Imetafsiriwa na Derrick Gasper Mkandara Rufufuuuuuu

Imetafsiriwa na Derrick Gasper Mkandara Rufufuuuuuu

wapeeenziii watazamaji ndugu zangu wapendwa,mkandala lufufu iliyopo yombo kwa limboa kwa mara nyingine tena inawaletea muvi kali kabisa ya cyborg
ambayo imetafsiriwa na capten derick gaspaer mkandala lufufuuuuu wako mabameja
 
Kuna movie ya shozniga( ehh natumai mmeelewa) huyu Rufufu mbwembe zilizidi. Mtu kasema “don’t touch me!” , yeye mtafsiri “ usinishike, usinishike utanichania chupi yangu” hadi leo sipendi muvi za kutafsiri, naona zinapunguza IQ kiaina
 
Ila lufufu kwenye fani ni Kama Bob Marley na reggae jamaa kahasisi fani ya utafsiri movie.

Maneno Kama Kanyabazongo... Kaliiinya!..
Kalinya mpaka leo nalitumia...kuna maneno mengi sana.Mjusi Konkobe 😀 😀 😀 😀

Nilisumbua sana kutoroka Shule kwa ajili ya Mkandara
 
Enzi hizo ulikua ukisikia "Wapeeeenzi watazamaji ndugu zangu wapendwa, mukandara rufufu videotek iliyopo katika jiji la daresalama inakuletea muvi ya Masokorindo (Deadly Prey)"

Kinachofuata hapo ni uongo uongo tu kwenda mbele halafu mwisho anamalizia "Imetafsiriwa na Rufufuuuuuuuuu Rokobhambabheja"😅😅

Jamaa alikua anatfsiri uongo sema anainogesha muvi hadi unaipenda. Kuna muvi moja jamaa alisema Get out Rufufu akasema "Nitakumaliza mara moja"😂

View attachment 1992356
Yule alikuwa ni Kaptein wa jeshi JWTZ,mstaafu,muvi za kivita alikuwa anazielewa vzr,na kizungu Ili ukitafsiri vizuri,usitafsiri neno kama neno moja kwa moja,utapoteza maana.

Mfano kwa kizungu mtu akisema"At the end of the day,if we don't get the cure,we will all die"Hilo neno "end of the day"tafsiri yake kwa kiswahili sio mwisho wa siku,hapo tafsiri mujarabu,ni "tusipopata hii Tiba,mwishowe wote tutapoteza maisha.
Au neno "breaking news"tafsiri yake sio habari mpasuko,

Hapo inabidi utafsiri maana ya ndani,concept,tafsiri sahihi ni "habari zilizotufikia hivi punde.
 
Back
Top Bottom