Ina maana gani hasa Mtanzania kufurahia vikwazo vya kimataifa kwa nchi yetu?

Kuna magaidi humu wanafuraihia kuwatwanga wenzao risasi na wanakwambia wejipanga Tena kuangamiza roho za watanzania.
Kuna hata tone la kuashiria furaha kwa mauaji katika makala haya? Tusiwe wepesi kuhukumu!
 
Tunasamehe pale inapotokea bahati mbaya.

Ila kwenye hili ilikuwa ni dhamira ambayo viashiria vyake vilijionesha kabla ya tukio.

Kabla ya maandamano viongozi walitoa kauli za kuvunja watu miguu, kuua watajitokeza kuandamana.

Na nikirejea kauli ya Polepole aliwahi kutudokeza mapema kuwa kuna timu ya wazee inaundwa kwa ajili ya kufanya maridhiano baada ya kile wanachotaka kufanya kabla ya uchaguzi.

Kwa mazingira hayo ni mtu mjinga tu ndio ataona maridhiano ni njia ya kweli ya kutuvusha hapa tulipo.

Na mbaya alipokuja kuharibu ni kwenye speech yake ya jana. Ile tone haioneshi nia ya kweli ya maridhiano.
 
Tukiwa kidato cha kwanza kwenye somo la uraia, yaani civics mada ya kwanza kufundishwa ilikuwa ni familia. Sijui mitaala ya wadogo zangu Gen Z inasemaje, ila sisi tulifundishwa kuwa familia ndio msingi wa jamii zetu na Taifa letu.

Kwa muktadha huu sitakuwa nimekosea kulifananisha Taifa na familia.

Fikiri kwamba imetokea sintofahamu nyumbani kwenu, ambapo mzazi ametenda jambo ambalo baadhi ya wanafamilia hamkubaliani nalo, kwamfano kaiweka reheni nyumba ya familia ili kupata mkopo kwaajili ya starehe zake binafsi.

Baada ya mambo kuharibika akawaiteni kitako, akakiri amekosea, akamwaombeni mama yenu aseme hakutoa idhini ilimradi tu nyumba yenu mnayoishi isalimike.

Katika mazingira kama hayo ndugu yenu mmoja akatoka kuwapa taarifa bank wanaomdai mzazi wako juu ya kikao chenu, nakuwapa bank mbinu ya kufanikisha kuuza hiyo nyumba yenu kwa lengo la kumkomoa huyu mzazi kwa ufujaji mali alioufanya. Wewe kama sehemu ya familia iliyopatwa na mkasa kama huu, utakuwa na maoni gani?

Kisa hiki kina shabihiana sana na hali ya nchi yetu kwa sasa. Mpaka sasa hatubishani tena kuwa watu waliuawa, walijeruhiwa, walipoteza mali na miundombinu iliharibika.

Hili lilitokea, na hatuwezi kulifuta hata tukilaumiana vipi. Lakini kwa hali ilivyo, linaelekea kutuletea madhara makubwa zaidi tuendako mathalani kuzuiliwa kwa baadhi ya misaada ambayo kwakweli ni kichocheo cha ustawi wetu.

Chukulia sekta ya afya kwa mfano; huduma nyingi tunazipata kupitia wahisani kupitia busket fund na miradi mingine. Ikitokea nchi yetu ikakosa misaada hii ni wazi kuwa sekta kama ya afya zitatetereka sana na kuna hatari ya kuwapoteza ndugu zetu kama vile wanaoishi na VVU kwa kukosa dawa.

Sasa hawa wenzetu wanaofurahia maazimio hasi yanayofanywa na mataifa wahisani kwa makosa tuliyoyafanya Octoba 29, wanatofautiana vipi na mtoto anaeshirikiana na wadai wa baba yake kuuza nyumba ya familia kwa lengo la kumkomoa huyo baba yake?

Katika maisha tunatakiwa kujifunza kusamehe na kuendelea mbele hata kama hao tunaodhani wametukosea ni wajeuri. Kesho yetu ni bora kuliko jana, kama tunayo dhamira ya dhati ya kuifanya kesho yetu kuwa bora tunaowajibu wa kulipa gharama ya kuachilia mambo mengine yatupite.

Waingereza wanamsemo wao kuwa, tukimrushia mawe kila mbwa anayetubwekea hatutafika safari yetu.
Sio lengo langu, kumtetea mtu au kumlaumu mtu katika makala yangu, Shabaha yangu ni kuwasihi ndugu zangu kuweka maslahi ya nchi mbele kwa kauli na vitendo vyetu.

Vikwazo vikiwekwa dhidi ya nchi yetu Rais Samia atakuwa wamwisho kuathirika. Hakuna siku Rais hatalala, hatakula au hatatibiwa kwasababu nchi ina hali mbaya.

