Imetosha Kikwete Kusemwa, Mlitaka afanyeje?

JK alisemwa kwenye msiba wa Magufuli na Sasa wa Lowassa ajitafakali
 

Noted
 

Street words
 

Hawezi

It was team work .
 
Kuna mtu anamlaumu Kikwete kwa kumkata Lowasa kwenye uraisi mkuu? Hoja inayojengwa ni Kikwete kuwa mnyima wa fadhila alizopata kwa Lowasa hata kufikia kuwa raisi. Alikuwa na nafasi ya kuendelea kutunza urafiki wao bila kuhusisha na nafasi za uongozi wa nchi. Hili la kuongoza nchi sio jambo la kirafiki, ni jambo la mtu mmoja mmoja. Kuna taarifa kwamba baada ya mwenzake kukiuzulu katika skendo ambayo ilisukwa vizuri ikasukika, JK aliamua kuwa adui wa kudumu wa Lowasa na kupambana naye hata nje ya mfumo. Jamaa hata wakati ndugu yake na rafiki yake huyu akipitia magumu hakuwahi angalau kwenda kumpa pole ya afya. Hii roho ngumu na mbaya ndicho wanachohoji watu na Wala sio mambo ya uraisi.
 
So what ? Ni lazima kufanya hivo ?they were never friends , ni watu wanaofahamiana tu .

Sio lazima kumjulia hali, kuna sheria inasema ni lazima aende?

Msilazimishe vitu ambavyo HAVIPO
Lowassa was not a saint , ni mtu kama watu wengine
Kanuni ya mahusiamo ya kijamii inakataa maandishi yako haya. Pole sana Jk. Yaani mtu unayekiri alikuja nyumbani kukushawishi ugombee uraisi anaumwa alafu usio haja ya kwenda kumpa pole kweli?
 
Hayo ni maneno ya siasa

Hakuna ushikaji wowote kati ya Edo na JK

NDIO nakupa siri

Rafiki wa kweli ule wa kiushikaji kabisa wa long time wa JK ni Ditopile tu

Huyo ndio rafiki wa kweli waJK
Mkuu mbona unakana kauli zako mwenyewe. Ziko clips kibao Kikwete akikiri kwa kinywa chake kwamba lowasa likuwa zaidi ya ndugu kwake.
 
Nadhani baadhi ya watanzania hasa hili kundi la mitandaoni hawako objective na hawajielewi wanataka nini.

Nj watu wa mihemko na matukio. Hawana kumbukumbu, hawana kanuni Wala itikadi wanayoiamini!
Kila kinachopumbaza nafsi zao Wanakiendea.

Kundi hili lina-mmiss Magufuli, LAKINI wkati huo huo linajifanya kulaani kukatwa kwa Lowassa.

Hivyo vitu ni mutually exclusive! Huwezi vipata vyote!
Magufuli na Lowassa wasingeweza kuwa Marais wakati mmoja!
Mnajufanya kuchukia ufisadi, halafu mnamkumbatia fisadi namba 1 according to CHADEMA's list of shame!
Enyi wehu nani amewaroga?
 
Umesema kweli. Hata mimi nimetoka mbali na mwendazake edo. Urais sio kitu utanunua au kupata kishikaji. Jk tumwache badala yake tumpe pole na pongezi.
 
Sasa wewe ndo msemaji wa kikwete au? Kama familia ya Edo inamwona kikwete kuwa ni msaliti na ika mnyima fursa ya kutoa neno msibani wewe N nani ubishe harafu unaumia nini kikwete akisemwa,? Kama ufisadi wote walikuwa wezi na mafisadi wakubwa . Ila kikwete ni msalitiiiii
 
Yaani nyinyi wapambe wa Lowasa mmeshafanya Urais ni cheo cha kupeana kiushkaji. Kwamba mtu akiwa rais basi akitaka rafiki, ndugu au mtoto wake awe rais, lazima itokee. Kwa mtazamo wenu Kikwete alimtaka Membe awe Rais, mbona Membe hakushinda hiyo nafasi ya kugombea Urais?

Tuambieni hapa chanzo cha utajiri wa kutupwa wa Lowasa ambaye alikuwa ni mtumishi wa uma ni kipi? Tuambieni huo usafi wa Lowasa ni upi? Yaani hii nchi kuna hulka ya kijinga sana ya wengi kuwa wapambe wa viongozi bila ya kuweka mbele maslahi ya Taifa letu. Tunajua viongozi wengi wa CCM ni wezi na wengi hugombea hizi nafasi za juu ili wajitajirishe na kutajirisha watu wao wa karibu.
 


Huyu mwandishi yeye anao ushahidi usio na shaka kwamba Family iliondoa jina?
 
Uko sahihi Mkuu!
Nadhani wamwache Mzee wa Msoga astarehe!
Nimpongeze kwa uvumilivu wake!
Alipokuwa Rais alisemwa kwa mengi, kwenye kifo cha JPM walimsema sana!
Na sasa kwenye kifo cha ENL wanamsema tena!

Jamani mwacheni astarehe kwa amani!
Rais anachaguliwa na Mungu hachaguliwi na mwanadamu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…