SI KWELI PreGE2025 Inadaiwa kuwa Mdude kapatikana nyumbani kwa Lema Arusha

SI KWELI PreGE2025 Inadaiwa kuwa Mdude kapatikana nyumbani kwa Lema Arusha

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
1746613972738.jpeg
 
Tunachokijua
Mdude Nyagali, kada wa Chadema na Mwanaharakati mwili wake ulichukuliwa na watu ambao hadi sasa hawajajulikana mara baada ya kushambuliwa sana, ingawa hapo awali taarifa zilieleza kuwa waliomfuata nyumbani kwake walijitambulisha kama polisi May 2, 2025.

Jeshi la polisi katika taarifa zake wameelza kuwa wanaendelea na jitihada za uchunguzi, wakati wakazi, wanachama na baadhi ya viongozi wa Chadema mkoa wa Mbeya wameendelea kumtafuta mdude katika maeneo mbalimbali katika jiji hilo.

Madai

Kumekuwapo na grafiki inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye nembo ya Jambo Tv ikiwa na ujumbe kuwa "Mdude akutwa Arusha Nyumbani kwa Lema". Aidha grafiki hiyo pia inaonesha screenshot inayodaiwa kuwa ni ya John Mrema akieleza kuhusu namna tukio hilo lilivyotekea.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa grafiki hiyo haijachapaishwa na Jambo Tv kama ilivyodaiwa.

Ufuatiliaji umebaini kuwa Jambo Tv hawakuchapisha grafiki wala kutoa taarifa yenye kufanana na hiyo katika kurasa zao rasmi.

Ufuatiliaji zaidi umebainisha pia kuwa inayoonekana kuwa ni screenshot ya John Mrema akilezea tukio la Kupatikana kwa Mdude Nyagali kwenye makazi ya Godbless Lema ni ya kugushi kwani haikuchapishwa na Mrema.

Jambo TV kupitia ukurasa kurasa zao wamekanusha kuhusika na grafiki hiyo na wamelaani matumizi ya chapa yao kwa kile kinachoonekana ni kwa maslahi binafsi ya watu wachache walioamua kufanya upotoshaji huo.

John Mrema pia kupitia ukurasa wake wa X amechapisha taarifa kukanusha kuhusika kwa kile kinachoonekana kuwa ni screenshot kutoka kwenye ukurasa wake wa X.

Godbless Lema amechapisha grafiki hiyo na kuonesha kusikitishwa kwake kwa taarifa hiyo huku akieleza kuwa hata wakiweza kutupa maiti yake (Mdude) nyumbani kwake atashukuru sana.
tunashukuru kwa taarifa inaonyesha na kudhibitisha wahusika halisi...tyunamtaka aliyetengeneza hio grafit mbona ni rahisi sana
 
Back
Top Bottom