Yatakayotupata hayo ni sisi masikini wa nchi hii. Kama tukilijua hilo sidhani kama tutashabikia maazimio hasi ya kimataifa yanapofanywa dhidi ya nchi yetu.
Mimi ni mwalimu, mishahara wangu ni kidogo sana,sijari Wala siogopeshwi na vikwazo, nitafurahi sana tukiwekewa vikwazo. Vikwazo Huwa ni vya muda,hulenga mhusika ajirekebishe ,akijerekebisha vinaondolewa

Hivyo kama Kuna vikwazo naviombea usiku na mchana bike, serikali ya mhaini mkuu Samia idondoke.
 
Tukiwa kidato cha kwanza kwenye somo la uraia, yaani civics mada ya kwanza kufundishwa ilikuwa ni familia. Sijui mitaala ya wadogo zangu Gen Z inasemaje, ila sisi tulifundishwa kuwa familia ndio msingi wa jamii zetu na Taifa letu.

Kwa muktadha huu sitakuwa nimekosea kulifananisha Taifa na familia.

Fikiri kwamba imetokea sintofahamu nyumbani kwenu, ambapo mzazi ametenda jambo ambalo baadhi ya wanafamilia hamkubaliani nalo, kwamfano kaiweka reheni nyumba ya familia ili kupata mkopo kwaajili ya starehe zake binafsi.

Baada ya mambo kuharibika akawaiteni kitako, akakiri amekosea, akamwaombeni mama yenu aseme hakutoa idhini ilimradi tu nyumba yenu mnayoishi isalimike.

Katika mazingira kama hayo ndugu yenu mmoja akatoka kuwapa taarifa bank wanaomdai mzazi wako juu ya kikao chenu, nakuwapa bank mbinu ya kufanikisha kuuza hiyo nyumba yenu kwa lengo la kumkomoa huyu mzazi kwa ufujaji mali alioufanya. Wewe kama sehemu ya familia iliyopatwa na mkasa kama huu, utakuwa na maoni gani?

Kisa hiki kina shabihiana sana na hali ya nchi yetu kwa sasa. Mpaka sasa hatubishani tena kuwa watu waliuawa, walijeruhiwa, walipoteza mali na miundombinu iliharibika.

Hili lilitokea, na hatuwezi kulifuta hata tukilaumiana vipi. Lakini kwa hali ilivyo, linaelekea kutuletea madhara makubwa zaidi tuendako mathalani kuzuiliwa kwa baadhi ya misaada ambayo kwakweli ni kichocheo cha ustawi wetu.

Chukulia sekta ya afya kwa mfano; huduma nyingi tunazipata kupitia wahisani kupitia busket fund na miradi mingine. Ikitokea nchi yetu ikakosa misaada hii ni wazi kuwa sekta kama ya afya zitatetereka sana na kuna hatari ya kuwapoteza ndugu zetu kama vile wanaoishi na VVU kwa kukosa dawa.

Sasa hawa wenzetu wanaofurahia maazimio hasi yanayofanywa na mataifa wahisani kwa makosa tuliyoyafanya Octoba 29, wanatofautiana vipi na mtoto anaeshirikiana na wadai wa baba yake kuuza nyumba ya familia kwa lengo la kumkomoa huyo baba yake?

Katika maisha tunatakiwa kujifunza kusamehe na kuendelea mbele hata kama hao tunaodhani wametukosea ni wajeuri. Kesho yetu ni bora kuliko jana, kama tunayo dhamira ya dhati ya kuifanya kesho yetu kuwa bora tunaowajibu wa kulipa gharama ya kuachilia mambo mengine yatupite.

Waingereza wanamsemo wao kuwa, tukimrushia mawe kila mbwa anayetubwekea hatutafika safari yetu.
Sio lengo langu, kumtetea mtu au kumlaumu mtu katika makala yangu, Shabaha yangu ni kuwasihi ndugu zangu kuweka maslahi ya nchi mbele kwa kauli na vitendo vyetu.

Vikwazo vikiwekwa dhidi ya nchi yetu Rais Samia atakuwa wamwisho kuathirika. Hakuna siku Rais hatalala, hatakula au hatatibiwa kwasababu nchi ina hali mbaya.

Yatakayotupata hayo ni sisi masikini wa nchi hii. Kama tukilijua hilo sidhani kama tutashabikia maazimio hasi ya kimataifa yanapofanywa dhidi ya nchi yetu.
Mfano wako ni irrelevant. Hapa kama nchi hakuna aliyeomba msamaha, zaidi ya kusema uongo, na kuwalazimisha wahanga kuwa ndio wakosaji. Hivi mnaamini tutaendelea kuishi kwenye misamahaya ya kuuana ili watoto, ndugu na jamaa wa viongozi wakae madarakani?

