Imekaaje hii!
Mrs Mtaba
14th April 2009, 08:51 PM
Za leo wana jf, jamani leo nilikuwa nagombana na Mr. kuhusu swala fulani hivi la mimi kwa kuwa sijawa na kazi bado kutokana na kwamba ni lazima nijue hii lugha ya wa denish ndipo nipate kazi nzuri...kwa kweli maisha yetu yamekuwa ya misukosuko sana kwa kuwa kipato nikidogo kumpelekea mpaka kushindwa kulipa bills zingine...hata hela yamatumizi yangu hushindwa kunipa.
Sasa nilikutana na buzi moja la kiarabu halina mke wala nini...limenipenda sana na linataka mahusiano nami...nikamwambia mimi nimke wa mtu...akasema poa tuu, akanipa mbinu kuwa tufanye kama naenda kumfundisha kimombo then tuendelee na mambo yetu...Nimemdokezea Mr. hili kawa mkali kweli...ila sasa cha ajabu mr. akaniambia eti aje nimfundishe hapa home...sasa nauliza hivi je nimefanya kosa kusema hivi, na je ningesemaje.