Tetesi: Imejulikana, CCM wanategemea kupewa hela za kampeni uchaguzi ujao Toka DPW.

Tetesi: Imejulikana, CCM wanategemea kupewa hela za kampeni uchaguzi ujao Toka DPW.

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,294
Reaction score
4,920
Mara nyingi CCM hutegemea pesa za uchaguzi Toka kwa matajiri Ambao huzawadiwa rasilimali zetu kiholela. Wakati huu imekua ni zamu ya DPW ndio maana inatetewa kwa nguvu zote.
Bibi tozo amehakikishiwa mpunga mrefu wa kampeni kwa chama chake ili waendelee kukaa madarakani na kuwalinda hawa wanyonyaji. Watanganyika tuwe macho. Narudia tena Watanganyika tuwe macho.
 
Hapana. Wana CCM wote bara tumeukataa mkataba. CCM si bora kuliko uhuru wetu. Ukiona mwana CCM anashabikia huu ujinga jua amehongwa au analinda kibarua chake tu.

CCM tuko pamoja na wananchi. Hatuuzi bandari zetu. Wakauze zao hukooo
 
Kampeni kwa hapa Bongo haihitaji fedha nyingi hivyo!!

Ni kutokutumia akili tu ndio tunashindwa!!
KWA Tehama iliyopo unashindwaje kuwafikia wananchi!!?
 
Mara nyingi CCM hutegemea pesa za uchaguzi Toka kwa matajiri Ambao huzawadiwa rasilimali zetu kiholela. Wakati huu imekua ni zamu ya DPW ndio maana inatetewa kwa nguvu zote.
Bibi tozo amehakikishiwa mpunga mrefu wa kampeni kwa chama chake ili waendelee kukaa madarakani na kuwalinda hawa wanyonyaji. Watanganyika tuwe macho. Narudia tena Watanganyika tuwe macho.
Ingawa umeandika kwa ufupi na watu wengi hawatasoma huu uzi jambo hili laweza kuwa kweli. Mkataba huu wa IGA unao ukakasi kwa mtu yeyote, hata huyo ambaye sahihi yake ipo pale. Hapana shaka yoyote kuwa mkataba umeandaliwa na Dubai bila shaka baada ya kupewa idhini. Pengine nao wametengeneza mkataba wa aina hii baada ya kufahamu kuwa mbali na kuendesha bandari watakuwa pia na jukumu la kuwezesha uchaguzi wa 2025. Ndiyo kusema upo uwezekano fedha za uchaguzi 2025 zimo ndani ya mkataba huu na ndiyo maana kuna chama cha siasa kimepata kudai hadharani kuwa wazungu na mashirika ya kimataifa tayari wameambiwa msaada wao kuwezesha uchaguzi huo hautahitajika! Hisia hizi zinapata nguvu tunapojiuliza, je, JPM alipata wapi fedha za uchaguzi wa 2020 bila misaada rasmi kutoka kwa wafadhili waliozoeleka? Kwanini alizuia watazamaji wa uchaguzi kutoka mataifa ya magharibi? Je, nj kwanini mara baada ya uchaguzi wa 2020 harakati za kunyakua ardhi ya Loliondo kutoka kwa wenyejj zilipamba moto na kuhitimishwa baada ya muda mfupi na bila mashauriano ya maana na jamii? Wanasiasa wa Afrika huweza kuuza nchi yao ilimradi wao wabakie madarakani.
 
Kampeni kwa hapa Bongo haihitaji fedha nyingi hivyo!!

Ni kutokutumia akili tu ndio tunashindwa!!
KWA Tehama iliyopo unashindwaje kuwafikia wananchi!!?
Kwa hiyo,,,hayo matumizi ya hiyo tehama na shughuli nzima za hiyo miundombinu ya tehama hazitakuwa na gharama??na kwa Maeneo mengi ya nchi yetu bado hajafikiwa sio tu na hiyo miundombinu ya tehama Bali hata Barbara tuu ni shida!!
 
Hapana. Wana CCM wote bara tumeukataa mkataba. CCM si bora kuliko uhuru wetu.
Bahati mbaya mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Kamati kuu ya CCM pamoja na Wabunge wa CCM wamesharidhia Agano aka Makubaliano aka Mkataba wa DP World ya Waarabu Dubai. Hiyo CCM unayoiongelea ni ipi?
Ukiona mwana CCM anashabikia huu ujinga jua amehongwa au analinda kibarua chake tu.
Bahati mbaya CCM kama chama msingi wake mkuu ni hongo na rushwa. Hiyo CCM unayoiongelea ni ipi? Rais wote wawili, Makamo wa Rais wote watatu, serikali zote mbili...! CCM inalinda itikadi yake!
CCM tuko pamoja na wananchi.
Je nao wananchi wako na CCM? Kalaghabaho!
Hatuuzi bandari zetu.
Naona uko ndotoni, amka, tayari zimeshauzwa!
Wakauze zao hukooo
Thubutu. Kula na kipofu mbona raha. Kumbuka za mlevi huliwa na mgema!
 
Back
Top Bottom