GE2025 Imfikie Rais ayafanye ili kuondoa kinachoendelea kwa wananchi

GE2025 Imfikie Rais ayafanye ili kuondoa kinachoendelea kwa wananchi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mheshimiwa rais,

Nakusalimu kwa unyenyekevu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Mheshimiwa rais, nafupisha sana nisikupotezee muda wako adhimu.

Mheshimiwa rais, yafuatayo ni mambo niliyoyatafiti na hivyo nimeona vema kukushirikisha kwa njia hii:

1. Nchi haijakushinda kama baadhi ya watu wanavyodai. Hata hivyo kuna 'machawa' wanaokuzunguka wana lengo hilo, kukufanya ufeli, hata hivyo umewaamini sana kwa sababu ya tabasamu lao usoni, maneno yao ya kukusifu na hata yale mliyoyarekodi kwa siri, walijua kuwa wanarekodiwa. Pima matokeo 'output' na athari 'outcome' ya mapendekezo na ushauri wao kwako na sio mashamsham 'vibe' za kipambe wanazokupa. NI WATU HATARI SANA KWAKO.

2. Tunafanya kazi kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadaye. Hakuna haja ya kuwaachia watoto wetu matatizo tunapoondoka madarakani au hata duniani. Kwenye 'deals' zenye utata hakuna mtu huiweka familia yake kuja kujibu baadaye na hasa katika mazingira ya kutokuwa na kinga ya kutokushtakiwa.

3. Tanzania mpya sio njema kabisa kwa CCM japo inaweza kuwa njema kwa taifa 'in a long run'. Tanzania mpya itazaliwa endapo (i) kesi ya TAL itaendelea (ii) Humphrey Pole Pole hatopatikana akiwa na hali njema (iii) Maswali ya wananchi kuhusu watekaji hayatojibiwa kwa vitendo (iv) Vita haramu dhidi ya vyama vya upinzani havitakomeshwa.

4. Yuko adui mkubwa na mwenye nguvu nyuma ya haya yanayotokea. Kwako amejifanya rafiki. Lengo lake ilikuwa uchafuke wewe, akutoe aweke watu wake. Humphrey Polepole akagundua na kukusaidia. Leo hii taifa limejua kuwa kumbe shetani sio wewe, bali kuna namna umekuwa 'captured', na kwa maslahi ya taifa inabidi ucheze mziki wao. TUTAKUOKOA.

Mama nakuomba ufanye yafuatayo ASAP (kwa unyenyekevu nakusihi):

1. Tuma watu wako (wale 'first class E1) washirikiane na vijana wa Nkunda mkamwokoe Humprey huko aliko. Humphrey hakuwa anakushambulia kama ulivyodhani bali alikuwa anakuokoa wewe, kwa mujibu wa viapo vyetu, wewe ndiye alama ya taifa. Haya ni mambo ya Cuba mama. Kama sio Humprey kutuonyesha adui namba moja wa dola yako ni nani leo hii wangeshakumeza. Ilikuwa usifike Oktoba. Ukichelewa, sijui kitakachojiri.

2) Kesi ya Tundu Lissu, DPP aipige chini fasta. Huyo Tundu Lissu hana madhara akiwa uraiani kuliko akiwa kwenye hali hii ya sasa. Taifa linachafuka sana. Tumieni watu wenye akili watakusaidieni, sio hao wenye kujua kuua tu bila kujua namna ya kulinda mustakabali wa taifa. I can also help.

3) Mtumie Humprey kukusaidia kabla ya 29/10. Ana uwezo na ana watu wenye uwezo, wa rika mbalimbali kuzima matatizo ambayo yanaweza kutokea kwa taifa. TISS wakikupa 'intel analysis' ya kweli utagundua kuwa anayeyasukuma haya yote anaendelea kufanikiwa kwa kukudanganya. Kumbuka walivyomdanganya JPM.

4) Msigwa angejitahidi kukutenganisha na udhalimu wa 'shetani wa pwani'. Huyo anayempa 'script' zinakuchafua wewe na kumpamba 'swp'. Alipaswa katika kila 'script', akutenge na kashfa zote: utekaji, kuuzwa bandari, Kiziga, Rostam, JK, mauaji n.k. kuna namna ya kuja na script zinazojenga taswira njema kuhusu rais, serikali n.k na sio hizo za kuwatisha Gen Z na za majigambo.

5) Tunaojua ukweli, tunajua rais wetu huhusiki na kashfa yeyote, isipokuwa UMETEKWA. Tunataka tukuokoe mama yetu, kutoka mikononi mwao 'before it's too late'.

