Imekuwa ni nadra sana kukuta waislam katika makabila haya

Imekuwa ni nadra sana kukuta waislam katika makabila haya

1. Wachaga - kumkuta mchaga muislam labda kwa mbali sana awe wa machame
2. Masai
3. Wakinga
4. Wangoni
5. Wajita
6. Wagogo

Wanyakyusa hapo zamani na wao ilikuwa ni nadra sana lakini sikuhizi imeanza kuwa kawaida utawakuta Mashehe kina Mwaipopo, wachezaji kina Azizi Andambwile, makocha kina Juma Mwambusi, na mitaani wapo wenye majina yote ya kiarabu.

Wakurya nao sikuhizi utawakuta waislam kina Mohammed, Abdallah, n.k.

Wapare ni kawaida sana kuwakuta waislam.

Wahehe wa Iringa waislam wapo wa kutosha tu na hata ukoo wa Chifu Mkwawa kwa dini ni Waislamu.
Ongeza na wafipa
 
Mnyakyusa kuitwa juma sio usisalamu wapp kibao afu wakristo na nadhani hata andambwile ni mkristo
 
Ukimwona mnyakyusa shekhe, kuna pesa ya uhakika hasa, ameifuata. Hawaendi kwa imani, wanafuata pesa. Ni kama Mwaipopo, hakuna uislam wala ushekhe pale, alifuata pesa. Mtu anatangaza kusilimu leo, mwezi ujao anakuwa shekhe. Mwaipopo alichukuliwa wakati ule wa Mwinyi, walipoingia wale wa itikadi kali.

Wahaya, kuna maeneo kumekuwepo na waislam wengi kiasi. Wakati ule Rugambwa wa kwanza akiwa kadinali, Hemed bin Juma bin Hemed alikuwa mufti wa Tanzania, na wote walikuwa wanatoka Kagera. Mikoa ya bara karibia yote, ukiondoa mikoa kama Tabora na Kigoma iliyokuwa vituo vya waarabu kununulia watumwa, iliyobakia ina idadi ndogo ya waislam, bila ya kujali ni kabila gani.
Ndiyo mara nyingi uwa waislamu wa mchongo walio tengenezwa na serikali kwa kazi maalumu..kama sasa walivyo tengenezwa wakatoliki wa mchongo wanaofanya maandamano bila ya kupigwa risasi wala vibari na awashitakiwi na yoyote...hao mashekh wakina mwaipopo ni bidhaa za serikali siyo dini ....wapo kwa kazi maalumu.
 
kama tu tunaambiwa uislam ulitengenezwa na vatican basi kwa mtindo huo serikali haishindwi kutengeneza waumini feki wa dini yoyote ikiamua kufanya hivyo kwa maslahi yake
 
kama tu tunaambiwa uislam ulitengenezwa na vatican basi kwa mtindo huo serikali haishindwi kutengeneza waumini feki wa dini yoyote ikiamua kufanya hivyo kwa maslahi yake
Mbona kwa tanzania imekuwa ni kawaida ...bakwata yote ipo kwa ajili ya serikali siyo dini wala uislamu na kuna mashekh wasio bakwata wengi tu ni mapandikizi ndani ya uislamu...asilimia 70 ya mashekh wakubwa tz ni mapandikizi...hata kwa wakristo mapandikizi yapo mfano mwamposa nk yaani viongozi wa dini wanao tumika kwa mlango wa NYUMA NA WAGIZA WA SERIKALI
 
1. Wachaga - kumkuta mchaga muislam labda kwa mbali sana awe wa machame
2. Masai
3. Wakinga
4. Wangoni
5. Wajita
6. Wagogo

Wanyakyusa hapo zamani na wao ilikuwa ni nadra sana lakini sikuhizi imeanza kuwa kawaida utawakuta Mashehe kina Mwaipopo, wachezaji kina Azizi Andambwile, makocha kina Juma Mwambusi, na mitaani wapo wenye majina yote ya kiarabu.

Wakurya nao sikuhizi utawakuta waislam kina Mohammed, Abdallah, n.k.

Wapare ni kawaida sana kuwakuta waislam.

Wahehe wa Iringa waislam wapo wa kutosha tu na hata ukoo wa Chifu Mkwawa kwa dini ni Waislamu.
Lengo kuu la dini na waleta (waanzisha) dini hapa duniani mathalani huku Africa ilikuwa ni kutawala (Kupitia dini mtu anakutawala kiakili(fikra(saikolojia))).

Na ndio maana ukiangalia makabila yaliokuwa na uhusiano na waarabu kipindi cha ukoloni yalikua sio ya kawaida ni yalikua makabila yenye nguvu na ushawishi na au yamekaa strategically kijiografia...

Mfano Mtwa Mkwawa aliekua Chief wa WAHEHE huyu alikua na Nguvu na serikali yake ilikua na mtandao mkubwa kijiografia hapa Tanzania.... Mtandao wake ulikua una-block major routes zilizotakiwa kutumiwa na waarabu kipindi hiko.

Kwakua Mkwawa alikua ni mtu wa diplomasia ilikuwa ukishindwa kuelewana nae kidiplomasia basi damu inamwagika.

Waarabu walikuwa wajanja walimfuata Mkwawa kwa amani na kwa ushirikiano zaidi(diplomasia) Mkwawa akakubali kushirikiana nao.

