuuza huko. Tunapiga kelele tupeleke finished product wakati watengenezaji wetu hawajali kabisa viwango. Ndio maana wanasema tuleteeni nanasi, sio juice zenu za kutengeneza mitaani na kuweka sumu kali
 
Watu wangi hatutambui kwamba tatizo kubwa la kunywa soda kama Pepsi, Coca Cola nk, ni kwamba zina sukari nyingi sana ambayo si jambo zuri kwa afya yako.

Sasa utakuta watu wengi sana wamekuwa na mawazo kwamba ni vema kunywa juice za dukani (processed juice) kuliko kunywa soda, na hata wengine wakiwa tayari kuwapa watoto wao wadogo juice za dukani huku wakizuia kabisa kuwapa soda.

Huko ni kufikiri kuliko potoka sana!

Imefikia mahali ambapo kunywa juice za dukani ni hatari zaidi kuliko soda, hasa ukizingatia hizi juice zinavyotengenezwa. Navyojua ni kwamba, ukilinganisha na soda, juice ziko juu sana katika viwango vya benzene na ascobic acid, vitu hatarishi kwa afya vinavyoleta kansa, ambavyo sio tatizo katika soda!

Kumbuka kwamba, japo kuna tatizo la sukari nyingi katika soda, standard ya soda kama Pepsi au Coca Cola, inadhibitiwa kimataifa. Soda unayokunywa Tanzania inatakiwa kuwa ya kiwango kile kile kama ile utakayokunywa USA au Ulaya. Na tunajua wenzetu wako strict sana kwenye masuala ya viwango.

Tofauti na soda, juice utengenezaji wake ni local - ni kama kila mwenye kiwanda cha juice anaamua aweke madudu gani kwenye juice yake, na usimamizi wa udhibiti wa utengenezaji juice hapa nchini ni dhaifu sana. Inasemekana kuna wakati hata suala la kupitisha standard za juice nchini linafanyika kisiasa, kwa amri kutoka juu - mpeni lebel ya standard huyo - labda tu kwa sababu ni mchangiaji sana wa fedha za chama fulani. Na pia, imethibitika kwamba katika juice nyingi zilizoko madukani, viwango vya kemikali zilizowekwa si sawa na ilivyoandikwa kwenye chupa ya juice.

Na pia tukumbuke kwamba juice zimetengenezwa kukaa hata zaidi ya miaka miwili zikiwa hazijanywewa, wakati mzunguko wa soda ni mdogo sana - ndani ya mwezi mmoja soda zilizotengenezwa zinakuwa zimeisha, na hivyo sio rahisi kuwa na mabadiliko ya kikemia kama ilivyo kwa juice!

Hivyo ndugu zangu, tafakari sana juu ya soda Vs juice. Ni kweli soda zina tatizo la sukari nyingi - lakini juice matatizo yake ni sukari nyingi pia na madawa kibao yanawekwa bila udhibiti thabiti, hasa katika nchi zetu hizi. Juice nzuri ya wewe kunywa ni ya kutengeneza mwenyewe nyumbani ukitumia matunda fresh!

Kwa mnaoweza kumfikia Prof. Janabi, muulizeni swali la moja kwa moja; kama hapa Tanzania ungelazimika kuchagua kati ya juice ya dukani na soda ili unywe, ungeona angalau uko salama kunywa nini kati ya hivi vitu viwili?
1. Kuandika jambo lolote linalohusu bidhaa kama juice, soda, bia etc bila takwimu/na au matokeo yoyote ya utafiti ni kuharibia watu biashara zao.

2. Hakuna watengezaji wa soda wanatumia benzene kama benzene kuhifadhi juice.

3. Prof Janabi siyo mtaalamu wa lishe na hajafanya utafiti wowote juu ya soda au juice i. e kwa soda au juice kwa hiyo ushauri wake hautakuwa tofauti na huu wako au wa waganga wa kienyeji

4. Wenye viwanda vya soda wamewekeza mitaji yao kwenye majengo, mitambo, wafanyakazi, wanalipa kodi nk na kama hujafanya utafiti wa kisayansi juu ya juice zao si vizuri kuwaharibia biashara zao.
 
