Kama raslimali siyo mali, basi nchi kama Botswana isingeendelea! Una mawazo mafinyu sana, na unashindwa kuangalia dunia inakwendaje iwapo reference yako yote ni kwenye ujenzi wa Tazara.
Rasilimali inakuwa mali au utajiri halisi (
disposable wealth) pale unapoigeuza kuwa mtiririko wa pesa taslimu (
liquid asset) ambao ndio huingia moja kwa moja kwenye matumizi. Ndivyo Botswana walivyofanikiwa kutajirika kupitia rasilimali zao za madini na wanyama. Kwa usimamizi makini na wa hali ya juu kweli kweli.
Sasa njoo hapa Tanzania. Tunajivunia madini yaliyoko ardhini na baharini. Mapori, misitu na wanyama. Vitu ambavyo tumeshindwa kabisa kuvigeuza kuwa utajiri halisi na kuutumia kujiletea maendeleo. Sababu? Uelewa mdogo wa wananchi, serikali ya kifisadi, mitaji haba. Matokeo? Hujuma na ufisadi mkubwa wa hizo rasilimali ghafi kwa kushirikiana na wawekezaji mafisadi. Wizi uliokithiri. Kudidimia kwa sekta binafsi nchini. Kufa kwa sekta ya uzalishaji wa msingi (primary industry). Mapato haba serikalini.
Kifupi rasilimali za Tanzania zimebakia jina tu kama za DRC, Angola, n.k. Hazina mchango wa maana kwenye uchumi. Zinatajirisha wawekezaji mafisadi wa nje, makampuni yanayoiuzia serikali mitambo na vifaa vya kiteknolojia (ndege, mitambo, magari etc.) na mafisadi wa ndani.
Sasa anapotokea mtu na kudai nchi hii ni tajiri sana. Ina rasilimali nyingi sana. HIVYO tutatumia hela za ndani kutekeleza miradi ya matrilioni ya shilingi kwa mkupuo, ni jambo la kushangaza sana. Ni aina ya utapeli wa fahamu za umma. Hizo hela hazipo. Hiyo dhana ya fedha za ndani
is just an illusion (Imagination).
Sasa kwa nchi ambayo miaka yote bajeti ya serikali hutegemea wafadhili kwa zaidi ya 80%. Ambayo hata matumizi ya kawaida ya serikali yanasuasua kwa kutegemea makusanyo ya ndani - hayatoshi. Halafu ghafla muanzishe miradi ya matrilioni kwa mpigo - kwa ndoto ya “rasilimali”, huku utamaduni wa ufisadi ukiendelea, lazima uchumi uyumbe sana. Ndio maana awamu hii inakopa kweli kweli
with no end in sight! Na hazitoshi wala hazitatosha.