IMF wametoa orodha ya nchi zenye madeni makubwa zaidi katika bara la Afrika, Tanzania haipo!

Mkopo ambao unahusisha Kukupangia sera huo ni Ujinga.

Tulilipa deni lote IMF, saiv wameenda kuchukua tena.

Si ajabu wanakupa mkopo na kukupangia matumizi yake. Mfano kajengee matundu ya Choo.
Kwani tatizo liko wapi?
 
Leo nimeanza kuelewa kwanini tuendelee kukopa zaidi
 
Hivi unadhani wewe unavyokopesheka ndivyo na Mo au Bhakresa anavyokopesheka? Au Simba anavyokopesheka unadhan atalingana na Namungo fc
 
Usihadaike na hizo namba, mzigo wa deni hupimwa na uchumi wa nchi. Kama wewe uchumi wako ni $300, ukikopa $400 utakuwa ni mzigo mkubwa sana kwako lakini kwa mwenye uchumi wa $4000, mkopo huo wa $400 ni mdogo tu.
 
Pesa za mikopo iliyopita inanemesha wachache na majority wanaishia kupigwa propaganda. Hatuko tayari kukopa kwa masilahi ya watu binafsi.
 
Mikopo sio yote inatoka IMF.
Zingatia hilo
 
Mkopo ambao unahusisha Kukupangia sera huo ni Ujinga.

Tulilipa deni lote IMF, saiv wameenda kuchukua tena.

Si ajabu wanakupa mkopo na kukupangia matumizi yake. Mfano kajengee matundu ya Choo.
Itakuwa wanauzoefu na tabia zetu. Halafu naona kile wanachopanga kinakuwa na faida na jamii!

Chukulia mfano wasingekuwa wanasimamia walichokubaliana, ina maana wanasiasa wangekuwa wanazipiga hela na kubadilisha matumizi.

Lazima wanasiasa wetu wawe na mipango ili wanapoenda kuombea mikopo sehemu fulani, basi hiyo sehemu ikamilike.

Kwa mfano, pesa walizokopa benki ya dunia kujenga barabara za mijini zimesaidia miji mingi kuwa na lami na taa za barabarani. Sharti mojawapo, lazima lami ianzie kwenye lami na iishie kwenye lami. Sharti hili linawabana wanasiasa wabinafsi kujipelekea barabara ya lami mpaka nyumbani kwao hata kama anaishi pembeni ya mji.
 
Tanzania Tuongeze bidii kukopa
 
Makamanda uchwara watawalalamikia IMF kwa nini hawakuijumlisha Tz, ha ha ha😎
 
Wewe uko wapi kwani?
Nipo huku ambako bado watu wanakwenda vichakani kumaliza mashauri yao. Huko kwenu vyoo vya matundu vimeenea kila mahali? Kila kaya inacho choo cha tundu kwa matumizi yake?
 
Nipo huku ambako bado watu wanakwenda vichakani kumaliza mashauri yao. Huko kwenu vyoo vya matundu vimeenea kila mahali? Kila kaya inacho choo cha tundu kwa matumizi yake?
Daaah nchi ngumu kwelikweli
 
Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…