Ni hivi, hatuko tayari kutawaliwa tena kwa shuruti na ccm, ni bora tukose hiyo misaada maana huenda ndio inayofanya ccm ipore chaguzi za nchi hii, na kulazimisha kukaa madarakani kwa shuruti. Hakuna uwezekano wa kizazi kuichoka ccm, kisha ikalazimisha kuendelea kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. Tena muombe tusipate silaha, maana hawa viongozi tusiowataka wanajenga viburi kwani wanapata ulinzi wa silaha. Ikibidi nchi za nje sio kusitisha misaada tu, watunyime mikopo, na ikiwezekana wasinunue hata bidhaa zetu.

Tarehe 9 tunarudi barabarani, safari hii haziharibiwi mali za watu, bali ni maandamano ya amani kuwa hatumtaki rais, na tunataka serekali ya mpito kueleke kupata katiba mpya, na tume huru ya uchaguzi. Tusiguswe na risasi maana hatuna silaha, na tukipigwa risasi mjiandae na uhasama wa kudumu na vikundi vya kigaidi kama m23. Enough is enough.
 
Tukiwa kidato cha kwanza kwenye somo la uraia, yaani civics mada ya kwanza kufundishwa ilikuwa ni familia. Sijui mitaala ya wadogo zangu Gen Z inasemaje, ila sisi tulifundishwa kuwa familia ndio msingi wa jamii zetu na Taifa letu.

Kwa muktadha huu sitakuwa nimekosea kulifananisha Taifa na familia.

Fikiri kwamba imetokea sintofahamu nyumbani kwenu, ambapo mzazi ametenda jambo ambalo baadhi ya wanafamilia hamkubaliani nalo, kwamfano kaiweka reheni nyumba ya familia ili kupata mkopo kwaajili ya starehe zake binafsi.

Baada ya mambo kuharibika akawaiteni kitako, akakiri amekosea, akamwaombeni mama yenu aseme hakutoa idhini ilimradi tu nyumba yenu mnayoishi isalimike.

Katika mazingira kama hayo ndugu yenu mmoja akatoka kuwapa taarifa bank wanaomdai mzazi wako juu ya kikao chenu, nakuwapa bank mbinu ya kufanikisha kuuza hiyo nyumba yenu kwa lengo la kumkomoa huyu mzazi kwa ufujaji mali alioufanya. Wewe kama sehemu ya familia iliyopatwa na mkasa kama huu, utakuwa na maoni gani?

Kisa hiki kina shabihiana sana na hali ya nchi yetu kwa sasa. Mpaka sasa hatubishani tena kuwa watu waliuawa, walijeruhiwa, walipoteza mali na miundombinu iliharibika.

Hili lilitokea, na hatuwezi kulifuta hata tukilaumiana vipi. Lakini kwa hali ilivyo, linaelekea kutuletea madhara makubwa zaidi tuendako mathalani kuzuiliwa kwa baadhi ya misaada ambayo kwakweli ni kichocheo cha ustawi wetu.

Chukulia sekta ya afya kwa mfano; huduma nyingi tunazipata kupitia wahisani kupitia busket fund na miradi mingine. Ikitokea nchi yetu ikakosa misaada hii ni wazi kuwa sekta kama ya afya zitatetereka sana na kuna hatari ya kuwapoteza ndugu zetu kama vile wanaoishi na VVU kwa kukosa dawa.

Sasa hawa wenzetu wanaofurahia maazimio hasi yanayofanywa na mataifa wahisani kwa makosa tuliyoyafanya Octoba 29, wanatofautiana vipi na mtoto anaeshirikiana na wadai wa baba yake kuuza nyumba ya familia kwa lengo la kumkomoa huyo baba yake?

Katika maisha tunatakiwa kujifunza kusamehe na kuendelea mbele hata kama hao tunaodhani wametukosea ni wajeuri. Kesho yetu ni bora kuliko jana, kama tunayo dhamira ya dhati ya kuifanya kesho yetu kuwa bora tunaowajibu wa kulipa gharama ya kuachilia mambo mengine yatupite.

Waingereza wanamsemo wao kuwa, tukimrushia mawe kila mbwa anayetubwekea hatutafika safari yetu.
Sio lengo langu, kumtetea mtu au kumlaumu mtu katika makala yangu, Shabaha yangu ni kuwasihi ndugu zangu kuweka maslahi ya nchi mbele kwa kauli na vitendo vyetu.

Vikwazo vikiwekwa dhidi ya nchi yetu Rais Samia atakuwa wamwisho kuathirika. Hakuna siku Rais hatalala, hatakula au hatatibiwa kwasababu nchi ina hali mbaya.

