Hii ni askari magereza hapo bado askari wapelelezi hawajaongea... Ukienda kufungua kesi polisi na kama mtuhumiwa ni wa kukamatwa hapo ndio utajua kwanini tunaililia Tanganyika... Na heri mtuhumiwa awe hayuko mbali utagharamia pesa ndogo kama usafiri ama kujaza mafuta gari ya polisi na posho yao kidogo(rushwa)
Kama yuko mkoa na ukiangaliwa unajiweza kidogo utagharamia
Chakula
Usafiri
Malazi
Pishi
Mpaka vinywaji vya mpelelezi
Mazingira haya yamesababisha madhila kwa wengi hasa kwenye upande wa kukosa haki, kukomoana na kubambikiana kesi.. Always mwenye nacho akipewa haki zote!
Imagine unagharamikia kwenda kumkamata mtuhumiwa wako.. Mkifika huko akaonekana anajiweza anaanza kupewa VIP treatment hukohuko na mkifika kituoni si ajabu ukageuziwa kibao wewe mwenye mtuhumiwa wako.. Haya yameshatokea sana.. Kuna mfano halisi nitatoa hapo chini[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Mwaka 2005 kuna mwananchi alitapeliwa shilingi milion kumi Kwenye biashara fulani na raia mmoja wa Kigeni (mzungu).. Baadae mzungu akakubali kurudisha ile pesa lakini sound zikawa nyingi mpaka jamaa akaamua kwenda police
Kwakuwa eneo la tukio lilikuwa Mikocheni hivyo alienda Oysterbay police.. Kufika akafungua kesi na kuambiwa inabidi kwenda kumkamata mtuhumiwa lakini hawakuwa na mafuta.. Jamaa akajitolea gari lake..
Wakaenda mpaka anapoishi mzungu kufika dogo akaachwa kwenye gari.. Wakaingia ndani maaskari wawili alioenda naye
Baada ya kama dk 20 hivi akatoka askari mmoja na kumwambia yule mwananchi aondoke kwanza watamtaarifu aende kituoni kesho yake kwakuwa wanafanya mawasiliano na ubalozini na kwamba kuna afisa ataenda pale
Japo alitia shaka kidogo lakini akaamua kuwaamini.. Hapo walishakubaliana pesa ikilipwa wale maaskari atawapa milion moja na wakawa tayari wameshachukua laki mbili..
Inaendelea....
Sent using
Jamii Forums mobile app