Ina maana ripoti zilizopita za CAG zilizokuwa zinawasilishwa ndani ya utawala Wa awamu ya 5 zilikuwa zinafanyiwa "editing"?

Hebu jiongeze ndugu yangu,yaani taasisi km Clouds waseme kuwa wanarisiti wakati hawana? Unazani baada ya ripoti ya CAG mambo huishia hapohapo. Hivi tunavyoongea taasisi na mashirika yote yaliyoshutumiwa yatatakiwa kujieleza na kutoa uthibitisho/utetezi wao. Huko ndo wataonyesha hizo risiti.
Yaani unataka nijiongeze kuwaamini clouds lakini hutaki kuiongeza kuamini taarifa ya CAG. [emoji23][emoji23][emoji23] Kama Clouds wana nyaraka waweke hadharani ni kitu cha kawaida katika auditing.

Lakini pia unatakiwa kujua CAG hakukagua Clouds amekagua wizara ya Mali Asili na Utalii sasa kama ameomba wizara documents za mkataba na hakupewa ulitaka awafuate Clouds ndio wammpe?

Swali la kujiuliza kwa nini Clouds wana documents (kama kweli wanazo) na wizara hawana?
 
Wakati wa hayati na yeye alikuwa anafa ile kauli ya Idd Amin
"Una haki na uhuru wa kuongea ila sikuhakikishi uhuru wako baada ya kuongea"
 
Hizo risiti za clouds umeziona mkuu?

Clouds katka majibu na utetezi wao , wamesema vitu vingi, ila mwisho wa siku kwenye swala la risiti, wamekiri kutokuwepo kwa risiti za kielectroniki.
Wakiwa katika kiredio chao wanavopiga kelele ukiuza toa risiti ukinunua dai risiti tena za efd wao hawana wapuuzi hao.
 
Bado tunaendelea na maombi yetu, Maulana atufanyie wepesi bungeni kama alivyotufanyia Ikulu...
Hahaaaaa........

Wewe humtakii mema yule Supikaaa wetu wa Jumba letu la uwakilishi!
 
Yaani unataka nijiongeze kuwaamini clouds lakini hutaki kuiongeza kuamini taarifa ya CAG. [emoji23][emoji23][emoji23] Kama Clouds wana nyaraka waweke hadharani ni kitu cha kawaida katika auditing.

Lakini pia unatakiwa kujua CAG hakukagua Clouds amekagua wizara ya Mali Asili na Utalii sasa kama ameomba wizara documents za mkataba na hakupewa ulitaka awafuate Clouds ndio wammpe?

Swali la kujiuliza kwa nini Clouds wana documents (kama kweli wanazo) na wizara hawana?
Ngoja tusubiri,Ukweli utajulikana maana tayari Maliasili kuna mtu kasimamishwa( Zamani tulizoea neno Katumbuliwa)
 
Inasikitisha sana tena inahuzinisha kuona ripoti ya CAG ya safari hii baada ya mwendazake kuzikwa, ikiibua madudu mengi mno, tofauti na ripoti zilizokuwa zikiwakilishwa hapo nyuma wakati wa utawala huu wa awamu ya 5 ambazo zilikuwa zinampamba sana mwendazake na kueleza Taifa letu linapaa sana kiuchumi!

Ushahidi wa mazingira ya ninachokisema hapa ni kutokana na kauli aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akipokea ripoti hiyo akimwelekeza CAG kicheere kuwa hapaswi kuwa na kigugumizi chochote na anapaswa kueleza kila kitu kwa uwazi katika ripoti yake ili watanzania ambao ndiyo walipa kodi wa nchi hii, waelewe namna pesa yao inavyotumika.

Nasema kuwa ripoti za awali zilikuwa zinakuwa "edited" kwa kuwa katika ripoti za nyuma za CAG tulikuwa tukiambiwa kuwa ATCL imetengeneza faida ya Shilingi bilioni 28, wakati katika ripoti hii ya CAG inasema wazi kuwa katika miaka 5 ya nyuma mfululizo, ATCL imekuwa ikipata hasara na katika mwaka Wa fedha wa 2019/2020 ilipata hasara ya shilingi bilioni 60!

