DOKEZO Inadaiwa Askari Magereza wa Ukonga wanajigharamikia wenyewe wanaposafirisha Wafungwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

wanyimeni wakija kuomba mafuta na vipuli vya magari yao.

serikali inafuga mbwa kwa kutegemea matapishi ya walevi,kwanini haitaki kuwajibika kwa swala lake!!!
 
Tunarekebisha mafao ya wenza wa viongozi tutawarudia baadae kidogo mkuu naripoti kutoka lumumba.
 
Naongeza kuwa kutokana kuwepo kwa utamaduni wa hofu imepelekea pia baadhi ya Askari Magereza kukosa pesa za likizo pamoja na pesa nyingine ambazo utakiwa kutolewa kwa nyakati tofauti kulingana na taratibu.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri sana huu

Ova
 
eti askari wanajigharamikia kuwasafirisha wafungwa mkoani, wewe, nyara ya serikali haisafirishwi hovyohovyo.......

we sema tu askari magereza wana malimbikizo ya madeni yao mbalimbali ya muda mrefu hayajalipwa, na hilo ni kweli lipo kwenye taasisi mbalimbali nchini na mara kadhaa serikali imeshalitolea maelezo na polepole madeni yale yameanza kulipwa kulipwa,

na huenda mnyetishaji wa taarrifa hii hajafikiwa bado,
na kwasabb anaamini atalipwa ndio maana ananyetisha taarifa kwa kificho.
Ni uvumilivu na subra ndio tabu miongoni mwa watumishi ndio maana jambo hili linawasiliswa kwa hisia na kwa namna mbalimbali kwa umma , lakini Jambo hilo katika ujumla wake Ni malimbikizo ya madai mbalimbali ya watumishi taasisi mbalimbali.
 
😂🤣Sasa si mzanzibari huyo
Kina yehee,kazi hawawezi ndo mana wanakuwa makondoo

Kumfanya Askari ajilipie Safari ya kikazi,ni kutengeneza mianya ya rushwa na haki kutotendeka mahakamani.

Ni kosa kubwa
Wanatakiwa wawalipe manake hiyo ni posho ya kazi,na si jukumu la Askari kumsafirisha mfungwa kwa kujilipia🙏
 

msemaji wa serikali wizara ya mambo ya ndani,vipi kuhusu kikokotoo kwa askari ni kweli kwamba serikali haioni ama imeona inapuuzia???
 
Hii ni askari magereza hapo bado askari wapelelezi hawajaongea... Ukienda kufungua kesi polisi na kama mtuhumiwa ni wa kukamatwa hapo ndio utajua kwanini tunaililia Tanganyika... Na heri mtuhumiwa awe hayuko mbali utagharamia pesa ndogo kama usafiri ama kujaza mafuta gari ya polisi na posho yao kidogo(rushwa)
Kama yuko mkoa na ukiangaliwa unajiweza kidogo utagharamia
Chakula
Usafiri
Malazi
Pishi
Mpaka vinywaji vya mpelelezi

Mazingira haya yamesababisha madhila kwa wengi hasa kwenye upande wa kukosa haki, kukomoana na kubambikiana kesi.. Always mwenye nacho akipewa haki zote!

Imagine unagharamikia kwenda kumkamata mtuhumiwa wako.. Mkifika huko akaonekana anajiweza anaanza kupewa VIP treatment hukohuko na mkifika kituoni si ajabu ukageuziwa kibao wewe mwenye mtuhumiwa wako.. Haya yameshatokea sana.. Kuna mfano halisi nitatoa hapo chini[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Mwaka 2005 kuna mwananchi alitapeliwa shilingi milion kumi Kwenye biashara fulani na raia mmoja wa Kigeni (mzungu).. Baadae mzungu akakubali kurudisha ile pesa lakini sound zikawa nyingi mpaka jamaa akaamua kwenda police
Kwakuwa eneo la tukio lilikuwa Mikocheni hivyo alienda Oysterbay police.. Kufika akafungua kesi na kuambiwa inabidi kwenda kumkamata mtuhumiwa lakini hawakuwa na mafuta.. Jamaa akajitolea gari lake..

Wakaenda mpaka anapoishi mzungu kufika dogo akaachwa kwenye gari.. Wakaingia ndani maaskari wawili alioenda naye
Baada ya kama dk 20 hivi akatoka askari mmoja na kumwambia yule mwananchi aondoke kwanza watamtaarifu aende kituoni kesho yake kwakuwa wanafanya mawasiliano na ubalozini na kwamba kuna afisa ataenda pale

Japo alitia shaka kidogo lakini akaamua kuwaamini.. Hapo walishakubaliana pesa ikilipwa wale maaskari atawapa milion moja na wakawa tayari wameshachukua laki mbili..

