Ingekuwa kwa wenzetu serikali nzima ingeachia ngazi. Huwezi kuachia watu watumia dawa then baadae ndio unasema ni utapeli!
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="colspan: 5"]Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Watanzania wengi wamekuwa na mila potofu wengine wamekuwa wakitumia dawa za kuongeza umri wamekuwa wengi hasa wa vijijini wamekuwa wanakimbilia kwenye Kikombe cha Babu. Je, Waziri ananihakikishiaje kuwa Dawa ya Babu inatibu Ugonjwa wa UKIMWI moja kwa moja?[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="colspan: 5, align: left"]
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 78 SESSION # 3 [/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 5"][TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="width: 10%"]
[/TD]
[TD="width: 90%"]
Answer From Hon.Mponda, Dr. Hadji Hussein
HEALTH AND SOCIAL WELFARE [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 5"]WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:
Mheshimiwa Spika, Kikombe cha Babu kama kinavyojulikana Babu wa Loliondo, hadi sasa bado tunakifanyia utafiti ili kutoa jibu kwamba kile Kikombe kimoja cha Babu kinatibu magonjwa yale matano ambayo Babu amedai anatibu. Taarifa tulizozitoa mwanzo kwa Watanzania, tulijibu swali la kwamba, dawa ile ni salama kwa matumizi ya afya ya binadamu na haina sumu. Tumewaambia Wananchi kwamba, kwa kile Kikombe cha Babu, anachokitoa ambacho anachemsha kilo tatu za ule mzizi ndani ya maji yali lita 60, bado imedhihirisha ni salama haina madhara.
Hivyo basi, tunaomba Wabunge mpeleke taarifa kwa Wananchi kwamba, wavute subira, tunaendelea na utafiti ambao tunahusisha na wagonjwa pia ambao tayari wamepata Kikombe cha Babu ili tutoe jibu kama kile Kikombe kinatibu yale magonjwa matano. Ninashukuru.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Source:
Parliament of Tanzania