Vile vile tujikumbishe kile kilichompata CAG aliyepita, Musa Assad baada ya kuibua ufisadi wa shilingi trillion 1.5 nini kilimpata baada ya kuibua ufisadi huo?

Kila mwananchi wa nchi hii ni shahidi namna CAG huyo alivyoundiwa "zengwe" na Spika Ndugai na Mwendazake, kwa kudhalilishwa sana hadi akatishiwa na Spika Ndugai kuwa akigoma kuja kuhojiwa na Kamati yake ya maadili, basi ataviagiza vyombo "vyake" vya dola vimlete pale bungeni akiwa amefungwa pingu mikononi!

Nini kilimpata CAG huyo kila mwananchi ni shahidi, namna CAG huyo alivyofurushwa kwa nguvu na kutimuliwa kazi!

Hivi kwa hii "trend" inayoendelea hapa nchini, ni mwananchi gani atakayeamini takwimu zilizokuwa zonatolewa chini ya utawala wa mwendazake, ambazo kwa maoni ya wananchi walio wengi zilikuwa ni za kughushi na zilizojaa uzushi na propaganda nyingi?
Huo ndiyo ukweli maana bwana yule kamwe asingeweza kukubali report imuumbue.

Kufuatia kuaga dunia ndiyo sasa watendaji walio chini yake ndiyo wanakuwa huru na kutenda kazi kwa uhuru.
 
Mkuu ndani ya miaka mitano iliyopita hapakuwa na ripoti za CAG zaidi ya usanii uliopitiliza. Watu "walishikiwa bastola" kuwasilisha kile mkubwa alipenda kukisikia. Ona sasa wanavyofunguka; you can note something.
Hii tabia ilishajikita hata kwenye baadhi ya wafuasi wake kuamini kuwa bwana mkubwa yeye kamwe hawezi kutenda makosa .

Kama ilifikia mahala wafuasi wake wakamfananisha na malaika au mtume huoni kuwa tulishafika kwenye kilele cha utumwa wa akili?
 
Usiamini ripoti ya CAG 100%.Km Clouds Media Group wana uthibitisho wa walipo ya risiti na CAG alipewa,lakini bado report yake inaonyesha kuna ufujaji kwanini tumuamini?
CAG ni taasisi iliyo pewa mamlaka kamili ya kukagua na wala usituletee huo ujinga wako wa kichawi.

Kama CAG amesema then wewe nani tukuamini?
 
Bado tunasubir sakata la manunuzi ya ndege kinyume na sheria/kanuni za manunuzi za serikali
 
Inasikitisha sana tena inahuzinisha kuona ripoti ya CAG ya safari hii baada ya mwendazake kuzikwa, ikiibua madudu mengi mno, tofauti na ripoti zilizokuwa zikiwakilishwa hapo nyuma wakati wa utawala huu wa awamu ya 5 ambazo zilikuwa zinampamba sana mwendazake na kueleza Taifa letu linapaa sana kiuchumi!

Ushahidi wa mazingira ya ninachokisema hapa ni kutokana na kauli aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akipokea ripoti hiyo akimwelekeza CAG kicheere kuwa hapaswi kuwa na kigugumizi chochote na anapaswa kueleza kila kitu kwa uwazi katika ripoti yake ili watanzania ambao ndiyo walipa kodi wa nchi hii, waelewe namna pesa yao inavyotumika.

Nasema kuwa ripoti za awali zilikuwa zinakuwa "edited" kwa kuwa katika ripoti za nyuma za CAG tulikuwa tukiambiwa kuwa ATCL imetengeneza faida ya Shilingi bilioni 28, wakati katika ripoti hii ya CAG inasema wazi kuwa katika miaka 5 ya nyuma mfululizo, ATCL imekuwa ikipata hasara na katika mwaka Wa fedha wa 2019/2020 ilipata hasara ya shilingi bilioni 60!

Vile vile tujikumbishe kile kilichompata CAG aliyepita, Musa Assad baada ya kuibua ufisadi wa shilingi trillion 1.5 nini kilimpata baada ya kuibua ufisadi huo?

