Pre GE2025 Inahitaji akili kubwa kiasi gani kuelewa kwamba kwa kuwa Zanzibar wana serikali na Rais wao, Rais wa Tanzania, kimsingi, ni Rais wa bara?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Currently Bara kunaongozwa na Mtaalamu kutoka nje
Na huyo mtaalamu anataka kuendelea Tena Kwa miaka mitano, bado tunakodia macho na PhD zetu,ila hatuelewi,Wala hatutaki kuambiwa.
 
Point of correction:

1. Usiseme "Rais wa Tanzania Bara". Sema hivi; Rais wa JMT automatic huwa ndiye Rais wa Tanganyika...

2. Hatuna nchi inaitwa "Tanzania Bara". Tanzania ni matokeo ya muungano wa nchi huru mbili TANGANYIKA na ZANZIBAR. Na kwa hiyo ukweli ni kuwa ziko nchi mbili zilizoungana TANGANYIKA na ZANZIBAR. Hakuna nchi na haijawahi kuwepo nchi inayoitwa "TANZANIA BARA" hata kama kuna juhudi na ulaghai wa ki - CCM kujaribu kuipoteza na kuifuta TANGANYIKA. Wamefanikiwa kwa muda, lakini Tanganyika itarudi tena si muda mrefu...!!

3. Ukweli ni kuwa mpaka sasa Tanganyika tunatawaliwa na raia wa kigeni toka nchi iitwayo Zanzibar. Na inashangaza sana kuwa sisi Watanganyika tumeuukubali ujinga na uhayawani huu....

4. Kwa kufikiri kwa akili ya kawaida tu, mtu aweza kujiuliza, hivi inawezekanaje nchi mbili huru zilizoungana zikawa na mfumo wa utawala wa hovyo kiasi hiki?

5. Zanzibar wana Rais wao na mfumo wao wa kiutawala ambao hauruhusu Mtanganyika kushiriki shughuli za kiutawala huko. Lakini ajabu ni hii, kwamba, sisi Wa - Tanganyika tumeruhusu kirahisi tu raia wa nchi mshirika mwenzetu wa muungano (Zanzibar) wafanye chochote watakacho ktk nchi yetu, wachukue nafasi za uongozi wetu, ajira za watoto wetu na mpaka sasa raia wao mmoja amekuwa Rais wa nchi hii...!!

This is absolutely ridiculous...

Ni kama vile sisi Watanganyika hatuna akili vile, hatujitambui wala kujielewa...

Tukatae hili. Tuukatae ujinga na upuuzi huu wa siasa mufilisi na uchwara za Chama Cha Mapinduzi - CCM...
 
mimi naona kuwa suluhisho la kudumu ni kuvunja muungano. Kuna mambo mengi yanayoiathiri tanganyika yamepitishwa kwa kivuli cha muungano. Kuendelea kuungana ni sawa na kuendeleakukaa na mwiba unaokuchomachoma kwenye sofa lako.
 
Jina la 'bara' ni porojo za wanaoficha ficha suala la muungano lisihojiwe. Sema Tanganyika.
 
Unatoka nje ya mada. Elewa thene ya thread. Mlifauluje mitihani yetu, Faiza Foxy hywa anauliza
Natokaje nje ya mada kwamba rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni wa bara tu, kwa kukuletea vifungu vya kikatiba vinavyoainisha mambo ya muungano?

Unajua muungano una mambo yake maalum yanayoongozwa na serikali ya muungano Tanzania nzima?
 
Ndio maana wengine tunaona Samia kwa jinsi alivyoweza kua rais kutokana na katiba apishe kua mgombea wa ccm kwan pamoja na kwamba kama mtanzania anaweza kugombea lakini sio mtanzania mwenye uwezo na sifa. Asipogombea watanzania wenye sifa na uwezo watajitokeza bila kuwekewa mikwala na chawa wa Samia. Watanzania wanahitaji kiongozi aina ya Magufuli ambaye anaweza kulitoa taifa kwenye umaskini na kujenga utawala wa haki na usawa kiuchumi na kijamii. Samia baada ya kushika kiti cha urais wananchi walishuhudia akikejeri sera za kimagufuli hadi kudiriki kuwapa tena uongozi watu waliyomkejeri na kumdharau magufuli. Hakika wananchi wengi hawana imani na Samia. Huu ndio ukweli.
 
Natokaje nje ya mada kwamba rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni wa bara tu, kwa kukuletea vifungu vya kikatiba vinavyoainisha mambo ya muungano?

