Ina maana ripoti zilizopita za CAG zilizokuwa zinawasilishwa ndani ya utawala Wa awamu ya 5 zilikuwa zinafanyiwa "editing"?

Yaani unataka nijiongeze kuwaamini clouds lakini hutaki kuiongeza kuamini taarifa ya CAG. [emoji23][emoji23][emoji23] Kama Clouds wana nyaraka waweke hadharani ni kitu cha kawaida katika auditing.

Lakini pia unatakiwa kujua CAG hakukagua Clouds amekagua wizara ya Mali Asili na Utalii sasa kama ameomba wizara documents za mkataba na hakupewa ulitaka awafuate Clouds ndio wammpe?

Swali la kujiuliza kwa nini Clouds wana documents (kama kweli wanazo) na wizara hawana?
 
Wakati wa hayati na yeye alikuwa anafa ile kauli ya Idd Amin
"Una haki na uhuru wa kuongea ila sikuhakikishi uhuru wako baada ya kuongea"
 
Hizo risiti za clouds umeziona mkuu?

Clouds katka majibu na utetezi wao , wamesema vitu vingi, ila mwisho wa siku kwenye swala la risiti, wamekiri kutokuwepo kwa risiti za kielectroniki.
Wakiwa katika kiredio chao wanavopiga kelele ukiuza toa risiti ukinunua dai risiti tena za efd wao hawana wapuuzi hao.
 
Bado tunaendelea na maombi yetu, Maulana atufanyie wepesi bungeni kama alivyotufanyia Ikulu...
Hahaaaaa........

Wewe humtakii mema yule Supikaaa wetu wa Jumba letu la uwakilishi!
 
Ngoja tusubiri,Ukweli utajulikana maana tayari Maliasili kuna mtu kasimamishwa( Zamani tulizoea neno Katumbuliwa)
 
Huo ndiyo ukweli maana bwana yule kamwe asingeweza kukubali report imuumbue.

Kufuatia kuaga dunia ndiyo sasa watendaji walio chini yake ndiyo wanakuwa huru na kutenda kazi kwa uhuru.
 
Mkuu ndani ya miaka mitano iliyopita hapakuwa na ripoti za CAG zaidi ya usanii uliopitiliza. Watu "walishikiwa bastola" kuwasilisha kile mkubwa alipenda kukisikia. Ona sasa wanavyofunguka; you can note something.
Hii tabia ilishajikita hata kwenye baadhi ya wafuasi wake kuamini kuwa bwana mkubwa yeye kamwe hawezi kutenda makosa .

Kama ilifikia mahala wafuasi wake wakamfananisha na malaika au mtume huoni kuwa tulishafika kwenye kilele cha utumwa wa akili?
 
Usiamini ripoti ya CAG 100%.Km Clouds Media Group wana uthibitisho wa walipo ya risiti na CAG alipewa,lakini bado report yake inaonyesha kuna ufujaji kwanini tumuamini?
CAG ni taasisi iliyo pewa mamlaka kamili ya kukagua na wala usituletee huo ujinga wako wa kichawi.

Kama CAG amesema then wewe nani tukuamini?
 
Bado tunasubir sakata la manunuzi ya ndege kinyume na sheria/kanuni za manunuzi za serikali
 
Kati ya sh bilioni 60 ambazo CAG anadai ATCL ilipata hasara, sh bilioni 15 zililipwa wakala wa ndege za serikali kama gharama za ukodishaji ndege kipindi ambacho ndege zilikuwa haziruki kutokana na corona. Hii ni kama kuchukua pesa mfuko wa kushoto na kuweka mfuko wa kulia, kimsingi hii sio hasara maana ni serikali hiyo hiyo imechukua hizo pesa. Ni udhaifu wa mkataba kati ya taasisi mbili za serikali. Hiyo pesa haijapotea kama inavyokuzwa na CAG..
 
... CAG kaibua audit queries; wanachopaswa Clouds kufanya ni kujibu hizo queries kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
 
Usiamini ripoti ya CAG 100%.Km Clouds Media Group wana uthibitisho wa walipo ya risiti na CAG alipewa,lakini bado report yake inaonyesha kuna ufujaji kwanini tumuamini?
Watanzania woote wanaoipenda nchi yao wana imani kubwa na report ya CSG kwa kila kipengele alicho kitaja kwenye hiyo report.

Nyie CHAWA wa jiwe endeleeni kuandamana .
 
Tumshukuru Mungu kwa muujiza kutuepusha na balaa life time, kasikia kilio cha Watanzania, nina imani Mama atajenga mifumo imara kwa katiba bora.
Na hili ni pigo kuu kwa wale mafarisayo ambao mpaka sasa hawaamini kama malaika wao hatunaye tena kwa mapenzi ya mungu.
 
Anaelewa sana ila huyo ni kati ya CHAWA wa mwendazake ambaye anafaidika na uwepo wake.
 
CAG ni taasisi iliyo pewa mamlaka kamili ya kukagua na wala usituletee huo ujinga wako wa kichawi.

Kama CAG amesema then wewe nani tukuamini?
Toa hoja utaeleweka mkuu sio kutukana. Hili ni jukwa la kutoa mawazo na kubishana/ kushindana kwa hoja.Kila mtu humu anaweza kutukana ila tunaheshimu utu na mawazo ya kila mtu.
 
Watanzania woote wanaoipenda nchi yao wana imani kubwa na report ya CSG kwa kila kipengele alicho kitaja kwenye hiyo report.

Nyie CHAWA wa jiwe endeleeni kuandamana .
JPM for life. No one like him
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…