Inadaiwa FIFA imeifungia Yanga kusajili madirisha matatu kutokana na deni la Kocha Luc Aymael

Inadaiwa FIFA imeifungia Yanga kusajili madirisha matatu kutokana na deni la Kocha Luc Aymael

Kwa mujibu wa @FARPostZA, FIFA imeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji kwa madirisha matatu (3) mfululizo baada ya kushindwa kumlipa fidia ya kuvunja mkataba aliyewahi kuwa Kocha wao Luc Aymael.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji ambaye pia amewahi kuzifundisha Free State Stars na Polokwane City za Afrika Kusini, Oktoba 2022 alishinda kesi ya kuvunjiwa mkataba na Yanga bila kufuata utaratibu.

Klabu ya Yanga ilipewa maelekezo ya kumlipa Kocha huyo jumla ya dola za Marekani 152,000 kufuatia kumfuta kazi pasipo kufuata taratibu miaka miwili iliyopita.

Baadae klabu ya Yanga ilipanga kulipa kiasi hicho kwa awamu tano (5) ambapo awamu ya kwanza alipaswa kuwa Oktoba 2022.

Kwa mujibu wa FARPost, Yanga ililipa deni hilo kwa awamu mbili, Oktoba na Novemba 2022.

Kwa maana hiyo, Yanga bado wanadaiwa na Eymael dola za Marekani 99,000 pamoja na ada ya adhabu ambayo ni dola za Marekani 5,000.

Watatoa tamko wenye timu yao huenda wote tukabaki kulalamikia tetesi zinapoteza muda
 
Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeifungia Klabu ya Yanga Kutosajili kwa Madirisha matatu yajayo kwa Kosa la Kutomlipa aliyekuwa Kocha Mkuu wao Luc Eymael Raia wa Ubelgiji.

Chanzo Taarifa: Shaffih Dauda

Na hivi Aziz K hivi sasa ni tia maji tia maji, huku Dumbia nae akiwa haeleweki kwa Kupigwa Miba na Nondo Namba hapati na Morisson nae amechagua Kushinda Juliana Pub Mbezi Beach badala ya Kucheza Mpira halafu Wachezaji wengi wakiwa Wameshanoki / Wameshachoka kuna Watu kwa Rungu hili la FIFA wanaweza kuweka Rekodi ya Kufungwa sana na Kufanya vibaya mno kwa Msimu ujao.

Na nawakumbusha tu kuwa huyu Kocha Luc Eymael anayewadai Yanga SC Pesa zake ndiyo yule yule aliyewatukana / aliyewaita wana Yanga SC wote kuwa ni Mbwa, Nyani na Some.

Kudadadeki imeisha hiyo Mkome!!!!
Kombe lenu jingine hili
 
Madirisha matatu maana yake ni msimu mmoja na nusu, sio mbaya sana wasikate tamaa.
 
Yaani awaite utopolo manyani mambwa mnabweka bweka hovyo na bado anawadai pesa mkilipa kweli nyie mambwa
 
Mnashangilia kwamba mtapata ahueni, yaani mpaka Yanga afungiwe ndio mnaweza ku battle nae
 
Ndiyo Pesa Ngapi Kwa Cash Ya Bongo Hiyo
Utakuta Utopolo Wenyewe Walikuwa Wanasema Deni Ni Himilivu
Kumbe Ndiyo Wanaharibu Kabisa
 
Hapo sidhani kama ni Sheria...ni suala la uwezo wa kulipa madeni ni mdogo...kule Uturuki sijui zile milioni 400 walishalipa!?
Yanga sijui kwenye mambo ya kisheria huwa wanakwama wapi
 
Hapo sidhani kama ni Sheria...ni suala la uwezo wa kulipa madeni ni mdogo...kule Uturuki sijui zile milioni 400 walishalipa!?
Yanga inawaumiza sana vichwa , hii miaka 10 itakua migumu sana kwenu
 
Back
Top Bottom