Unajua muungano una mambo yake maalum yanayoongozwa na serikali ya muungano Tanzania nzima?

Najua muungano una mambo yake maalum yanayoongozwa na serikali ya muungano Tanzania nzima, lakini kwa sasa majukumu hayo ni kidogo mno, kwa sababu ni kama 5% tu ya majukumu ya raisi. Kimsingi, raisi akiamua kutoyafanya, Zanzibar haitaathirika kwa sababu ya kuwa na serikali yake ambayo haitegemei serikali ya muungano kwa karibu 95%. Majukumu ya raisi wa muungano kwa karibu 95% yanahusu Tanzania bara.

Unaona Kiranga, katiba ya Tanzania haisemi kuwa raisi wa Tanzania atakuwa kutoka bara tu, lakini imebatilisha suala la kusema raisi wa Tanzania atachaguliwa kwa mtindo wa zamu kati ya Tanzania bara na visiwani kama ilivyokuwa mwanzoni. Ndio maana tukawa na Mkapa, then Kikwete then Magufuli. Haikuwa kwa kuwa Katiba ilisema raisi atoke bara tu.

Sasa ilikuwa iendelee hivyo na isingekuwa rahisi mtu wa Tanzania visiwani awe ndio mgombea uraisi wa Tanzania. Mojawapo ya sababu ni kwamba ilijionyesha wazi raisi wa Tanzania majukumu yake yako zaidi bara kwa sababu Tanzania visiwani wana serikali yao na hawaingiliwi kwa namna yeyote na raisi wa Tanzania. Kimsingi basi, bila kuliweka kwenye maandishi au Katiba, raisi wa Tanzania siku zote angetoka bara na makamu wake kutoka visiwani. Kilichobadilisha hilo ni kifo cha Magufuli, ambapo automatically tukawa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar, jambo ambalo halikutarajiwa. Na hilo halipingani na katiba.

Sasa lengo la thread hii, na nitasema kiingereza kwa msisitizo, ni kuonyesha kwamba under the current set up of the union between Tanzania mainland and Zanzibar, it is constitutionally correct the president of Tanzania is from Zanzibar, but it is constitutionally inappropriate. And because it is constitutionally inappropriate, it creates an urgent need for us to correct the constitution. That is why I said, in the meantime, president Samia can offer not to contest for the presidency in the next general election, out of her own free will, because as long as the constitution allows it, it is within her rights to contest for the presidency

To illustrate, today, some politically foolish members of parliament, because of their majority in the parliament, could decide to change the constitution such that someone from Kenya, for example, can become the president of Tanzania. Once you have changed the constitution to allow for that, it will be constitutionally correct for a Kenyan to become president of Tanzania. But will it be constitutionally appropriate?
 
Kwanza hakuna kitu kinaitwa Tanganyika au Tanzania bara.
Muunganiko wa Zanzibar na Tanganyika uliiua mazima Tanganyika wakati huo Zanzibar ikibakia kuwa nchi huru!
Yaani kifupi ni muunganiko ambao haupo kwenye mantiki wala kwenye mahesabu!
Hauna win-win arrangements!

Soma hapa kwanza:
The 'United Kingdom' refers to a political union between England, Wales, Scotland, and Northern Ireland. Although the UK is a fully independent sovereign state, the four nations that make it up are also countries in their own right and have a certain extent of autonomy.https: (Is the UK a country?)
 
Umepata vipi figure ya 5% ?
 
Umepata vipi figure ya 5% ?
Expert opinion! Lakini unaweza kukadiria kutokana na shughuli za Muungano chini ya raisi, kama jeshi, mambo ya nje. Nini kingine? Sasa ndio unasema hayo yanachukua asilimia ngapi ya shughuli za raisi za kila siku, na kiasi gani yanaathiri Zanzibar?
 
Ndio maana watu wanadai serikali ya Tanganyika.
 
Expert opinion! Lakini unaweza kukadiria kutokana na shughuli za Muungano chini ya raisi, kama jeshi, mambo ya nje. Nini kingine? Sasa ndio unasema hayo yanachukua asilimia ngapi ya shughuli za raisi za kila siku, na kiasi gani yanaathiri Zanzibar?

So, the 5% is made up, like your assumption that the union president is only a bara president.

The union president appoints Zanzibaris to the union cabinet, at will. She just appointed Mahmoud Kombo to be MP and Foreign Minister. How can she be only a bara president?

Ina maana nilivyokuwekea mambo ya muungano hujayasoma kabisa au unayadharau tu kwa sababu yanaharibu hoja yako ya kutunga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…