Kama unasema USA Ngoja nikueleweshe Kidogo.
Marekani aliingia Afghanistan mwaka 2001 na kuisambaratisha Serikali iliyokuwa Chini ya Taliban. Taliban wote wakaelekea Msituni. Mimi kwangu huo nauita Ushindi wa Marekani Kijeshi nchini Afghanistan.
Mwaka 2021,Marekani ikaweka mkataba na Taliban wa Marekani kuondoa Majeshi yake Mara ifikapo tarehe 31 Agosti. Marekani ilifikia uamuzi huu baada ya Mashirika ya kimataifa Mara kwa Mara kukosoa Operation za Marekani nchini Afghanistan kwamba zinaua Raia wa nchi hiyo. Pia Taliban walikuwa wanajilipua Sokoni na Misikitini na kuua Raia wengi wa Afghanistan. Marekani ikapata shinikizo la kufanya Mazungumzo na Taliban ili waache kujilipua na kuacha Kuua Raia wa Afghanistan. Kuona hivyo,Marekani ikaona isiwe shida. Wakaiachia Jeshi la Serikali msala wa kupambana na Taliban. Baada ya kuondoka Majeshi ya Marekani,ndipo Taliban wakaipindua Serikali dhaifu ya Ashraf Ghan. Hapo Marekani ilishindwa Kisiasa nchini Afghanistan baada ya kushinda kijeshi mwaka 2001.
Kwa upande Mwingine,Urusi alishindwa vyote,Kijeshi na Kisiasa. Mjahideen walizitungua ndege Nyingi Sana za kijeshi za Urusi.