Imeshindikana vipi kuwapa tenda DP world au shirika lingine kuwa train kwa vitendo watanzania kusimamia bandari kwa miaka miwili kisha wao kuondoka?

Imeshindikana vipi kuwapa tenda DP world au shirika lingine kuwa train kwa vitendo watanzania kusimamia bandari kwa miaka miwili kisha wao kuondoka?

Kwa mfano hata Mwarabu akitupa mgao wetu wa Bandari hizo fedha zitakuwa zikipigwa juu kwa juu, na CAG atakuwa daima analalama tu kila siku, ndio maana mimi I don't care about mkataba ninachoangalia ni mizigo ikiwa mingi local economy itafaidika.
 
Umesema ukweli jambo muhimu ni kuboost local economy ili muzunguko uwe juu, biashara iwe rahisi kufanyika dollar ishuke pesa yetu ipande thamani, ila kuhusu government revenues tuachie wenye mamalaka waendeshe v8 zao wajenga majumba waende tuwa za nje nk.
 
Umesema ukweli jambo muhimu ni kuboost local economy ila muzunguko iwe juu, ila government revenues tuwachie wenye mamalaka waendeshe v8 zao wajenga majumba nk.
Hata fedha za Migodi zimejengewa Airport maporini wakati Uwanja wa Ndege wa Bukoba hata taa hauna, wanaenda kununua Madege makubwa huku wanajua kabisa kuwa soko la usafiri wa anga hatuliwezi ndege zinapaki wanaagiza zingine wanachojali ni upigaji..
 
Barabara anapewa mkandarasi
Airport kujengwa anapewa mkandarasi
Bandari imejengwa na wakandarasi
Bunge limejengwa na wakandarasi

Sisi watanzania tumelewa na vyakupewa na kufanyiwa ifike muda tufanye kila kitu wenyewe.
Ikulu tulijenga wenyewe na inahadhi ya kiwango cha kupigiwa mfano mnaita kimataifa. Madini tumeshindwa kuwekeza, gas tumeshindwa, makaa ya mawe tumeshindwa hata bandari tumeshindwa kisa uvivu, mawazo mgando na roho ya kushindwa, wizi (umimi) na kutojitoa kwa ajili ya wengine.
 
Wapo maprofesa wenye kujua sehemu mbali mbali ila ndo wakwanza kwa wizi wa mali zetu.

Acheni wafanye kazi tupate commission. Maana wabongo ni wezi sana.
 
Wao wamefunzwa namna ya kusimamia bandari, hiyo knowledge yao imeshindikana kuihamisha kwa watanzania nasi tuweze kusimamia bandari yetu?

Waletwe hapa wakae hata miaka miwili na kisha waondoke, pakitokea tatizo wawe wanakuja hata kwa wiki wanarudi kwao.

Haya mambo kwa jinsi yalivyo kwa kujenga utegemezi kwa watu wengine wasimamie nyumba yenu ndio yanayotufanya waafrika siku zote kuonekana tabaka la chini kiasi cha kushindwa kujisimamia.
Wabongo ukiwaachia kitengo wanawaza upigaji kupeana tenda na kuweka ndugu zao kitengo........ Acha ipite kama miaka 20 wabongo watakua na akili za kuwajibika,,, kuna kizazi cha wapigaji lazima kipite kwanza
 
Watanzania hawawezi endesha kitu
Angalia TTCL, TRC, ATCL, DAWASA

Kisha angalia

Azam, METL, Azania, GSM,
Raia wengi tu wangependa kuona kampuni binafsi zikiendesha sekta nyingi katika nchi, sio bandari tu bali hata TANESCO, treni, stendi za mabasi, masoko n.k kinachopigiwa kelele hasa ni terms za mikataba na hao wawekezaji na jinsi mchakato ya ubinafsishaji inavyopelekwa na kuacha maswali mengi zaidi yasiyojibiwa.
 
