Imewahi kukutokea ukazidishiwa hela ulipoenda kutoa pesa? Ulichukua hatua gani?

Kuna jamaa nimeenda dukani kwake duka la Mpesa aniwekee sh 4100 ameniongezea sifuri moja!

Siyo mara moja wala mara 2 ni mara kadhaa. siku ya 31/12/2024 tu nimeenda sokoni kununua vitu sokoni mama mmoja akanizidishia 2000 bahati mbaya hapo sikuhesabu ila baada ya hatu kama saba amatisa nikajua mama huyu kanizidishia 2000 nikarudi.

Nikamuuliza maam nimekupa sh10k nikanunu vitu vya 4000 mbona umenirudishia 8000 badala ya 6000?
nikampa akasema basi nimeamini mtu akitenda mema hulipwa mema asubuhi pia kuna mtu alisahau hela yake hapa mezani nikaiona ameenda kama lisaa ndo anarudi nikampa asante sana baba. nikaenda zangu.

yapo mengine mengine tu ya hela kubwa yaani mtaji mzima nilikuwa narudisha
 
Kuna jamaa nimeenda dukani kwake duka la Mpesa aniwekee sh 4100 ameniongezea sifuri moja!

Imewahi kukutokea ukazidishiwa hela ulipoenda kutoa pesa? Ulichukua hatua gani?
Nakumbuka mwaka 2004 nilikuwa napeleka materials kiwandani, nililipwa nikawa nadai 70000. Siku ya kwenda kumaliziwa malipo "Mhindi" kajiçhanganya kila elfu 10 kanipa laki! Jumla nikapewa 700000!
Nikaongeza mtaji. Hiyo hela faida yàke nikawa nàjenga nyumba, hadi tenda inaisha na nyumba iliisha. Lakini hiyo nyumba nilihonga.
 
Imenitokea last week branch ya crdb nilienda ku withdraw pesa ndani kwa cheque. Yule dada akanizidishia 10k. Nikatoka nje ndio nikagundua, nikataka nisepe nayo ila nafsi yangu ikagoma, ilikua 24 december.
Nikarud ndani nikamrudishia.
Kesho yake nikapigiwa simu na jamaa yangu ambaye nilikua namdai pesa 400k zaid ya mwaka akagoma kulipa na nikaamuaga kumsamehe na namba yake nikafuta maana hata mawasiliano yalikatika.

Jamaa akanipigia tar 25 dec chrismass niko ndan nimelala mchana ,akawa anaomba msamaha kwa kupotea na pesa yangu, nikamwambia asijali nilishasamehe awe na amani, akasema hapana, tulipomaliza kuongea nikaona 400k imesoma kwenye simu.

Nikashangaa sana, nafsi yangu ikanambia "ni ile 10k ya jana uliorudisha bank ndio imevuta hii 400k"
 
Hongereni sana mkuuu
 
Kuna jamaa nimeenda dukani kwake duka la Mpesa aniwekee sh 4100 ameniongezea sifuri moja!

Imewahi kukutokea ukazidishiwa hela ulipoenda kutoa pesa? Ulichukua hatua gani?
Rudisha ela ya watu , mbona ela kidgo sana inakutoa utu,,kwanza aliyekuwekea ameajiriwa na pengine atakatwa kweny mshahara wake ,,na itabadilika kua laana kwako
 
Hiyo imenitokea muda huu tu hapa,nimechukua Uber kuja job,nauli ilitakiwa iwe elfu 3,nikampa noti ya elfu 10 tena nae akanirudishia elfu 17 bila kujua,nikamwambia sitaki mabalaa ya asubuhi asubuhi hivi nikamrudishia 10k yake .
 
Nakumbuka mwaka 2004 nilikuwa napeleka materials kiwandani, nililipwa nikawa nadai 70000. Siku ya kwenda kumaliziwa malipo "Mhindi" kajiçhanganya kila elfu 10 kanipa laki! Jumla nikapewa 700000!
Nikaongeza mtaji. Hiyo hela faida yàke nikawa nàjenga nyumba, hadi tenda inaisha na nyumba iliisha. Lakini hiyo nyumba nilihonga.
Kama ni mhindi hakuna haja ya kumrudishia.
 
Itategemea na mtu aliyenizidishia pamoja na kiasi Cha fedha na hali yangu ya uchumi kwa wakati huo
Kuna tajiri mmoja alinizidishia hela nilipomrudishia alinicheka sana na matusi juu
Nilijikita fala sana
Hilo halikua tatizo lako mkuu, ni tatizo lake!!..
 
Back
Top Bottom