Inabidi Watanzania tumuombe msamaha Rais Magufuli


Mimi huyo sio baba yangu ila ni mwananchi wa Tanzania na huyo ndio Rais wa nchi. Hakuna ibara au kifungu chochote cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kinasema Rais ni baba wa wananchi wote wa Tanzania.
 
...JK alipokkuwa Mkuu,JPM alikuwa mmoja wa washauri wake.
Mbaya zaidi inaonekana mwenyewe ameshasahau kwamba alikuwa ni sehemu ya huu utawala tangia awamu ya tatu akishiriki mambo yote ya hovyo!
 
Mimi huyo sio baba yangu ila ni mwananchi wa Tanzania na huyo ndio Rais wa nchi. Hakuna ibara au kifungu chochote cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kinasema Rais ni baba wa wananchi wote wa Tanzania.
Kwani baba anasifa zipi ukiondoa ya kukuzaa??
 
Mnasema njaa njaa mnataka mm ndio nikawapikiee??...hiyo kauli live kutoka kwa Mhe. rais mpendwaa......kaz ipooo
 
Alidhani mtu kama wewe utamtia nguvu kwa kumshukuru kwa mema anayotenda kipindi kaanza kurekebisha nchi hadi sasa, kumbe yale ya upande wa pili ndio unashabikia!!!...akachoka akaona aanze kufanya tu kwa moyo Mungu atamlipa maana hafanyi kuifurahisha mishetani.
Tukisema usikojoe hapa!....tunamaanisha hivyo...ukikojoa tukikunyonga usije ukaanza kusema mbona adhabu ni kubwa, swala wewe ukifa hicho kitendo OVU hakitakuwepo na kikijirudia inamaana mtendaji yupo radhi kufa basi
 
Binafsi siwezi muomba msamaha binadamu mwenzangu ambaye najua sijamkosea
 
Heri nyie wenye baba yule
 
Baba hakuitaka hii kazi wamembambika kwa ushindi wa mezani hicho kitu kinamuuma sana hana raha kabisa. Alikuwa anatania tuu wakampa ushindi wa nyuma ya pazia, sasa anajuta na akipata pa kutolea hasira anafanya kweli.
 
Kuhusu hili niko upande mwongine na wala siko naye, pesa za rambirambi kuliwa na kuviacha vichanga vinanyeshewa wakati pesa yao umebugia si jambo dogo. Mungu mwenyewe ndo atamsamehe akiona inamfaa na si sisi.
 
Ulimpigia kura?
 
Kama kuna kosa kubwa ambalo nimelifanya kwa miaka ya hivi karibuni na linaniuma basi kupanga foleni halafu kumchagua huyu mkuu.
Just dont regret yet it might be too early.
Nna uhakika ni pressure ya hiyo post. Hakujua ikoje. Ina pressure gani.
Mwisho wake kakuta matarajio yake kuyatimiza sio easy kama alivyodhani.

Sasa ku cope na hiyo post imekya ni challenge kubwa. Nna uhakika ingekua ni kitu rahisi angeomba kuresign alafu aombe ridhaa labda baadae hivi
 
Viashiria Vya kiongozi mzuri wa nchi;
Kwanza Mcha Mungu wakweli kisha,
1. Upeo,mwelewa wa shida za watu na mshirikishaji mzuri wa watu (uchumi sayansi na technolojia)
2. Ajuwe diplomasia,kuheshimu watu na kujiheshimu.
3. Mtulivu,mstahimilivu na asiye na vinyongo. Awapende watu wooote na kuwatendea haki bila kubagua kabisa,kabila,rangi ama vyama Vya siasa nk.
 
Kama ni bifu acha tulibebe tu mpaka mwisho
 
Kuna ukweli hapa. Maana ukifuatiliahutuba zake, unakata tamaa halafu unamuombea tu. Rais ukatamani kuwa IGP? Au kushughulishwa na mashabiki wa yanga wanaofuta gari ya mwenyekiti wao? Kikwete alijiandaa na aliupenda urais, mbali ya experiece ya chama aliokuwa nayo. Kama engelipata sapoti nzuri huenda angelifanya makubwa sana.
 
Sasa tumuombe radhi kwa kosa lipi tulilo mkosea? Kwa kuanza hebu orodhesha makosa matano ambayo watanzania wamemkosea mheshimiwa rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…