Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 7,186
- 14,274
Mwisho wake ulikuwaje Kaka?Inaendelea...
Kilichotokea ni kwamba wale maaskari walipofika kwa mzungu wakaona hapa kuna dili... Hivyo wakamtishatisha pale kwamba anapelekwa mahabusu kisha mahakamani
Mzungu akalainika akaomba yaishe palepale lakini wakamkazia kwamba hiyo ngoma ni mpaka mahakamani.. Pona yake amlipe yule mwananchi pesa yake na wao awape dola 2000 halafu watampeleka mpaka airport asepe
Mzungu akaona hii imekaa njema akatoa dola elfu tano sawa na around milion kumi akawapa.. Kwahiyo yule askari aliyeshuka chini kumwambia mwananchi aondoke alikuwa tayari ana pesa yake yote lakini hakumpa hata mia
Aliporudi juu wakamwambia kila kitu kiko sawa hivyo afungashe fasta.. Mzungu akiwa anajifungasha wale maaskari wakapiga simu airport na kufanya booking ya siku ile usiku kwa mtuhumiwa aliyetakiwa kuondoka nchini maramoja
Wakaondoka na mzungu mpaka terminal hotel wakampa chumba apumzike mpaka usiku na mizigo awaachie waitangulize airport na kama ana pesa zake azifiche vizuri kwenye begi kubwa
Mzungu akaingia kingi, akamaliza nao chao kilichobaki akasunda kwenye begi wakamuacha chumbani wakaondoka na mabegi yake!
Walipoondoka na mabegi walifungua na kuchukua pesa yote usd 55,000, na usiku ulipofika wakampakia kwenye ndege akaondoka bila kujua keshapigwa!
Kesho yake yule mwananchi anafika polisi Oysterbay anaambiwa mtuhumiwa wake katoroka na wanamtafuta!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app