Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,430
- 11,813
Ahhahahhah eti suala la gwajima.
Mimi simung'unyi maneno mkuu naongea kilicho moyoni mwangu.
Sina huzuni wala furaha nipo kama zamani.
Huzuni niliyoipta kwa kuona matusi ya mshikaji akiwatukana wahusika basi ndio huzuni hiyo hiyo ambayk niliipata kuskia jamaa katekwa.
Sijaona kwamba kafanyiwa kubwa mnooo ambalo linastahiki kupigiwa kelele wakati na yeyr alikuwa ni mtukanaji mkubwa tena matusi ambayo ukimuambia mtu haya anayetukanwa ni mkuu wa Nchi hawezi amini.
Wote ni wahalifu,waliyemteka ni mhalifu mwenzao.
Kama yeye alionyesha ubabe wa mitandao kwa kufanya uhalifu wa kutukana.
Basi nawatu wanaonyeaha ubabe wao kwa kumteka na kumtia adabu huko aliko.
Kama ambavyo hakukuwa na sababu ya yeye kutukana bali angeongea uhalisia tu.
Basi na hao watekaji nadhani hawana sababu ya kumteka huyo mtu wangesema wazi tatizo nini.
Wote kwangu wako level moja.
Kila mmoja amejaribu kuonesha umwamba wake ila huyu mmoja kaonyesha kwenye mtandao na mwingine kafanya vitendo.
Ni tuhuma hadi pale itakapothibitishwa mahakamani.
Hata mimi siwezi tetea mhalifu pale itakapothibitika mahakamani kuwa alifanya kosa.
Waungwana wanasemea sheria kuzingatiwa kwa mujibu wa katiba.
Je Abdul Nondo yeye alikosea nini kwa mfano?