Imetafsiriwa na Derrick Gasper Mkandara Rufufuuuuuu

Imetafsiriwa na Derrick Gasper Mkandara Rufufuuuuuu

Rufufu mukama wa bambeija (mfalme wa koo ya bambeija) ndiye nilikuwa namwelewa enzi hizo.

Kwasasa movie iliyotafsiriwa kwa style hiyo siwezi hata itazama unless iwe imefanyiwa professional dubbing kama wanavyofanya azam.
 
Kama unajua Kihaya huyo Mkandara alikuwa anatumia Kihaya kwenye movie zote.

Kalinya
Nyugunyu
Mwani
Masokolindo
 
Hiyo Baby's Day Out alifanya poa sana. Kuna sehemu yule mama kibonge mwenye maziwa makubwa alishuka kwenye gari akampakia mtoto bila kujua. Hapo Lufufu akasema "Belinda, mamaa alimaarufu kama Kibele Kyokya" [emoji23][emoji23]
 
Kanyampasila -lock up/gereza
Mpurutulizo -kamba
Mbariga -miguu
Mkuku mkuku -haraka haraka
Msobe msobe -ile unambeba mtu kibabe babe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]




All in all, usiombe ukutane na Dj Afro ametafsiri movie ya Jack Chan
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwenye we are solders alisema eti ukisikia risasi imekunasa unarudi nyuma kinyeng’enyuu unaanguka kinyangaramila ndio inakuwa mwisho wako
 
Enzi hizo ulikua ukisikia "Wapeeeenzi watazamaji ndugu zangu wapendwa, mukandara rufufu videotek iliyopo katika jiji la daresalama inakuletea muvi ya Masokorindo (Deadly Prey)"

Kinachofuata hapo ni uongo uongo tu kwenda mbele halafu mwisho anamalizia "Imetafsiriwa na Rufufuuuuuuuuu Rokobhambabheja"😅😅

Jamaa alikua anatfsiri uongo sema anainogesha muvi hadi unaipenda. Kuna muvi moja jamaa alisema Get out Rufufu akasema "Nitakumaliza mara moja"😂

View attachment 1992356
He was so talented
 
Naam kupitia yeye watu wamejiajiri wengi sana. Shida rufufu alikua anatafsiri muvi za kichina na kivita tu tena zile za zamani kabisa. Unaweka li VHS lako hapo linakoroma balaa kwaliti mbaya
Utakuwa wa juzi wewe mkuu...Zamani hizo VHS ndo zilikuwepo peke yake.

Rufufu alitisha sana, alikuwa anajua sana, huwezi mfananisha na watafsiri wa siku hizi.Nasikia alifariki (RIP) Thats why Muvi mpya hajatafsiri.
 
Capt Derick Gaspar Mkandala ajengewe sanamu lake nitachangia mifuko 50 ya siment
 
Huu uzi nimecheka sana, lufufu alikua anajua alaf anajua tena
 
Back
Top Bottom