Inadaiwa FIFA imeifungia Yanga kusajili madirisha matatu kutokana na deni la Kocha Luc Aymael

Inadaiwa FIFA imeifungia Yanga kusajili madirisha matatu kutokana na deni la Kocha Luc Aymael

Ila viongozi wa Yanga bna.hili jambo lingetoke simba ungeona matusi kwa wachambuzi
 
Kwa mujibu wa @FARPostZA, FIFA imeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji kwa madirisha matatu (3) mfululizo baada ya kushindwa kumlipa fidia ya kuvunja mkataba aliyewahi kuwa Kocha wao Luc Aymael.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji ambaye pia amewahi kuzifundisha Free State Stars na Polokwane City za Afrika Kusini, Oktoba 2022 alishinda kesi ya kuvunjiwa mkataba na Yanga bila kufuata utaratibu.

Klabu ya Yanga ilipewa maelekezo ya kumlipa Kocha huyo jumla ya dola za Marekani 152,000 kufuatia kumfuta kazi pasipo kufuata taratibu miaka miwili iliyopita.

Baadae klabu ya Yanga ilipanga kulipa kiasi hicho kwa awamu tano (5) ambapo awamu ya kwanza alipaswa kuwa Oktoba 2022.

Kwa mujibu wa FARPost, Yanga ililipa deni hilo kwa awamu mbili, Oktoba na Novemba 2022.

Kwa maana hiyo, Yanga bado wanadaiwa na Eymael dola za Marekani 99,000 pamoja na ada ya adhabu ambayo ni dola za Marekani 5,000.
Hizi ndizo habari napenda kusikia
 
Hizi ndio mada zinazo wapa faraja mambo mengine yasha kua magumu
Yaani wakipata taarifa za aina hii, shida zao zote zinakwisha! Hata wasipochukua ubingwa wowote ule ndani msimu wa Ligi, wenyewe huwa hata hawajali.

Maana wameshapata tayari kitu cha kupoozea maumivu yao. Aisee Rage apewe ulinzi maalum.
 
Back
Top Bottom