Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

GoPPiii.

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
1,792
Reaction score
3,075
Nimebahatika kuona vipindi kadhaa vya mchungaji Mwamposa.

Yawezekana ukimtoa Yesu (Kwenye ukristo) kiumbe mwenye kufanya miujiza mingi hapa duniani anaweza kuwa huyu Mchungaji.

Sitaki kuhukumu kama ni mkweli au Lah, ila kwa wanaoshuhudia kwenye vipindi vyake anaweza vunja rekodi.

Nadhani ile miujiza ya Yesu ya uponyaji huyu mchungaji ataivunja rekodi zake, isipokuwa Kulisha watu 5000 ambao walikula na kusaza na kufufuka kwa yesu.

Kuna yoyote amepatwa na muujiza wa Mwamposa haswa uponyaji humu?
 
Ufunuo wa Yohana 21:6
[6]Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

And he said unto me, It is done. I am Alpha and Omega, the beginning and the end. I will give unto him that is athirst of the fountain of the water of life freely.
 
Ufunuo wa Yohana 22:17
[17]Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
And the Spirit and the bride say, Come. And let him that heareth say, Come. And let him that is athirst come. And whosoever will, let him take the water of life freely.
 
1684680308286.png
 
Nadhani ile miujiza ya Yesu ya uponyaji huyu mchungaji ataivunja rekodi zake,isipokuwa Kulisha watu 5000 ambao walikula na kusaza,na kufufuka kwa yesu.
Rekodi ya Yesu mbona ilishavunjwa siku nyingi tu

Sio sababu watumishi wa sasa wako vizuri kuliko Yesu la .Ila Yesu Mwenyewe aliomba na kuwaombea watakaofuata baadaye wavunje hiyo rekodi kwa maombi yake

Enzi za Yesu alihubiria watu wachache tu kwa sauti yake tu sasa hivi spika zipo xaweza wafikia wengi kuliko mkutano wa Yesu pia kipindi cha Yesu aliweza wafikia tu waliohudhuria mkutano wake tena wa lugha yake tu bila mkalimani leo watu waweza hubiria dunia nzima mabilioni ya watu kupitia television, nk wa mataifa na lugha mbalimbali kupitia Television ,YouTube, nk kwa kutumia wakalimani nk

Kufanya wanaomwamini makubwa kuliko yeye ni majibu ya maombi aliyoomba sio sababu mtumishi yuko smart sana.Hata wewe waweza fanya makubwa kuliko Yesu

Yohana 14:12​

Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
 
Back
Top Bottom