Watanzania hawawezi endesha kitu
Angalia TTCL, TRC, ATCL, DAWASA
Huu ni usemi wa kipumbavu. Kwa nini unataja Watanzania badala ya genge lilillong'ang'ania kwa nguvu uongozi wa taifa hili kwa miaka nenda rudi? Genge ambalo limejimilikisha hatma ya nchi kwa mabavu kwa miaka nenda rudi.

Usithubutu kuwabeza wala kuwaonea Watanzania kwa ujumla wao kwamba hawawezi kuendesha taasisi hizo. Wapo Watanzania huko nje ambao wamefanya makubwa kwenye taasisi za nje ya Tanzania na kujizolea sifa kemkem katika utendaji wao.

Kuna tatizo kubwa hapa ndani ya nchi. Taifa liko mikononi mwa genge la wezi, genge la wanyang'anyi, genge la wala rushwa na genge la walafi. Mpaka hapo Watanzania watakapochukua hatua kuondokana na hili genge hatutoboi.

Kwa huu mkataba hilo genge linahalalishiwa ulaji ambao uko nje ya uwezo wetu kuushughulikia hata tukiugundua. Kuna watu binafsi watapokea mamilioni kwa mabilioni kupitia huu mkataba. Adui yetu namba wani ni CCM, zimwi tunalolilea sisi wenyewe!

Mtu makini ukipewa saa moja ya kutatua tatizo, tumia dakika 55 kutafakari na kujadili shida zilizopo halafu dakika 5 tu kutoa suluhisho. Nakuapia CCM hutumia dakika 5 tu kukufikiria shida zilizopo lakini dakika 55 kujadili maslahi bonafsi.

HIMARS, you cannot solve a problem from the same mind-set, same thinking and same consciousness that created it. You must learn to see the world anew.
 
Yaani Dpworld badala ya afanye biashara aje afanye trainings....
Alikwambia Nani wao Dp world ni training centre??

Watz wengine cjui tunawaza nn [emoji23][emoji23][emoji23]licha ya Training hata hio ela ya kujenga tunayo
 
Mijitu mingi inayolalalma humu inafikiri hao Dp world ni kikundi cha waarabu wawili watatu...
Ukiwaambia mbona wanaendesha bandari USA Hadi China na ujerumani na UK...hawanga majibu

Wa tz ni rahisi kuchotwa akili.hasa pale anapoambiwa kaibiwa hua tunajidai wazalendo na kutetea hata tusichojua ..nchi imejaa wapuuuzi
 
Hata fedha za Migodi zimejengewa Airport maporini wakati Uwanja wa Ndege wa Bukoba hata taa hauna, wanaenda kununua Madege makubwa huku wanajua kabisa kuwa soko la usafiri wa anga hatuliwezi ndege zinapaki wanaagiza zingine wanachojali ni upigaji..
Hayo yote kuafaida mpaka ya pewe wawekazeji wa nje uzoefu wa hio biashara soon au later ATCL ndo shirika lingine litakalo kabidhiwa kwa wawekezaji, kwasbb halileti faida kwa taifa zaidi ya hasara kila mwaka .......Tanzania hatuna wizara ya economic strategic planning, ukijiuliza kwanini mwenda zake kwa kamwanga zaidi ya 2trion shilling kwenye shirika la ndege lisio leta faida kwa taifa. Hiyo pesa ingewekezwa kwenye agriculture schemes tungekua mbali
 
Wao wamefunzwa namna ya kusimamia bandari, hiyo knowledge yao imeshindikana kuihamisha kwa watanzania nasi tuweze kusimamia bandari yetu?

Waletwe hapa wakae hata miaka miwili na kisha waondoke, pakitokea tatizo wawe wanakuja hata kwa wiki wanarudi kwao.

