IMF kuinua makadirio ya ongezeko la uchumi wa China ni habari njema kwa uchumi wa dunia

IMF kuinua makadirio ya ongezeko la uchumi wa China ni habari njema kwa uchumi wa dunia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111504019127.jpg


Hivi karibuni Shirika la Fedha la Kimataifa IMF liliinua makadirio ya ongezeko la pato la taifa la China kwa mwaka wa 2024, kutoka asilimia 4.6 za awali hadi asilimia 5, hatua inayoonesha imani ya jumuiya za kiuchumi za kimataifa kuhusu uchumi wa China. Makadirio haya pia yameongeza matumaini kwa nchi nyingi za kusini, ambazo uchumi wake umefungamana sana na uchumi wa China.

Kila mara taasisi za fedha za kimataifa zinapotoa takwimu kuhusu uchumi wa China, wataalam wa mambo ya uchumi na fedha, pamoja na wawekezaji na wanaviwanda, wanaofuatilia kwa makini takwimu hizo, hasa ikizingatiwa kuwa kinachotokea au kubadilika kwenye uchumi wa China kinagusa moja kwa moja hali ya uchumi wa nchi nyingine duniani. Ni wazi kuwa kuanzia kipindi cha janga la COVID duniani, uchumi wa China ulikumbana na changamoto mbalimbali na kupungua kiasi, hali hii ilichochewa kiasi na siasa za kijiografia barani Ulaya, mashariki ya kati na katika sehemu nyingine duniani.

Kutokana na hatua mbalimbali za ndani zilizochukuliwa na serikali ya China, hasa kurekebisha muundo wa uchumi na kuhimiza mageuzi, hali ya uchumi wa China inaendelea kuboreka na takwimu zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, ni ushahidi kuwa hatua hizo zimekuwa na matokeo chanya. Hali halisi ni kwamba, katika muda mrefu uliopita uchumi wa China ulitegemea zaidi uuzaji wa bidhaa za viwandani nje ya nchi, lakini kutokana na sera za uchumi zenye uhasama dhidi ya bidhaa za China hasa zilizoibuka hivi karibuni kutoka kwenye nchi za magharibi, migogoro ya kijeshi inayotokea katika sehemu mbalimbali duniani, na sintofahamu za kiusalama katika sehemu mbalimbali duniani, vimefanya uuzaji nje wa bidhaa za viwanda utafutiwe mibadala.

Kwa sasa matumizi ya ndani ni moja ya mibadala inayohimizwa na serikali ya China, na njia hii inaonekana kuwa na matokeo chanya kutokana na China kuwa na idadi kubwa ya watu wa tabaka la kati. Njia nyingine ni kuhimiza zaidi sayansi na teknolojia kwenye shughuli za kiuchumi, hali hii imeongeza tija kwenye shughuli za kiuchumi na kuleta faida kwa wajasiriamali na wenye viwanda.

Takwimu zilizotolewa na IMF kuhusu makadirio ya ongezeko la uchumi wa China, zimetolewa katika wakati ambapo mkutano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulikuwa unafanyika, na moja ya ajenda muhimu ni kinatarajiwa kupanga mageuzi yatakayochochea maendeleo ya hali ya juu ya China.

Pamoja na kuwa uchumi wa China unaonesha mwelekeo mzuri, ni wazi kuwa changamoto mbalimbali duniani zinaweza kuwa na athari hasi kwenye ongezeko la uchumi wa China. Marekani inaendelea kuyumbisha utulivu wa kisiasa kwenye nchi mbalimbali duniani, na kuna uwezekano kuwa uchaguzi ujao wa Rais wa Marekani ukawa na matokeo hasi sio tu kwa siasa za kijiografia duniani, bali kwa uchumi wa nchi nyingine. Umoja wa Ulaya ambao ni moja ya washirika wakuu wa kibiashara wa China, unapanga kutoza ushuru wa forodha wa hadi asilimia 38 kwa magari ya umeme ya China.

China imekuwa inachukua hatua mbalimbali kurekebisha hali ya uchumi wa ndani, hatua ambazo sio tu zina manufaa katika ongezeko la uchumi wa China, bali pia zina manufaa kwa uchumi wa dunia. Nchi za magharibi kwa upande mwingine, licha ya zenyewe kuwa wanufaika wakubwa wa soko la China na ongezeko la uchumi wa China, zimekuwa zinachukua hatua mbalimbali kujaribu kukwamishwa maendeleo ya China, na kufanya hivyo sio tu zijaribu kujidhuru, bali pia zinadhuru nchi nyingine duniani.
 
Back
Top Bottom