IMF: Kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Uganda Kufikia 11% Kuanzia Mwaka 2025 Baada ya Pesa za Mafuta Kuanza Kumiminika

Kwa sera zipi? Unadhani uchumi unakua Kwa maneno ya kijinga ya majukwaani ya Wanasiasa mbumbumbu?
Hao wanasiasa wasio mbumbumbu wamefanya nini zaidi ya kuuza rasilimali zetu kwa bei za kutupwa?

Gas iko wapi?

Ilisikika sauti ya mwanasiasa unaowasema si mambumbumbu kwamba, kufikia 2015, Tanzania itauza umeme kwa mataifa jirani na matumizi ya ndani itakuwa kila unit moja itauzwa kwa sh 30, na kwamba uchumi wake utafikia kiwango cha 17% kiko wapi?

Pumbafu kabisa
 
Rasilimali zenu zipi zilizouzwa? Walichofanya ndio kuifikisha Tanzania ilipo Sasa
 
Cha ajabu mkuu hiyo nchi uliyoitolea mfano ya Ethiopia zaidi ya 40% ya national budget yake inapokea msaada kutoka WB/IMF.
Pia Ethiopia hiyo hiyo ina mass unemployment kuliko nchi yeyote hapa Afrika mashariki.
Na ni miongoni mwa nchi zinazopokea msaada wa chakula kutoka WFP.
Cha kuongezea ni nchi ambayo ina poor social development na inaongoza kwa idadi ya vijana wanaokimbia nchi ukanda wetu.

Sasa nashindwa kuelewa hizi criteria za ukuaji uchumi zinazotumika zinaakisi nini??
Maana kwa udongo ni mambo mawili tofauti.
 
Huo ni uongo wa Karne eti Msaada wa IMF wa 40%,jifunze kutofautisha mikopo na Msaada.

Mikopo ni sehemu ya Mapato ya Nchi na inalipwa.

Mambo mengine uliyoeleza sababu ziko wazi kwamba ni Kasi kubwa ya population ndio inawatatiza kiasi kwamba hiyo growth rates Yao Wameshindwa kuondoka kwenye kundi la LCD licha ya kuwa na Uchumi mkubwa Afrika.

But Imani yangu ni kwamba wakirwjea kwenye Amani na Waka sustain Ukuaji wa over 10% Kwa miaka 10 zaidi Watafika Mbali sana na kupunguza hizo Changamoto.
 
uongo bhn uchumi wa Tz ukuaji ni 5.7-6.2%. Sasa hii ndo mara nne kweny 11% alafu kufikia 2035 una uhakika gan Tz haijafikia double figure?
 
Sidhani kama hiyo 40% ni mikopo bali kuna pahala nilisoma kuwa ni grants/aids kutoka IMF kuinua nchi masikini.

Kuhusu population kaka hiko ni KIGEZO DHAIFU SANA.Maana kuna nchi kama Central African Republic wana population ndogo ila masikini wa kutupwa.
Pia Ethiopia haina vita za kiasi hicho kuifanya isipige hatua kimaendeleo.
Ni vijiugomvi vya kikabila tu.
1)Hakuna uhakika wa ajira.
2)Huduma za kijamii kama elimu,maji,chakula, miundombinu ya usafiri,afya bado viko chini saaaanaaaa.
Na hii nchi haijawahi kutawaliwa sasa tujiulize inakwama wapi!?
 
Vyote ukichanganya ndio vinaleta hiyo average,hata Tanzania ni hivyo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…