6) Tuko kambini hapa, fanya upande wako na sisi tutakulinda, wasikudanganye walamba damu, hutaingia Ikulu kwa njia zao, acha sisi wananchi tukuthibitishe. Mbaya wetu tushamjua. Aliyetaka kutuchonganisha na wewe mama yetu tushamjua. Picha mbaya waliyotengeneza tutaiondosha.

Tusikilize sisi wananchi wako tulio na mapenzi thabiti kwako. Achana na machawa na huyo shetani wa Pwani WATAKUPOTEZA mama.

Nimetimiza wajibu wangu mama. Nimekwambia ukweli.

Nina mengi ya kukuambia, lakini nimejaribu kukupa hayo machache bila kumpa adui faida.

Nawasilisha kwako kwa unyenyekevu mkubwa, mheshimiwa rais.

Asante!

Ninja.
Namba 4 ya kwanza kuhusu Polepole umedanganya. Yaani unasema Polepole alitaka kumsaidia Samia?? Polepole ni abiria kwenye ambaye alikuwa kwenye mtumbwi unaoendeshwa na Samia, wakiwa katikati ya bahari akaamua kuanza kuutoboa mtumbwi.

Mtu kama huyu anapogundulika, anakamatwa na anatoswa kwenye bahari na kuwa chakula cha papa
 
Namba 4 ya kwanza kuhusu Polepole umedanganya. Yaani unasema Polepole alitaka kumsaidia Samia?? Polepole ni abiria kwenye ambaye alikuwa kwenye mtumbwi unaoendeshwa na Samia, wakiwa katikati ya bahari akaamua kuanza kuutoboa mtumbwi.

Mtu kama huyu anapogundulika, anakamatwa na anatoswa kwenye bahari na kuwa chakula cha papa
Una habari kuwa HP alianza kumshauri kwa usiri mkubwa lkn Mama kashupaza shingo? Alimshauri pia kwa maandishi na alipoona kimya akawatumia na Wazee fulani bila mafanikio?

Haya tuliokuja kuyaona ni baada ya safari ndefu ya ushauri uliotupwa kapuni bila kufanyiwa kazi.
 
Una habari kuwa HP alianza kumshauri kwa usiri mkubwa lkn Mama kashupaza shingo? Alimshauri pia kwa maandishi na alipoona kimya akawatumia na Wazee fulani bila mafanikio?

Haya tuliokuja kuyaona ni baada ya safari ndefu ya ushauri uliotupwa kapuni bila kufanyiwa kazi.
Kwani alikuwa anamshauri Samia yeye kama nani? Mbona Mwendazake alipofuta mikutano ya vyama na kuanza kuliburuza bunge hakumshauri?

Na kwa akili gani alizonazo Polepole aliyepata Div Zero Benjamin Mkapa Sec awe mshauri wa Rais?

Yeye alipewa kazi ya Ubalozi na alipaswa afanye kazi ya ubalozi. Mambo ya ushauri kuna watu walioajiriwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Haiwezekani kila mtu anajifanya mshauri wa Rais
 
Acheni aendelee kushupaza shingo. Oktoba 29 asipokimbia nchi, tukimkamata tutampakaa UPUPU kwenye makalio yake. Atajuta sana.
Mnachoweza ni matusi na matisho ya mtandaoni tu lakini kwa GROUND hakuna mwenye ujasiri
 
6) Tuko hapa na sisi tutakulinda, wasikudanganye acha sisi wananchi tukuthibitishe.
Tusikilize sisi wananchi wako tulio na mapenzi thabiti kwako.

Nawasilisha kwako kwa unyenyekevu mkubwa, mheshimiwa rais.

Asante!

Ninja.
Naunga mkono hoja, Hayo mengine yote, the time is too little too late, kitu cha maana cha kufanya ni October 29 kwenda kutiki.
P
 
Umwambii kitu kwa jamaa wa pwani hadi ameahidi kumjengea uwanja wa mpira kwa jina lake
 
Mtaishia kuandamana mtandaoni tu, hakuna watanzania wa hivyo.
Kama una uhakika tutaandamana mitandaoni tu, wasiwasi wako ni nini? Wewe ndio Abdul? Kiziga? au kijana wa Mombo?
 
Mtaishia kuandamana mtandaoni tu, hakuna watanzania wa hivyo.
We mjinga, huoni vile rais wako Samuya anavyohangaika na bahasha za hongo? Hadi anaona soo, safari hii ninyi majizi mtakimbia nchi tu.
 
Back
Top Bottom