Binafsi ntajitolea kumtetea babu huyu kwa sababu zifuatazo
1:Serikali imeshindwa kuwatimizia wananchi mahitaji yao mpaka wanahangaika kutafuta tiba mbadala.
2;Uchumi wa samunge umepaa, kwani ikumbukwe hata barabara ilikua hovyo
3:Mawasiliano yameimarishwa ,saa hizi samunge unatwanga kotekote
4:Vijana walijipatia ajira na kutengeneza mitaji
5:Viongozi waliwashawishi wananchi waende kupata kikombe wakati wakijua wao Role models
6:Babu Alisema wazi wenye Imani ndio watapona,Hivyo imedhihirisha wananchiwengi wa TZ hawana Imani:Mf; Nna rafiki yangu yeye ni mgonjwa wa kisukari,aliniambia hajapona sukari,ila maumivu aliyokuwa akiyapata mwanzo,hadi leo hii hayapo tena.Pia kuna watuwengine waliniambia,wakiwa na wake zao Vigongo vyao vimeongeza performance mara dufu.Hivyo inaashiria hawa walinda na Imanio Haba kujaribu.
7:Babu aliwashauri pamoja na dawa yake waendelee kutumia na hizo nyingine hadi unapopita muda,wao wakaacha.Hilo la kuvunja masharti tu,watu waliisha haribu dozi.kwani hata hizi za kitaalam zina masharti pia.huwezi pewa dawa ya siku saba,wewe ukanywa sikumbili au tatu ukaacha utegemee kupona.
8:serikali ilinufaika na biashara ya utalii,na fedha za kigeni kwani wateja wa nje ya nchi pia walikuja samunge.
9:tuliweza kufahamu juu ya ile nchi ya waarabu iliyopo pale Loliondo,kupora rasilimali zetu.
10:watanzania waliweza kufanya Utalii wa ndani ambao,umekuwa ni adimu kwao.
11:CCM walinufaika na kupungua kwa mjadala,wa Dowans na Uchaguzi, hivyo wao wanapaswa kuwa wa kwanza kumtetea na ndio wamenufaika zaidi.lakini kama ilivyo ada kwa CCM wakiisha kutumia hawana haja na wewe,kwani wao huamini kuwa"Mavi ya kale hanuki"
n.k,n.k
My take;Mema aliyofanya babu ni mengi kuliko hata mabaya ,mbayo kwanza naami hayapo,zaidi tu ya ya ile foleni ya kihistoria.