Mkwawa kuwakubalia wa arabu na kupokea utamaduni wao ni kosa kubwa la kiutawala hadi apo alikua ameshafeli tayari, hata angewashida wajerumani isingekua na afya kwani tayari alikuwa mtumwa wa waarabu, na Jamii zote za kanda ya kati na nyanda za juu kusini zingeacha ukuu wao(utamaduni wao) na kuwa waarabu.

Mkwawa alikua mtu makini ila kitendo cha yeye kua mtu wa dini aidha Ukristo au uislamu alikosea pakubwa na aliwakosea sana wahehe.
Ila yote ya yote usilolijua ni sawa na usiku wa giza.
 
achaga upotoshaji we mjuba, wale wa mwembechai walikuwa walevi wa uislam waliokuwa wanaharibu mali za watu kisa tu imani yao. Utaendaje kuvunja bucha za nguruwe biashara za watu? Kuna wakristo huwa hawapendi pombe lakini hawaendi kuvunja mabaa ya watu, hawavuti sigara lakini hawaendi kuharibu mashamba ya tumbaku na kuvunja kiwanda cha sigara na bia. Nyie ni wapumbavu na wajinga, dini imewalevya mpaka mnapandisha mizuka kuharibu mali za watu
Kadhia ya mabucha ya nguruwe ilikua ni 1991 kipindi cha mwinyi,na ilikua kigogo siyo mwembechai,baada ya mkiristo mpumbavu kumuuzia mtoto wa kiislam nguruwe badala ya ng'ombe
Kadhia ya mwembechai ni 1998 kipindi cha mkapa, baada ya padre kwenda kushitaki polisi /mkuu wa mkoa kuwa yesu anatukanwa
 
ndio walio impose uislam kwa machifu na watemi and then zile chiefdom zao zikawa islamized na matokeo tunayaona leo walikopita waarabu
Wali impose vipi uislam kwa machifu bila mamlaka?..mkwawa alisilimu mwenyewe,ntemi wa unyanyembe alisilimu mwenyewe
 
hao ni wanyaturu wa kaskazini mwa singida, ilongero huko kuna waislam kwa kuwa waarabu walipitapita huko. Singida kusini waislam ni wachache. Singida mjini kwenyewe tu wakristo ni wengi kuliko waislam, angalia makanisa yanauyojaza nyomi ndio utajua wingi wao
Singing mjini wakristo wengi!?😃😃 Singida mjini ni mji wa wanyaturu,mapema 2000s maofisa wa serikali hawaitishi watu ijumaa sababu hakuna atakaekuja,kujaza kanisa la watu mia mbili siyo issue kwenye mji wenye watu laki kadhaa
 
Mbona kwa tanzania imekuwa ni kawaida ...bakwata yote ipo kwa ajili ya serikali siyo dini wala uislamu na kuna mashekh wasio bakwata wengi tu ni mapandikizi ndani ya uislamu...asilimia 70 ya mashekh wakubwa tz ni mapandikizi...hata kwa wakristo mapandikizi yapo mfano mwamposa nk yaani viongozi wa dini wanao tumika kwa mlango wa NYUMA NA WAGIZA WA SERIKALI
hii ndio ile dhana kwamba dola ni kubwa mpaka kwenye dini ipo! Kuna watumishi wa mungu ukiwagusa utakuwa umeigusa serikali, kumbe ni watumishi wao na ndio maana wakifa serikali kama yote hujaa misibani kwao kwa kutoa heshima za mwisho. Na hao viongozi wa dini hawataki uiseme serikali vibaya utagombana nao
 
Kadhia ya mabucha ya nguruwe ilikua ni 1991 kipindi cha mwinyi,na ilikua kigogo siyo mwembechai,baada ya mkiristo mpumbavu kumuuzia mtoto wa kiislam nguruwe badala ya ng'ombe
Kadhia ya mwembechai ni 1998 kipindi cha mkapa, baada ya padre kwenda kushitaki polisi /mkuu wa mkoa kuwa yesu anatukanwa
shukrani kwa kuweka kumbukumbu sawa, vipi kuhusu yule mwislam aliyeitwa Dibagula, yeye alifanyaje na kesi yake iliishaje?
 
Ukimkuta MSUKUMA Mwislamu ujue huyo amefuata au amepelekwa huko na Majini. Si mnawajua Wasukuma kwa kupenda ushirikina? Sasa wakibobea sana katika ushirikina hupata majini ambayo ili yawape nguvu zaidi yanawalazimisha wawe Waislamu.
 
shukrani kwa kuweka kumbukumbu sawa, vipi kuhusu yule mwislam aliyeitwa Dibagula, yeye alifanyaje na kesi yake iliishaje?
Dibagula alikua mhadhiri wa ulinganifu,akisoma biblia,alishitakiwa kwa kusema yesu siyo Mungu,alishinda kesi, maana hizo kesi za yesu siyo Mungu mlalamikaji alikua serikali
 
Mnyakyusa kuitwa juma sio usisalamu wapp kibao afu wakristo na nadhani hata andambwile ni mkristo
Juma Mwambusi aliewahi kuwa kocha wa Yanga na Mbeya city ni Mnyakyusa na kwa dini ni Muislam tena swala tano
 
Back
Top Bottom