Kwanini inajengwa fikra kuwa wanafunzi kujiandikisha ni kosa kama wametimiza miaka 18? Na kwanini tunahisi hawa wanafunzi ni wa chama fulani wakati hawajatuonesha kadi za vyama vyao?
Pia mbona kama kuna kuchanganya kujiandikisha na kupiga kura? Ieleweke wazi kua hili ni zoezi la uandikisha wapiga kura. Baadae au hata sasa vyama vifanye hamasa au ushawishi kwa waliojiandikisha ili wawapigie kura.
Tunajinasibu kwa kuamini kuwa mabadiriko ya kweli yataletwa na vijana, wakati huo hatutaki vijana hususani wanafunzi kujiandikisha. Ieleweke kua kama hakuna waliojiandikisha kupiga kura hata utoe sera gani hutapata kura.
Tena ingetolewa fursa vyama vyote kupita shuleni na vyuoni kuhamasisha wanafunzi waliotikiza vigezo kujiandikisha. Labda kuondoa utata ingetakiwa kila anayejiandioisha aje na kitambulisho halali chenye umri wake.
Wanafunzi wanahukumiwa kwakua wanakuja na sare zao lakini kuna mtu anaweza kuja kujiandikisha bila kuwa mwanafunzi lakini umri wake mdogo. Nilitamani kuona video ya wanafunzi wakilazimishwa kuniandikisha. Ila pamoja na majukumu mengine ya walimu, ni kazi yao ya msingi kuhamasisha wanafunzi kujiandikisha. Kwa hilo tusiwatuhumu kuwa wanakibeba chama fulani.
Pia hiyo aina ya uongeaji/lafudhi inanipa shaka kama hapo ni Tabora.
Ni maoni yangu.