Inaendelea....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kali.
Shida jeshi la Magereza lina makachero wengi sana, ukiamza ku organize tu rafiki yako tena muliyeanza kazi siku moja anakuchoma.
Ndipo utajuta na kusaga meno
 
msemaji wa serikali wizara ya mambo ya ndani,vipi kuhusu kikokotoo kwa askari ni kweli kwamba serikali haioni ama imeona inapuuzia???
suala la kikokotoo si suala la askari pekee, ni suala la jumla kwenye ajira sekta binafsi watumishi wale wana maoni, malalamiko na Mapendekezo yao juu ya kikokotoo na fao la kujitoa na vilevile sekta ya umma kuna Mapendekezo, malalamiko na maoni yao juu ya kikokotoo.
Serikali sikivu na imara iko kazini, na katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha majawabu mujarabu yatatolewa kuhusu jambo hili la kikokotoo...
 
Ahahaha
Nimecheka kama mazuri vile
Yaani mtuhumiwa wako anaanza kupepewa na maafande kisa ana shekeli then wewe unaambiwa vua viatu wakusweke ndani 😭😭😭
 
mambo mengine umeyaeleza sawa sawia, ila hicho kitanganyika huwa ni kinini?
 

semaji la serikali ya ccm wizara ya mambo ya ndani,zipo taasisi hazihusiki kabisa na kikotoo hiki ikiwamo wizara ya ulinzi,ofisi ya rais,wakati serikali hii sikivu inaamua kupitisha kikokotoo ilizingatia nini???maana hawa watumishi wizara ya mambo ya ndani ni wao pekee wana mishahara(MBUZI)ukizingatia na watumishi wa taasisi nyingine.
mfano mwalimu anayemaliza utumishi leo wa miaka 30,kwa kikokotoo chake hakosi kiinua mgongo angarau 70ml,wakati askari wa mambo ya ndani kwa kwa hesabu hizo hizo kama amebahatika sana ni milioni 25.serikali sikivu inasikiliza mziki ama inasikiliza malalamiko ya wananchi na watumishi wake???

kwanini haikufikiria kuboresha kwanza maslahi yao kisha iwawekee kikokotoo badala yake imefanya kama kuwatwisha mzigo mzito kwenye mlima mkali na kiu??

kwako semaji.
 
Msheshimiwa Magufuli kipindi anamteua Afande Brigadier Mzee hakufanya bahati mbaya. Magereza ni zaidi ya jipu ni hivyo tu ni askari hawawezi Andaman.

Magereza mpaka uniform za kazi kama mzungumzaji mmoja hapo juu alivosema wanauziwa na jeshi lenyewe[emoji23][emoji23] , hii nchi wakuu hakuna sehemu salama, kama ni reform inabidi ifanyike kubwa sana.
 
Inaendelea...
Kilichotokea ni kwamba wale maaskari walipofika kwa mzungu wakaona hapa kuna dili... Hivyo wakamtishatisha pale kwamba anapelekwa mahabusu kisha mahakamani
Mzungu akalainika akaomba yaishe palepale lakini wakamkazia kwamba hiyo ngoma ni mpaka mahakamani.. Pona yake amlipe yule mwananchi pesa yake na wao awape dola 2000 halafu watampeleka mpaka airport asepe

Mzungu akaona hii imekaa njema akatoa dola elfu tano sawa na around milion kumi akawapa.. Kwahiyo yule askari aliyeshuka chini kumwambia mwananchi aondoke alikuwa tayari ana pesa yake yote lakini hakumpa hata mia

Aliporudi juu wakamwambia kila kitu kiko sawa hivyo afungashe fasta.. Mzungu akiwa anajifungasha wale maaskari wakapiga simu airport na kufanya booking ya siku ile usiku kwa mtuhumiwa aliyetakiwa kuondoka nchini maramoja
Wakaondoka na mzungu mpaka terminal hotel wakampa chumba apumzike mpaka usiku na mizigo awaachie waitangulize airport na kama ana pesa zake azifiche vizuri kwenye begi kubwa

Mzungu akaingia kingi, akamaliza nao chao kilichobaki akasunda kwenye begi wakamuacha chumbani wakaondoka na mabegi yake!
Walipoondoka na mabegi walifungua na kuchukua pesa yote usd 55,000, na usiku ulipofika wakampakia kwenye ndege akaondoka bila kujua keshapigwa!

Kesho yake yule mwananchi anafika polisi Oysterbay anaambiwa mtuhumiwa wake katoroka na wanamtafuta!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafuta ya taasisi nani anayaminya?

Yaani usafirishaje mfungwa Kwa pesa Yako ya mfukoni?
Mafuta yanakuja kwa bajeti ,ishu pesa serikali ni kuwa na mlolongo mrefu katika kuclaim ndio tatizo...
Chukulia mfano kuna watu hapo Tamisemi wanadai pesa zao za kuanza kazi ni zaidi ya miezi bila bila ila baadhi wameshapewa.


Hiyo kusafirisha ni nadra sana kuwa na emergency ila nyingi ni scheduled ambayo ishatambulika kweny bajeti mapema na kama pesa washapewa ...Uhuni ni wizarani wakishirikiana na wakuu baadhi,kwa nn wengine wapate na wangine wasipate!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…