Yatakayotupata hayo ni sisi masikini wa nchi hii. Kama tukilijua hilo sidhani kama tutashabikia maazimio hasi ya kimataifa yanapofanywa dhidi ya nchi yetu.
🚮🚮🚮
 
Achana na muktadha wa kifamilia, tuje kwenye Taifa na uhalisia
Watu wanafurahia vikwazo kwa sababj vinazidi kumchafua Samia
Na Samia ni muuaji, fisadi asiye mzalendo kwa hiyo watu wanafurahia vikwazo kwa sababu vinamchafua Samia na kumpa wakati mgumu kutumia akili kufikiria cha kufanya, ilihali Samia mwenyewe ana IQ ndogo
 
Tukiwa kidato cha kwanza kwenye somo la uraia, yaani civics mada ya kwanza kufundishwa ilikuwa ni familia. Sijui mitaala ya wadogo zangu Gen Z inasemaje, ila sisi tulifundishwa kuwa familia ndio msingi wa jamii zetu na Taifa letu.

Kwa muktadha huu sitakuwa nimekosea kulifananisha Taifa na familia.

Fikiri kwamba imetokea sintofahamu nyumbani kwenu, ambapo mzazi ametenda jambo ambalo baadhi ya wanafamilia hamkubaliani nalo, kwamfano kaiweka reheni nyumba ya familia ili kupata mkopo kwaajili ya starehe zake binafsi.

Baada ya mambo kuharibika akawaiteni kitako, akakiri amekosea, akamwaombeni mama yenu aseme hakutoa idhini ilimradi tu nyumba yenu mnayoishi isalimike.

Katika mazingira kama hayo ndugu yenu mmoja akatoka kuwapa taarifa bank wanaomdai mzazi wako juu ya kikao chenu, nakuwapa bank mbinu ya kufanikisha kuuza hiyo nyumba yenu kwa lengo la kumkomoa huyu mzazi kwa ufujaji mali alioufanya. Wewe kama sehemu ya familia iliyopatwa na mkasa kama huu, utakuwa na maoni gani?

Kisa hiki kina shabihiana sana na hali ya nchi yetu kwa sasa. Mpaka sasa hatubishani tena kuwa watu waliuawa, walijeruhiwa, walipoteza mali na miundombinu iliharibika.

Hili lilitokea, na hatuwezi kulifuta hata tukilaumiana vipi. Lakini kwa hali ilivyo, linaelekea kutuletea madhara makubwa zaidi tuendako mathalani kuzuiliwa kwa baadhi ya misaada ambayo kwakweli ni kichocheo cha ustawi wetu.

Chukulia sekta ya afya kwa mfano; huduma nyingi tunazipata kupitia wahisani kupitia busket fund na miradi mingine. Ikitokea nchi yetu ikakosa misaada hii ni wazi kuwa sekta kama ya afya zitatetereka sana na kuna hatari ya kuwapoteza ndugu zetu kama vile wanaoishi na VVU kwa kukosa dawa.

Sasa hawa wenzetu wanaofurahia maazimio hasi yanayofanywa na mataifa wahisani kwa makosa tuliyoyafanya Octoba 29, wanatofautiana vipi na mtoto anaeshirikiana na wadai wa baba yake kuuza nyumba ya familia kwa lengo la kumkomoa huyo baba yake?

Katika maisha tunatakiwa kujifunza kusamehe na kuendelea mbele hata kama hao tunaodhani wametukosea ni wajeuri. Kesho yetu ni bora kuliko jana, kama tunayo dhamira ya dhati ya kuifanya kesho yetu kuwa bora tunaowajibu wa kulipa gharama ya kuachilia mambo mengine yatupite.

Waingereza wanamsemo wao kuwa, tukimrushia mawe kila mbwa anayetubwekea hatutafika safari yetu.
Sio lengo langu, kumtetea mtu au kumlaumu mtu katika makala yangu, Shabaha yangu ni kuwasihi ndugu zangu kuweka maslahi ya nchi mbele kwa kauli na vitendo vyetu.

Vikwazo vikiwekwa dhidi ya nchi yetu Rais Samia atakuwa wamwisho kuathirika. Hakuna siku Rais hatalala, hatakula au hatatibiwa kwasababu nchi ina hali mbaya.

Yatakayotupata hayo ni sisi masikini wa nchi hii. Kama tukilijua hilo sidhani kama tutashabikia maazimio hasi ya kimataifa yanapofanywa dhidi ya nchi yetu.
Ina maana kubwa sana kwamba ccm imechokwa na baya lolote liwakute hata kama itatupasa kula nyasi tupo tayari
 
Back
Top Bottom