In Memoriam: Siku Saba za Maombolezo ya Mzee R. M. Kawawa

In Memoriam: Siku Saba za Maombolezo ya Mzee R. M. Kawawa

Maombolezo siyo maana watu wasifanye kazi... Maombolezo ni kutoa heshima kwa kiongozi mkuu kama huyu aliyetumikia taifa kukumbukwa...Nashauri tufanye kazi kwa bidii na maarifa wakati huu wa maombolezo na baadaye katika kumuenzi Simba wa vita...
 
Maombolezo siyo maana watu wasifanye kazi... Maombolezo ni kutoa heshima kwa kiongozi mkuu kama huyu aliyetumikia taifa kukumbukwa...Nashauri tufanye kazi kwa bidii na maarifa wakati huu wa maombolezo na baadaye katika kumuenzi Simba wa vita...
Tukopamoja mkuu.....maana nakumbuka hata zile siku 30 za mwl JKN watu walifanya kazi au
 
nakubaliana na siku saba,

lakini ningefurahi kama zingekuwa angalau 14. mnajua huyu ni simba kwelikweli, kumbuka alikuwa waziri mkuu wa pili wa tanganyika na pia waziri mkuu wa tanzania na makamu wa pili wa raisi nk. mnafikiri nyerere kumuachia uwaziri mkuu muda mfupi baada ya uhuru kilikuwa kitu rahisi?

mkiangalia historia ya afrika wakati ule hata wakati wetu huu mtakubaliana nami kuwa hapajapata kuwa na mfano wa hawa watu wawili (nyerere na kawawa) hapa duniani!

raha ya milele ummpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani
 
sinkala-albums-sinkala-picture813-flag4.gif
 
Rais ametumia busara kubwa sana, na kwa kumuenzi Mzee wetu basi Rais awashughulikie mafisadi ambao wanaimaliza nchi.
 
Wakuu kwani hatuna mwongozo wa siku za maombolezo ya kitaifa? Wataalam wa itifaki naombeni mwongozo
Pumzika kwa amani Simba wa Vita!
 
Wakuu kwani hatuna mwongozo wa siku za maombolezo ya kitaifa? Wataalam wa itifaki naombeni mwongozo
Pumzika kwa amani Simba wa Vita!

kawawa kama makamu wa rais mstaafu anastahili siku 7......hiyo ni pamoja na makamu wa rais wengine wote wastaafu ..kikatiba!!!

sina kumbukumbu vema lakini najuwa kuwa rais ni siku 30...[akifia ofisini].,mstaafu ni siku 14...[nyerere alipewa special consideration ya 30 dys kama founder]....makamu wa rais/waziri mkuu/rais wa zanzibar akifia ofisini siku 14 pia....nadhani marekebisho ya mwisho ya katiba yaliweka hili swala!
 
Duu watu kweli wavivu.....Mlipanga kuwe off week nzima....
 
siku saba??? nyingi sana, atleast wangefanya siku 3, nchi tajiri na zilizoendelea they dont do these things
Tovuti,
Naamini Haikukusudiwa kufunga maofisi na Shughuli kwa hizo siku saba, ila Bendera ziwe nusu mlingoti nasi tuwe katika hali ya maombolezo na kutafakari Mchango wa Utumishi wa Mwenzetu huyo Mzee wetu aliyetangulia. Mola amweke pema (amin)
 
sijui tbc wanayo filamu inayoitwa "mhogo mchungu"?

inasema sinema hii mhusika mkuu alikuwa marehemu mzee kawawa
ila baadae "ilipigwa marufuku/iliondolewa sokoni".
 
Siku ya maziko yake inatakiwa tukae nyumbani ili tuomboleze kuondokewa na mzee wetu. Kama Nyerere alivyokuwa huyu mzee alikuwa muadilifu kweli kweli. Hana chembe ya ufisadi wala tamaa ya madaraka. Kama mwenzake alikaa kijijini Madale au Kiluvya akijishughulisha na kilimo.

Tunaomba Mungu aiweke roho ya mpendwa wetu mzee RMK mahali pema peponi Amin.

RIP mzee RMK

Marehemu Kambarage na Kawawa walikuwa viongozi wazalendo na waadilifu; kuthibitisha hayo tutaona kesho nyumbani kwake huko Madale jinsi alivyoishi maisha ya kawaida ingawa aliwahi kushika nyadhifa nyingi na kubwa katika taifa letu. Hiyo siku ya mazishi itakuwa fulsa kwetu kupata kigezo cha jinsi ya kuwapima uzalendo na uadilifu wa viongozi wetu waliopo madarakani; hawa wa siku hizi kwa muda mfupi tu waliokaa madarakani wamekwisha jilimbikizia vijisenti huko nje na kujenga mahekalu mijini na hata huko vijijini kwao ambako hawaoni aibu mahekalu yao yakizungukwa na matembe ya majirani wananchi walipa kodi wao!!
 
leo nimeamini kama kweli watz ni wavivu na hawapendi kazi, jamani siku 7 zote, na hakuna anayelalamika, na nchi yetu masikini ya mwisho

Jamani kama hauelewi maana ya maombolezo ni bora ukauliza. Siyo kwamba ktk siku saba za maombolezo watu hawataenda kazini. Kazi huwa zinaendelea kama kawaida ila bendera ndo zina pepea nusu mlingoti kwa siku saba.

Msitoe comments kwa vitu ambavyo hamvijui vizuri.
 
Back
Top Bottom