IMF yaisamehe Tanzania deni la Tsh. Bilioni 33 kwa ajili ya Corona

Hello ndogo sana hiyo kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapoomba relief sio lazima upate unachoomba. Wamejikuna pale wanapoweza hilo ndio kwangu mimi naona ni la msingi. Hata kama una shida unapokwenda kuomba msaada wa dharura chochote unachopata unashukuru. wangeweza kabisa kusema hatukupi na hilo lingekuwa sawa vile vile. Hiyo relief itasaidia kwa njia moja au nyingine. Wewe ulitaka watoe ngapi? Soma hiyo taarifa kwanza uielewe wacha kukurupuka.
 

Its a partial forgiveness of debts to IMF.

Hivyo IMF wamemsikiliza raisi Magufuli na wamekubaliana na hoja yake kuhusu IMF kusamehe madeni kwa nchi inazozidai khasa wakati huu wa COVID-19.

Hivyo katika deni tunalodaiwa tumesamehewa hizo dola milioni 14.3 ambazo zinakuwa pumped back to bongoland Tanzania.

Hivyo deni letu IMF limepunguzwa kwa dola milioni 14.3.

Kitita hicho chatosha kabisa kuendeleza gurudumu la maendeleo.

Hongera sana Mr President.

Hapa Kazi Tu.
 
Hakuna mahali wamesema mmesamehewa deni. Somauelewe
 

Mtu akisoma kwa makini atagundua kuna tofauti kati ya mleta thread alichopendekeza watu waelewe na uhalisia wa kinachozungumzwa ndani ya Mada!
 
Mkuu Rais Magufuli aliomba debit relief na Mabeberu yametekeleza km mwamba alivyotaka
Aliomba billioni zaidi ya 700 kapewa 28. Sasa 28 si hata yeye anazo? Hii ni kama wamemnyima tu. Huu ni kama msaada ambao hata Marekani alitoa kama Bilioni 15.
 
Hawa IMF wangesema tu kuwa wamekataa kuisaidia Tanzania.

Ni wenye Catastrophe Containment and Relief Trust nchi zimepewa msaada na mikopo ya mabilioni ya shilingi kama sio matrilioni sisi tunakuja kupewa bilioni 28?

Ukisoma barua ya serikali kuomba huo msaada ilielezea kwa uchungu sana kuwa hali ni mbaya sana tena kuanzia July 2020 inahitaji msaada wa haraka sana kuokoa uchumi.

Jambo la kushangaza imf wanatupatia bilioni 28 tu? Hizi si hata Mo angetupatia tu.

Eu imeipatia Kenya pesa za bure Billioni zaidi ya 750 za kitanzania sisi tunapewa na IMF bilioni 28?.

Hebu turudi kwenye sense kidogo. Hivi serikali iliwaza nini kuandika barua kuomba msaada wakati wanajua kabisa hawakufuata hata sharti moja la kupewa msaada? Au walijua watawadanganya imf na watakubali?

Au serikali wanafikiri wazungu hawajui kinachoendelea hapa nchini? Wewe ulishasema corona haipo halafu unaandika barua kuomba msaada usaidiwe kupambana na corona, corona ipi?

Toka corona iamze hii ni barua ya 4 serikali inaandika kwa wanaoitwa mabeberu ambao hawatupangii chochote kuwaomba hela lakini zote zinagonga mwamba.

Ya kwanza serikali iliomba Dollar millioni 198 mwezi February, ikakakosa, ya pili ni mwezi March tuliomba kusamehewa kulipa madeni huku tumedanganya idadi halisi ya madeni yetu kwa zaidi ya Trillion 6. Tukanyimwa kwa uongo.

Barua ya tatu tukaandika IMF kua tumetumia Dollar 372 Millioni kusamehe kodi ya VAT kwa makampuni yanayoingiza vifaa vya kupambana na corona na kusaidia biashara ndogo ndogo zisiathirike na Dollar 302 Millioni ya kununua vifaa vya kupambana na corona. Tukakosa kwa kusema uongo.

Ya nne ndio hii tumepewa billioni 28. Naamini serikali hawatakata tamaa. Wataandika nyingine tena ya 5.
 
Tumepewa msamaha, hatujakopeshwa, that's the good thing. Kenya na Uganda hizo pesa watazilipa tena kwa riba kubwa. NO FREE MONEY
 
Tumepewa msamaha, hatujakopeshwa, that's the good thing. Kenya na Uganda hizo pesa watazilipa tena kwa riba kubwa. NO FREE MONEY
Aliekwambia Kenya wamepewa kwa riba kubwa ni nani? Soma hapa chini.
Kwenye hizo grant jumla hadi sasa ni Dollar million 300 na nchi nyingine zimetoa Dollar million 33 jumla 333 Millioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…