Kila mwananchi wa nchi hii ni shahidi namna CAG huyo alivyoundiwa "zengwe" na Spika Ndugai na Mwendazake, kwa kudhalilishwa sana hadi akatishiwa na Spika Ndugai kuwa akigoma kuja kuhojiwa na Kamati yake ya maadili, basi ataviagiza vyombo "vyake" vya dola vimlete pale bungeni akiwa amefungwa pingu mikononi!

Nini kilimpata CAG huyo kila mwananchi ni shahidi, namna CAG huyo alivyofurushwa kwa nguvu na kutimuliwa kazi!

Hivi kwa hii "trend" inayoendelea hapa nchini, ni mwananchi gani atakayeamini takwimu zilizokuwa zonatolewa chini ya utawala wa mwendazake, ambazo kwa maoni ya wananchi walio wengi zilikuwa ni za kughushi na zilizojaa uzushi na propaganda nyingi?
Kati ya sh bilioni 60 ambazo CAG anadai ATCL ilipata hasara, sh bilioni 15 zililipwa wakala wa ndege za serikali kama gharama za ukodishaji ndege kipindi ambacho ndege zilikuwa haziruki kutokana na corona. Hii ni kama kuchukua pesa mfuko wa kushoto na kuweka mfuko wa kulia, kimsingi hii sio hasara maana ni serikali hiyo hiyo imechukua hizo pesa. Ni udhaifu wa mkataba kati ya taasisi mbili za serikali. Hiyo pesa haijapotea kama inavyokuzwa na CAG..
 
Hebu jiongeze ndugu yangu,yaani taasisi km Clouds waseme kuwa wanarisiti wakati hawana? Unazani baada ya ripoti ya CAG mambo huishia hapohapo. Hivi tunavyoongea taasisi na mashirika yote yaliyoshutumiwa yatatakiwa kujieleza na kutoa uthibitisho/utetezi wao. Huko ndo wataonyesha hizo risiti.
... CAG kaibua audit queries; wanachopaswa Clouds kufanya ni kujibu hizo queries kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
 
Usiamini ripoti ya CAG 100%.Km Clouds Media Group wana uthibitisho wa walipo ya risiti na CAG alipewa,lakini bado report yake inaonyesha kuna ufujaji kwanini tumuamini?
Watanzania woote wanaoipenda nchi yao wana imani kubwa na report ya CSG kwa kila kipengele alicho kitaja kwenye hiyo report.

Nyie CHAWA wa jiwe endeleeni kuandamana .
 
Tumshukuru Mungu kwa muujiza kutuepusha na balaa life time, kasikia kilio cha Watanzania, nina imani Mama atajenga mifumo imara kwa katiba bora.
Na hili ni pigo kuu kwa wale mafarisayo ambao mpaka sasa hawaamini kama malaika wao hatunaye tena kwa mapenzi ya mungu.
 
Wewe na genge lako ndo hamuamini usitulishe matangopori. CAG ameongelea kutokuwepo kwa mkataba wa malipo na stakabadhi za kielektlonic. Unajua anamaanisha nini? Unamlipaje mtu mil.600+ bila maandishi zaidi ya stakabadhi za kuandika kwa mkono?
Kama hujaelewa niko tayari kukuelewesha zaidi.
Anaelewa sana ila huyo ni kati ya CHAWA wa mwendazake ambaye anafaidika na uwepo wake.
 
CAG ni taasisi iliyo pewa mamlaka kamili ya kukagua na wala usituletee huo ujinga wako wa kichawi.

Kama CAG amesema then wewe nani tukuamini?
Toa hoja utaeleweka mkuu sio kutukana. Hili ni jukwa la kutoa mawazo na kubishana/ kushindana kwa hoja.Kila mtu humu anaweza kutukana ila tunaheshimu utu na mawazo ya kila mtu.
 
Watanzania woote wanaoipenda nchi yao wana imani kubwa na report ya CSG kwa kila kipengele alicho kitaja kwenye hiyo report.

Nyie CHAWA wa jiwe endeleeni kuandamana .
JPM for life. No one like him
 
Back
Top Bottom