Binafsi naliangalia hili swala kitofauti kidogo
Timu kama timu inakua na idara zake na wakuu wa idara wanakua wanawakilisha maamuzi ya timu
Timu ikigoma kulipa kodi na mtunza maduhuli akagoma kwamba timu inaonewa maana yake hapo huo ndio msimamo wa club na sio muhasibu
Kamati ya usajili ikifanya makosa kiusajili hatahukumiwa mwenyekiti wa kamati itaadhibiwa club
Mwenye maamuzi ya club ndani ya uwanja ni KOCHA
Maamuzi yoyote yasio ya kibinafsi hayo ni maamuzi ya club na sio kocha
Timu inaambatana na baadhi ya viongozi na wote walikuwepo uwanjani na kusapoti maamuzi pengine wao ndio walimuagiza asiingize timu maana wao ndio walikua na muda wa kukagua kama ambulance ipo au la, maana kazi ya kocha ni uwanjani tu lakini protokali zingine zote wanakuwepo wawakilishi wa club kushughulikia
Sasa inakuaje Makata ana adhibiwa kama Makata personal? Inakua ni kama vile makata katukana au kampiga mtu au kafanya kosa lina muhusu personal
Kwanini maamuzi kama club yamuumize makata peke yake?
Vipi viongozi wawakilishi si walikuwepo? Si walisapoti?
Au Makata aliketa ubabe yeye kama yeye tu na club ika mruka?
Kwa muktadha huu sioni kama Kocha Makata katendewa haki
Club ingepigwa fine na kuporwa point