Ina maana gani kumsomesha mtoto kwa mamilioni ya fedha halafu anapangiwa Shule za kawaida?

Ni kweli inewahi kuwa mwalm ? ,unataka serikali ifanye nini?
 
Dah, ticha mbona hapo mwisho umeamua kuzingua...!?
 
Na pia kama huna hela kwa sasa ya kumrudisha mtoto wako kwenye shule za mamilioni, jitahidi kuwa mpole.
Niwe mpole kivipi nalipa kodi mkuu...

Baki na ujinga huohuo... Mmejenga ikulu mbili . Two state houses in a single country. Na mnaongeza Samia complex..

Hizo pesa zingeweza jenga shule special zaidi ya 50.

Hivi mmelogwa.
 
Wachangiaji wengi hapa naona mnaifanya Serikali iache kufikiri..

Na kwa akili hizi nnazoziona hapa, Samia uza nchi tu. Tutagawana pesa huko mbele.
Kati ya mambo ambayo naipongeza Serikali, basi ni hili la kuwapanga watoto wenu katika zile shule za Kata ambazo wazazi tulizikimbia hapo awali.

Watoto lazima wachangamane bhana.
 
Lakini na wewe mkuu elimu si hiyohiyo uliopata? Au wewe kuanzia awali mpka chuo umesomea Botswana.Watanzania wote waliopita shule tunafanana kifikira kwa kuwa tumekula mtaala mmoja
 
Kazi ipo.....ticha kwenye matusi umebobea
 
Lakini na wewe mkuu elimu si hiyohiyo uliopata? Au wewe kuanzia awali mpka chuo umesomea Botswana.Watanzania wote waliopita shule tunafanana kifikira kwa kuwa tumekula mtaala mmoja
Ni kweli kabisa nami nimepata elimu hiyo kama msingi.

Lakini niliamua kutoka ndani ya chupa ya elimu kandamizi kibogoyo ya Bongo.

Unapoona Waziri wa Elimu hapeleki watoto wake shule za umma maana yake ni simple tu, hana imani na mtaala anaousimamia kuwa na tija ya baadaye kielimu kwa mwanae.

Ufisadi eneo la elimu pamoja na taratibu za kijima ndo ujinga wenyewe
 
Tujitahidi tu kwenda na wakati. Serikali imegundua watoto wengi kutoka shule zao za Kata, wanasoma katika mazingira magumu. Hivyo wameona watoe kipaumbele kwa hawa watoto kwenda zile shule za vipaji.

Kwa wale watoto wa Feza, kimsingi wamesoma kama kuku wa kisasa! Hawa sasa ndiyo wanapelekwa shule za kata ili kwenda kuongeza morali ya ufaulu. Na katika hili kwa kweli tuungane kuipa serikali maua yake. πŸŒΉπŸ’πŸŒ·

Au nasema uongo ndugu yangu? πŸ˜‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…