Ina maana kocha Mbwana Makata haruhusiwi kufundisha hata timu ya shule au chuo?

Ina maana kocha Mbwana Makata haruhusiwi kufundisha hata timu ya shule au chuo?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Eti wakuu, TFF wanamiliki mpira wote wa miguu nchini? Maana huyu kapewa adhabu ya kutojihusisha na mpira wa miguu nchini kwa miaka mitano. Inamaana hata shule au chuo haruhusiwi kufanya ukocha?
 
Binafsi naliangalia hili swala kitofauti kidogo

Timu kama timu inakua na idara zake na wakuu wa idara wanakua wanawakilisha maamuzi ya timu

Timu ikigoma kulipa kodi na mtunza maduhuli akagoma kwamba timu inaonewa maana yake hapo huo ndio msimamo wa club na sio muhasibu

Kamati ya usajili ikifanya makosa kiusajili hatahukumiwa mwenyekiti wa kamati itaadhibiwa club

Mwenye maamuzi ya club ndani ya uwanja ni KOCHA
Maamuzi yoyote yasio ya kibinafsi hayo ni maamuzi ya club na sio kocha

Timu inaambatana na baadhi ya viongozi na wote walikuwepo uwanjani na kusapoti maamuzi pengine wao ndio walimuagiza asiingize timu maana wao ndio walikua na muda wa kukagua kama ambulance ipo au la, maana kazi ya kocha ni uwanjani tu lakini protokali zingine zote wanakuwepo wawakilishi wa club kushughulikia

Sasa inakuaje Makata ana adhibiwa kama Makata personal? Inakua ni kama vile makata katukana au kampiga mtu au kafanya kosa lina muhusu personal

Kwanini maamuzi kama club yamuumize makata peke yake?
Vipi viongozi wawakilishi si walikuwepo? Si walisapoti?

Au Makata aliketa ubabe yeye kama yeye tu na club ika mruka?

Kwa muktadha huu sioni kama Kocha Makata katendewa haki

Club ingepigwa fine na kuporwa point
 
Kuna mwingine anasubiri kula mvua kisa kaandika "Ligi dhaifu"
 
Back
Top Bottom