Ina maana katika hii Serikali ajira ni kwa walimu na watu wa afya tu?

Ina maana katika hii Serikali ajira ni kwa walimu na watu wa afya tu?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,397
Reaction score
12,415
Ndugu zangu naomba kuuliza katika hii.

Ili tuache utani katika swala la ajira.

Swali langu ni kwamba: Inamaana ajira zote serikalini huwa ni kwa walimu na watu wa afya tu. Vipi kuhusu fani zingine?
 
Huko mahitaji ni mengi ndio maana wanaajiri sana, wengine wanastaafu, wapo wanaofariki, bado kuna shule nyingine hazina walimu wa kutosha mpaka leo, lakini pia shule na vituo vipya vya afya vinafunguliwa kila kona ya nchi.
 
Acha utanii mkuu
 
Mbona hizi nyingine zinatolewa kila kukicha kwenye website ya utumishi wakati wewe unapoteza muda kwenye haya majukwaa wenzio wanashindana na wanapata kazi.
 
usiwe na hofu ni issue simple, afya na elimu ndio maeneo yaliyo na ajira nyingi za moja kwa moja kutoka serikalini sisi wa fani nyingine ni swala la serikali kutengeneza mazingira ya kuzalisha ajira mpya kupitia sekta binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu naomba kuuliza katika hii.
Ili tuache utani katika swala la ajira.

Swali langu ni kwamba: Inamaana ajira zote serikalini huwa ni kwa walimu na watu wa afya tu. Vipi kuhusu fani zingine?
Serikali hua na mfumo uitwao Wengi wape
 
Kwenye sekta ya afya na elimu sidhani kama unaweza kujisifu kwamba umeajiri aise. Tunataka kuona ajira zikitengenezwa katika sekta za utalii, kilimo, biashara, benki, madini, mafuta, gesi, madawa, ujenzi n.k.
Huko ndiko kwenye maendeleo ya nchi.
usiwe na hofu ni issue simple, afya na elimu ndio maeneo yaliyo na ajira nyingi za moja kwa moja kutoka serikalini sisi wa fani nyingine ni swala la serikali kutengeneza mazingira ya kuzalisha ajira mpya kupitia sekta binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada uwe unatembelea hiyo site ya ajira ya Serikali hapo juu.

Usitegemee mhasibu au afisa utumishi akifa au kustaafu ajira hiyo itatangazwa kama ya halaiki.

Umepewa mfano mzuri sana hapo juu, shule inaweza kuwa walimu 40 lakini kada zingine mtu mmoja mmoja tu.
 
Kwenye sekta ya afya na elimu sidhani kama unaweza kujisifu kwamba umeajiri aise. Tunataka kuona ajira zikitengenezwa katika sekta za utalii, kilimo, biashara, benki, madini, mafuta, gesi, madawa, ujenzi n.k.
Huko ndiko kwenye maendeleo ya nchi.
naam umenena vyema lakiniii mahitaji ya hizo sekta sio ya mass employments kama ilivyo kwa afya na elimu mkuu , ukizingatia serikali ya the late JPM ilikua haijaweka kipaumbele kwenye ajira.

ila kukweli ajira zitaongezeka sana katika sekta zote kutokana na mikakati iliyopewa kipaumbele na serikali ya mama Samia ,hasa la kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu wa na CWT
Chama hiki kinawapambania sana
 
Ndugu zangu naomba kuuliza katika hii.
Ili tuache utani katika swala la ajira.

Swali langu ni kwamba: Inamaana ajira zote serikalini huwa ni kwa walimu na watu wa afya tu. Vipi kuhusu fani zingine?
Hajira za walimu,Afya,ulinzi,hizi ni ajira za mkupuo hivyo hata kustaafu kwake huwa hivyo hivyo kwahyo hata pengo linakua kubwa tofauti na sekta zingine ambazo hajira zake sio za makundi na kustaafu kwake kuonesha pengo Ni nadra Sana hivyo acha tu walimu na Afya waajiri wengi,nazani utakua umepata mwanga kidogo,
 
Sasa hizo zinatengenezwa? Tutengenezee ajira hizo zipo tu wala hazina faida yoyote katika uchumi hizo. Hivi mfano ajira za walimu zinachangieje kukuza uchumi. Hizo ajira zipo kila mwaka hizo.

Tunataka kuona ajira ambazo zinapimika mfano tukiona ajira za viwandani zimeongezeka tunasemaaa aaaa sasa nchi imekua na viwanda.
Vutia wawekezaji jenga viwanda hizo ndio ajira tunazozihitaji sanaa
 
Back
Top Bottom