Ina maana gani kufuatwa na kivuli cha marehemu?

Mkuu kwanza pole kwa unayoyapitia naelewa inavyokuwa ngumu kuamini/kukubali kuondokewa na mpendwa wako.

Hatua 5 za mambo hayo ni kama hivi

1. Denial
2.Anger
3.Bargaining
4.Depression
5.Acceptance

Ukiangalia kwa undani naona uko bado hatua ya kwanza ambayo ni ngumu sana ila inahitaji tu umakini kufikia hatua zote tano maana sio mchezo.

Unahitaji kujitahidi kuuwezesha ubongo wako ukubali hadi kufikia hatua ya 5 ya kukubaliana tu na ni lazima maisha mengine yaendelee mkuu suicidal ideation usizipe nafasi kabisa japo ni kweli kuondokewa na mpendwa ni ngumu na haiwezekani kurudi assume ni kama umepata hitilifu ya gari kwenye tyre mwisho ukaamua utembee na rim tu hadi mahali ndio upaki kwa dharura japo ni hatari ila inawezekana.


Mwisho japo sio kwa umuhimu naamini uko bado kwa Biden naamini ni sehemu iliyo na experts wengi sana wa mental issues wanaweza kukusaidia ila kwa wabongo ukiendekeza nia hiyo watakugeuza fursa utakuja hapa kufungua muendelezo wa uzi wa kutapeliwa. Kila la heri mkuu mtumaini Mungu naye atakufanyia wepesi.

Atè então
 
Sikuwai kuja waza kwamba nitakuja kuwa na metal breeakdown,kazi imekua ngumu sana kufanya ,nilikua ninaamini nina weza handle kila kitu ,ila kumbe hili kwangu ni pigo ambalo sikuweza lihimili ,asante sana kwa sasa naona niko kweli kwnye hatua ya kwanza ambayo inanipa ugumu sana ,kweli suidcidal thoughts zinakuja kila wakati huwa naona kama hakuna haja ya kuishi ninajitahidi sana kujaribu kukubali ila kila saa nina rudi nyuma ,kwa sasa ninajitahidi kuelewa hali na nitazingatia sana ushuri wako , asante sana na ubarikiwe.
 

Bado hujakubaliana na hali ndo tatizo lako. All of this starts in your mind, your mind is playing tricks on you sababu hujataka kuukubali uhalisia.

Kama aliumwa hadi kupatwa na mauti jipe moyo kapumzika utaukubali uhalisia.
 
Bado hujakubaliana na hali ndo tatizo lako. All of this starts in your mind, your mind is playing tricks on you sababu hujataka kuukubali uhalisia.

Kama aliumwa hadi kupatwa na mauti jipe moyo kapumzika utaukubali uhalisia.
Asante sana najitahidi na nitajitahidi sana kukubali hali.
 
Pole sana bro , ila zingatia tu hayo utakaa vyema inachukua muda lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…