Imekuaje barabara karibia nchi nzima zinabomolewa na kuachwa kwa mda mrefu bila marekebisho

Imekuaje barabara karibia nchi nzima zinabomolewa na kuachwa kwa mda mrefu bila marekebisho

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
765
Reaction score
490
Hii ni Tabia chafu sanna ya kufumua barabara kisha inaachwa zaidi ya miezi sita huku ikiathiri maisha ya watu kwa maradhi ya macho mafua vifua vumbi kali sanna magari kuharibuka kwa mashimo tumerudi miaka nyuma huko.

Kwanini kama budget hazijatengwa barabara zifumuliwe?

Naendelea kusema Serikali ya mama ina tatizo la kimfumo mambo hufanyika hovyo hovyo.

Na cha kushangaza kelele za machawa ni nyingi mno Bimkubwa yameshinda mwambieni akae pembeni
 
Kwani hujui kwamba ukijua kujenga ni lazima ujue kubomoa?

Hii ni kanuni ya *mainjinia
 
Hii ni Tabia chafu sanna ya kufumua barabara kisha inaachwa zaidi ya miezi sita huku ikiathiri maisha ya watu kwa maradhi ya macho mafua vifua vumbi kali sanna magari kuharibuka kwa mashimo tumerudi miaka nyuma huko
Kwanini kama budget hazijatengwa barabara zifumuliwe?
Naendelea kusema Serikali ya mama ina tatizo la kimfumo mambo hufanyika hovyo hovyo
Na cha kushangaza kelele za machawa ni nyingi mno Bimkubwa yameshinda mwambieni akae pembeni
Tulia dogo, bado tunafanya ile kwa kitaalamu inaitwa upembuzi yakinifu na waliochelewa kuona barabara Iko kwenye ukarabati waone [emoji1787][emoji1787].
 
Kama barabara
zipi hizo mtoa hoja?
usinambie kwa tanzania bara hii huko unapoishi hakuna barabara iliofumuliwa ikaachwa tu ila kilio zaidi kipo mtwara asilimia 80 ya barabara zote zimefumuliwa tangu mwezi wa pili na zimeachwa tu mfano watu tunosafiri kutoka masasi songea barabara inavipande vingi vilivyotelekezwa tu
 
Bado hamjasema. DMDP tangu April imeshindwa kuanza. Subirini tujihakikishie kurudi 2025 kwanza.
 
Jumatatu ya wiki iliyopita nilikua natoka DSM kwenda Masasi,,,tukiwa tupo kibuyu kuna sehemu oanaitwa kinene kabla hujafika Kimanzi chana ghafla barabara mbele imekatwa ina vumbi na hakuna alama ebwana tuliingia na ki IST mzima mzima tukiwa na 120 ilibidi tusimame kuikagua kwanza. Sijui kwanini njia ya kusini haithaminiwi kabisa yaani kutoka mbagala kokoto mpaka masasi njia ni mbovu sana.
 
usinambie kwa tanzania bara hii huko unapoishi hakuna barabara iliofumuliwa ikaachwa tu ila kilio zaidi kipo mtwara asilimia 80 ya barabara zote zimefumuliwa tangu mwezi wa pili na zimeachwa tu mfano watu tunosafiri kutoka masasi songea barabara inavipande vingi vilivyotelekezwa tu
Masasi-Songea njia ilikua safi ,ni sehemu gani wamefumu maana ule mkeka bado mpya aisee.
 
Hii ni Tabia chafu sanna ya kufumua barabara kisha inaachwa zaidi ya miezi sita huku ikiathiri maisha ya watu kwa maradhi ya macho mafua vifua vumbi kali sanna magari kuharibuka kwa mashimo tumerudi miaka nyuma huko.

Kwanini kama budget hazijatengwa barabara zifumuliwe?

Naendelea kusema Serikali ya mama ina tatizo la kimfumo mambo hufanyika hovyo hovyo.

Na cha kushangaza kelele za machawa ni nyingi mno Bimkubwa yameshinda mwambieni akae pembeni
Bi mkubwa ameshasema yeye chura kiziwi hivyo hasikii kelele... Huyu Rais 2025 akijaribu hata kujishindanisha na tofali na uchaguzi ukawa huru hatoboi.
 
Back
Top Bottom