MRS MTABA,
naomba nikutahadharishe pia usije ukawa unaapply directly solutions zinazotolewa na wanawake humu jamvini! watch out. most of them sio wanawake. hata kama ni wanawake wamepinda sana
This is a very serious allegation. Tuwe makini na kauli zetu, zinakuwa too general na zinaelekea kutukuza mfumo dume. Je, wewe umeishakutana na hao "most" uka-prove kwamba sio wanawake?
Wewe ungekuwa ni mmoja wa akina dada/mama hapa jamvini ungejisikiaje kwa kusoma such a sweeping statement?
Hivi kuna mahali kwenye majina yetu kunaonyesha gender/sex? Je, umejuaje kwamba hao "wanawake" most of them sio wanawake? Kwa kuwa umeishaweka label kwamba most of them sio wanawake, je, una uhakika Mrs Mtaba ni mwanamke?
Kipimo cha kupinda michango yao hao wanawake ni nini? Je, hakuna members wenye majina ya kiume ambao hutoa michango iliyopinda?
Ushauri kupinda ama kutopinda inategemeana na mtoa ushauri amekutana na yepi katika mahusiano/ndoa yake. Wengine wanaamini jino kwa jino (kama Mrs Mtaba), wengine wana amini ukipigwa shavu la kulia unageuza na la kushoto lipigwe. Sasa ushauri upi uliopinda? Kila mtu anaangalia experience yake na ndipo anatoa ushauri.
There is no universal solution in marriage problems, solution ya Mrs Mtaba inaweza ku-work kwake, lakini isi-work kwa mtu mwingine. Wanaume wengine ukiwageuzia shavu la pili, atakuzabua kibao na baada ya hapo atapiga mateke kabisa. Mwenye experience mbaya kiasi hiki lazima ataonekana amepinda sana kwa kuwa alikutana na mume/bf jambazi na akamfundisha ujambazi pia. Wanaume wengine wanaweza ku-cheat kwa "kupitiwa na shetani" na akigundulika harudii tena, so ukiweka jino kwa jino utakuwa wrong. Mioyo ya binadamu ni vichaka you will never know what they are up to, na hivyo sometimes solutions zinakuwa ni kama pata potea, maana hujui kiini cha tatizo ni nini, sawa na kwenda kuagua kwa mganga wa kienyeji.
Nadhani kila memba ana haki ya kuchangia hoja/mada na ni juu ya muomba ushauri kuchagua achukue ushauri upi.