Shirika la Fedha za Kimataifa IMF imesema Uchumi wa Uganda utaanza kupata Ukuaji mkubwa kuanzia mwaka 2025 ambapo Kasi ya Ukuaji wa Uchumi itaongezeka kutoka asilimia 6.2% mwaka 2024 na kufikia asilimia 10.8% kuanzia mwaka 2025.
Ukuaji huo utachangiwa na kuanza Kumiminika Kwa pesa za mauzo ya Mafuta mwishoni mwa mwaka 2025.
Kasi hii kubwa ya Uchumi wa Uganda itakuza Ukubwa wa Uchumi wa Nchi hiyo kutoka GDP ya $ 49bln (2024) Hadi GDP ya $ 120bln (2035) ambapo Wachambuzi wa Uchumi wanasema Uchumi huo utalingana Kwa Ukubwa na Tanzania.👇👇
View: https://x.com/Reuters/status/1834128627794931796?t=rBXwRZpnNB7hhcOWwp-hJQ&s=19
My Take
Kuna haja ya Tanzania kwenda kujifunza Kwa Ethiopia iliwezaje kukuza Uchumi wake Kwa double digit Kwa miaka 10 na kuzipita Kenya,Angola na Sudani kuwa Baba wa Uchumi Afrika Mashariki huku hawana Mafuta Wala gesi.
Vinginevyo Tanzania tutapitwa na Uganda Kwa Ukubwa wa Uchumi (GDP size) baada ya mwaka 2035.
Nchi zote ambazo zilipata maendeleo makubwa ni zile ambazo Uchumi wake uliwahi kujua Kwa double digit yaani kuanzia 10% Kwa miaka 10 mfululizo Duniani kote ndipo zilipunguza umaskini Kwa nusu vinginevyo Hali itazidi kuwa tete.
Hii growth rates ya 4-7% ambayo tumekuwa nayo Kwa miaka zaidi ya 15 haijawahi na Wala haitakuja saidia kuondoa umaskini 👇👇
View: https://x.com/TanzaniaInvest/status/1833424456926044371?t=OuBdrDykvfYDPafDjZrbMg&s=19
Pia soma
WB: Uchumi wa Tanzania (GDP) Umeongezeka na kufikia $ 80 Bilioni mwaka 2023.