Nakumbuka mwaka 2015 pale cocobeach Coca-Cola walikuwa wanagawa vinywaji vyao vya coka vilivyokaribia kuexpire vilikuwa vile vichupa vidogo (Bambucha) aisee nilikunywa hadi yule jamaa aliyekua anagawa akanishngaa na ilikua ukimaliza unaenda kujichukulia mwenyewe hakuna anaekuzuia
Hujachekewa kapime bandama
 
kitu ambacho nimejifunza ni kwamba watu wengi hawajali swala la kuzingatia kuhusu ubora wa chakula pamoja na usafi katika ulaji . Kwa hiyo mada kama hizi angalau kwa sehemu zinawakumbusha watu kuchukua tahadhari kuhusu kuchukua hatua kwa mtu mmoja mmoja yeye binafsi kuilinda afya yake. Ukitaka kuthibitisha hili ,mtu yeyote anaye toa elimu juu ya maswala ya ulaji ulio bora anaonekana kama kituko, otherwise hii dunia ni dunia ya watu kuangalia utengenezaji wa faida no matter what ,kwa hiyo zile food description zilizo nyingi ni uongo hazimaanishi kivile, maana kuna vinywaji vimeandikwa non alcoholic lakini watu wakinywa wanalewa hivyo uamuzi uwe wa mtu yeye binafsi kujilinda afya yake.
 
1. Kuandika jambo lolote linalohusu bidhaa kama juice, soda, bia etc bila takwimu/na au matokeo yoyote ya utafiti ni kuharibia watu biashara zao.

2. Hakuna watengezaji wa soda wanatumia benzene kama benzene kuhifadhi juice.

3. Prof Janabi siyo mtaalamu wa lishe na hajafanya utafiti wowote juu ya soda au juice i. e kwa soda au juice kwa hiyo ushauri wake hautakuwa tofauti na huu wako au wa waganga wa kienyeji

4. Wenye viwanda vya soda wamewekeza mitaji yao kwenye majengo, mitambo, wafanyakazi, wanalipa kodi nk na kama hujafanya utafiti wa kisayansi juu ya juice zao si vizuri kuwaharibia biashara zao.
Hujui unachokisema, unaongea porojo tu. Kuandika kuhusu juice additives unahitaji takwimu? Unaonyesha jinsi usivyo na shule juu ya haya mambo.

Nenda kaongee na kina Lisu wenye akili wakuelimishe, kwa sababu tuna matarajio mtu kama Lisu akiwa kiongozi sidhani ataruhusu ujinga kama huu nchini wa kuua watu kwa chemicals, eti kwa kuwa wanalipa kodi. Ndio hayo ya mambo ya kuamrisha watu wapewe TBS lebels kwa amri toka juu

Ni aibu na hasara kwa Chadema kwa mtu kama wewe kujihusisha nao kwa kutumia kauli yao ya No Reform No Election. Kama wewe ndio aina ya wanachama wa Chadema basi Tanzania hatuna chama makini cha siasa, tuanze upya na jeshi. Ni aibu kwa Chadema kusema wana mfuasi kama wewe.
 
