Naelewa ndio maana nakupinga, ni kweli teknolojia imekuwa sana ila kufuta kumbukumbu fulani uache nyingine hiyo inawezekana kwenye movie tu, hata hiyo amerika waliopiga hatua kiteknolojia hawawezi kufanya hiyo jambo upo?
Katika mawazo yako ni sawa, kwa sababu hujui unachoongelea hapa.
Wewe kutojua haina maana wengine nao hawawezi kujua.
Kumbukumbu ni za aina mbalimbali, kuna kumbukumbu za mambo ya karibuni, na kuna kumbukumbu za mambo ya muda mrefu. Kuna watu wanapoteza kumbukumbu za aina mbalimbali kutokana na magonjwa yanayowapata akilini. Msingi wake hapa ni kwamba, katika ubongo kuna sehemu mbalimbali zinazohusika na kumbukumbu. Sehemu moja ikidhurika, inaathiri aina fulani ya kumbukumbu bila kuathiri aina zingine.
Maana yake hii ni kwamba ubongo unavyo vimelea(?),'receptors' mbalimbali zinazoweza kutumiwa kuziba eneo hilo la ubongo. Dawa zinaweza kufanya hivyo.
Ukishajua 'receptors' za kumbukumbu fulani zipo wapi, unaelekeza dawa katika eneo hilo kuziziba receptors za huko.
Sasa kama hujui 'receptors' za jambo fulani zipo wapi, obviously huwezi kujua namna ya kuziziba.
Pombe na dawa, inayofannya kazi kwenye ubongo, pamoja na kwamba haichambui eneo maalum sana, inaathiri hata za mambo mengine.
Dawa za kulevya ni hivyo hivyo.
Sasa mimi ninakwambia, badala ya kupeleka kiholela dawa zinazoathiri ubongo, kazi iliyopo sasa ni kuzichambua/kuchambua maeneo maalum ndani ya ubongo yanayohusika na jambo unalotaka kulififisha.
Hizi siyo 'movie' tena kama unavyofikiri wewe.
Na bado, mambo ndiyo yanazidi kunoga katika maeneo kama haya.
Bahati yetu iliyo mbaya, bado tunao viongozi wasiokuwa na maono ya kuwaelekeza vijana wetu wakachakarike katika mambo muhimu kama haya.