Haya mambo kwa jinsi yalivyo kwa kujenga utegemezi kwa watu wengine wasimamie nyumba yenu ndio yanayotufanya waafrika siku zote kuonekana tabaka la chini kiasi cha kushindwa kujisimamia.
Sababu zake ni hizi kama ifuatavyo:

MOSI: Ni kwa sababu kwa sasa tunapata takribani tuseme TRILLION X kutoka Bandani wakati wao wakija, tutaptya possibly zaidi ya mara kumi (10X) ya hizo huku na wao wakipata pia

PILI: Katika hali ya kawaida, Serikali huwa haifanyi biashara na hivyo haina SPECILALIZATION kwenye eneo fulani la biashara. Kwa hiyo chances ni kwamba DP WORLD wakitu-train na kutuacha tuendelee, pato letu bandanrini linaweza kupanda labda kutoka X na kufikia 5X na si 10X kama inavyokisiwa sasa

TATU: DP WORLD wao ni Kampuni ambayo IME-SPECIALIZE kwenye maswala haya ya Bandari katika ngazi ya KIMATAIFA. Watakapokuja kuwekeza na kupandisha pato letu bandarini hadi kufikia 10X, hapo hapo na wao pia watakuwa wanapata faida kwenye uwekezaji huo

  • Kwa hiyo kwa kifupi, DP WORD wakiwekeza, sisi tutapata 10X badala ya X ya sasa, na wao pia watapata
  • DP WORD wasipowekeza, tutaendelea kupata X kutoka bandarini
  • Aidha DP WORD wakitufanyyia trainining tu bila wao kuwekeza, pato letu bandanrini linaweza kuwa tuseme 5X badala ya 10X
Na kwa sababu wewe pia unajua kuchagua, nadhani unaweza kusema ni optioni ipi kati ya hizi tatu ambayo inaweza ikatufaa zaidi
 
Ndio imeshindikana Sasa kwani hiyo Bandari si imekuwa inasumbua sua kwa miaka zaidi 60 Sasa hakuna jipya?

Kwanza Kuna sekta gani ambayo Tanzania inafanya Kwa ufanisi? Kuanzia sekta za biashara Hadi Huduma za jamii ni hovyo tuu..

Kote huko Kuna Wataalamu waliobobea ila hulka na tabia za Watzn ndio shida tupu.
Upigaji !
 
Sababu zake ni hizi kama ifuatavyo:

MOSI: Ni kwa sababu kwa sasa tunapata takribani tuseme TRILLION X kutoka Bandani wakati wao wakija, tutaptya possibly zaidi ya mara kumi (10X) ya hizo huku na wao wakipata pia

PILI: Katika hali ya kawaida, Serikali huwa haifanyi biashara na hivyo haina SPECILALIZATION kwenye eneo fulani la biashara. Kwa hiyo chances ni kwamba DP WORLD wakitu-train na kutuacha tuendelee, pato letu bandanrini linaweza kupanda labda kutoka X na kufikia 5X na si 10X kama inavyokisiwa sasa

TATU: DP WORLD wao ni Kampuni ambayo IME-SPECIALIZE kwenye maswala haya ya Bandari katika ngazi ya KIMATAIFA. Watakapokuja kuwekeza na kupandisha pato letu bandarini hadi kufikia 10X, hapo hapo na wao pia watakuwa wanapata faida kwenye uwekezaji huo

  • Kwa hiyo kwa kifupi, DP WORD wakiwekeza, sisi tutapata 10X badala ya X ya sasa, na wao pia watapata
  • DP WORD wasipowekeza, tutaendelea kupata X kutoka bandarini
  • Aidha DP WORD wakitufanyyia trainining tu bila wao kuwekeza, pato letu bandanrini linaweza kuwa tuseme 5X badala ya 10X
Na kwa sababu wewe pia unajua kuchagua, nadhani unaweza kusema ni optioni ipi kati ya hizi tatu ambayo inaweza ikatufaa zaidi
Tatizo letu sio kuwa watu hawakuwa trained kwa hizo kazi bali watu sio waadilifu tu !!
 
Back
Top Bottom