kitu ambacho nimejifunza ni kwamba watu wengi hawajali swala la kuzingatia kuhusu ubora wa chakula pamoja na usafi katika ulaji . Kwa hiyo mada kama hizi angalau kwa sehemu zinawakumbusha watu kuchukua tahadhari kuhusu kuchukua hatua kwa mtu mmoja mmoja yeye binafsi kuilinda afya yake. Ukitaka kuthibitisha hili ,mtu yeyote anaye toa elimu juu ya maswala ya ulaji ulio bora anaonekana kama kituko, otherwise hii dunia ni dunia ya watu kuangalia utengenezaji wa faida no matter what ,kwa hiyo zile food description zilizo nyingi ni uongo hazimaanishi kivile, maana kuna vinywaji vimeandikwa non alcoholic lakini watu wakinywa wanalewa hivyo uamuzi uwe wa mtu yeye binafsi kujilinda afya yake.
Mkuu umeongea point sana. Tanzania kinachotuua ni kwamba TBS wakitoa lebel basi wanajisahau. Sidhani kama wanafanya spot checks - watakuambia hatuna fedha za kutosha kucheck products zilizoko kwenye shelves. Wakienda viwandani kuchukua sample wanapewa zawadi ya hizohizo bidhaa wanazotakiwa kucheck, kama carton za juice, wanaondoka wanakenua meno kwa furaha! Hawajui kuwa hiyo ni corruption.

Halafu ukiwalalamikia TBS kuhusu bidhaa fulani, badala ya kufanya uchunguzi na kujihakikishia wanasema tulishacheki huko nyuma tukaona wako sawa. Sasa kama mlicheki huko nyuma mnajuaje hawa watu waliendelea kuwa sawa baada ya kupewa lebel ya TBS? Umeona malalamiko kwenye video clip, na jinsi TBS wanavyotoa majibu ya kisiasa, utafiri wao ndio kitengo cha marketing za watengenezaji juice wanaolalamikiwa!
 
Juice vingi utasoma zinafoood grade zenye E-numbers ambazo zimepigwa marufuku usa miaka ya 1980s kwa kuwa waliona ni hatari
 
Mnataka kucomplicate sana mambo, vitu visivyo salama kwa afya ni pombe, sigara na wanawake.

Hizo zingine mbwembwe tu.
 
Mnataka kucomplicate sana mambo, vitu visivyo salama kwa afya ni pombe, sigara na wanawake.

Hizo zingine mbwembwe tu.
Sawa Mkuu. Huyu mtu hapa chini amekuwa hivi kwa sababu ya pombe, sigara na wanawake!

1739870423141.png

Na kama ulienda shule soma hapa

Juice additives, particularly artificial sweeteners, high fructose corn syrup, and certain artificial flavors, can negatively impact health by contributing to issues like blood sugar spikes, increased risk of obesity, and potential neurological effects, making it generally advisable to choose juices with minimal additives or opt for whole fruits instead; while some additives may be considered safe in small amounts, excessive consumption can raise concerns
According to several studies, health issues such as asthma, attention deficit hyperactivity disorder (ADHD), heart difficulties, cancer, obesity, and others are caused by harmful additives and preservatives. Some food additives may interfere with hormones and influences growth and development.

It is one of the reasons why so many children are overweight. Children are more likely than adults to be exposed to these types of dietary intakes. Several food additives are used by women during pregnancy and breast feeding that are not fully safe. We must take specific precaution to avoid consuming dangerous compounds before they begin to wreak havoc on our health.
 
Hujui unachokisema, unaongea porojo tu. Kuandika kuhusu juice additives unahitaji takwimu? Unaonyesha jinsi usivyo na shule juu ya haya mambo.

Nenda kaongee na kina Lisu wenye akili wakuelimishe, kwa sababu tuna matarajio mtu kama Lisu akiwa kiongozi sidhani ataruhusu ujinga kama huu nchini wa kuua watu kwa chemicals, eti kwa kuwa wanalipa kodi. Ndio hayo ya mambo ya kuamrisha watu wapewe TBS lebels kwa amri toka juu

Ni aibu na hasara kwa Chadema kwa mtu kama wewe kujihusisha nao kwa kutumia kauli yao ya No Reform No Election. Kama wewe ndio aina ya wanachama wa Chadema basi Tanzania hatuna chama makini cha siasa, tuanze upya na jeshi. Ni aibu kwa Chadema kusema wana mfuasi kama wewe.
Povu la nini?
Mwaga matokeo ya utafiti wako hapa.
Unajua tofauti kati ya benzene na benzoic acid?
 
Back
Top Bottom