Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Shirika la fedha duniani (IMF) limeionya selikali ya Kenya kwamba inaweza kuelemewa na madeni, kutokana na kudorora kwa uchumi wa nchi hiyo unaosababishwa na janga la corona.
Deni la Kenya kwa sasa ni 67% ya pato jumla la Taifa.
Ikumbukwe wiki 3 zilizopita IMF iliikopesha Kenya dola milioni 700. Mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Mombasa amesema Kenya ilikopa fedha hizo ili kusaidia shughuli za selikali katika kipindi hiki cha janga la corona maana hakuna uzalishaji unaoendelea na selikali imeishiwa.
Mchambuzi huyo ameonya pia hatua za kukabiliana na corona hasa kufungia watu ndani kuwa huenda likawa janga jipya nchini Kenya na uchumi utazidi kudidimia.
Ikumbukwe pia J. P. Magufuli alishauri haya mashirika ya fedha yanapaswa kuzifutia kabisa madeni ambayo yanazidai nchi masikini katika kipindi hiki badala ya kuzikopesha na kuzidisha mzigo tena.
Hili suala la IMF kuzifutia madeni nchi zinazochipukia nmeona ameshauri pia Mgombea urais kwa tiketi ya Democrat nchini Marekani, lakini watu walimkejeli JPM.
Hawa ndio Kenya inayoshindana na Tanzania kwa kutaka kufunga mipaka.
Chanzo: DW mchana huu.