Inakera kuona msanii mmoja tu ndo anapaparukiwa na makampuni

Status
Not open for further replies.
Sister uwezo alionao diamond kajengewa na nani???
Au vodacom wamemjengea?
My dear kuna watu wanasaidiwa kufika mahali gulani na wengine wanajisaidia wenyewe kufika mahali fulani.. . .. ..na ukumbuke muda mwingine unamsaidia mtu na kumjenga...... Na hata hapo diamond alipofika si kwa juhudi zake peke..... Inawezrkana kuna wengi wamemsaidia kwa namna moja au nyingine.

Tuache hizo lazma ufike mahali fulani tuwe multipurpose.
 
...kuna wasanii wakali na wenye fan base kubwa kuzidi hata huyo Diamond, kwa mfano King Kiba ndio msanii mwenye fan base kubwa hapa bongo. Ina maana makampuni hayamuoni au figisufigisu....
Isho_boy bhana, huyo Kiba mwenyewe hata kuandika caption anajionea taabu ndo mtu ampe u- brand ambassador!!

Halafu hivi una habari cku hizi marketing imehamia kwenye social media ambako huyo Kiba si tu kwamba hata mambo ya kuandika caption anajionea taabu lakini kutokana na mapozi yake, watu kibao wana followers wengi zaidi yake wakati ktk hali ya kawaida ilitakiwa awe amekaliana kooni na Diamond lakini matokeo yake anakaliana kooni na kina Rose Ndauka!

Halafu ngoja nikujuze kitu kidogo. Kiba haja - follow mtu Instagram. Usually haandiki caption. Kibiashara hayo mambo mawili yanatoa picha kwamba ana poor social interaction kwahiyo ni ngumu sana mtu kumpa u - ambassador msanii anayeonesha ana poor social interaction!

Kama ushawahi kuhudhuria interviews na unafahamu jinsi ya kujibu maswali ya "what are your extracurricular activities au hobby zako ni zipi basi bila shaka utanielewa namaanisha nini hapo kwenye social interaction.
 
Diamond ni mchapakazi sana, ni mtafutaji hachoki na huo uwezo kajijengea..... Ni kweli kuna watu waliomfikisha hapo ila juhudi binafsi zinachangia
Lakini huwezi sema hayo makampuni ndo yamemuandaa kuwa hivo alivo yamempa kazi baada ya kuwa hapo alipo, hivi hivo kiba afight makampuni yamuone
 
Sister, yaani unatarajia kampuni za kibiashara zifanye favor za kumwinua mtu? Wao shida yao ni mtu ambae tayari yeye mwenyewe ni brand na kama Tanzania hakuna mtu mwenye hizo sifa watatumia hata celebrities wa nje!
 
Ndiyo maana hatufanikiwi mana hatutaki kuwa source ya mafanikio ya fulani. Mpe mtu nafasi...mjenge afu useme hana uwezo. Wenzetu wanaendelea sababu wanakuza watu.......sidhani kama kuna wasanii hawana juhudi binafsi....kama AY .......tukubali tukatae sisi bado sana.....tukimng'ang'ania mmoja ni huyohuyo... Wakati ukute kuna watu wengine wanaweza kufanya kama yule ama zaidi ya yule. .......
 
Sister, yaani unatarajia kampuni za kibiashara zifanye favor za kumwinua mtu? Wao shida yao ni mtu ambae tayari yeye mwenyewe ni brand na kama Tanzania hakuna mtu mwenye hizo sifa watatumia hata celebrities wa nje!
Kwahiyo celebrate ni diamond tu? AY na wengineo sio?
 
Lynne, sio kwamba ni anti-social fulani bali ni totally anti-social!

Instagram haja - follow mtu hata mmoja. Majority ya posts zake haandiki hata caption. Hizo sababu mbili peke yake zinatoa reflection kwamba the guy is anti-social. Zile caption zina - reflect uwezo wa mtu ku- interact na followers! No caption means you don't communicate! Sasa ni vp umpe u-brand ambassador mtu ambae ha-communicate!!
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] bila kusahau interviews zake zinaboa.
 
Mama vodacom wanahitaji pesa kuinua mtu sio kazi yao, hata akiwa sio diamond, siku bambo akiwa star mwenye level zake vodacom wanaweza kumtumia ila kamwe hawawezi kuanza kumuandaa bambo leo awe brand ndo aitangaze voda UNACHOKIWAZA HAKIWEZEKANI MPENZI
 
Hadi hapa team kiba wanaweza jua kwanini kiba abaki porini kutulindia wanyama wetu dhidi ya majangili
 
Basi tunashida sana....kama tunamtegemea mtu mmoja kwenye kutangaza biashara. Sasa hawa wengine utawanyanyuaje? Bora wangeangaliwa top 3 ya wasanii wenye mashabiki wengi.
Unaonaje ukianzisha kampuni yako ukachukua hao top 3...usilazimishe kisichowezekana kwenye biashara nani alikuambia kuna top 3...? Biashara inaangalia nani atakupa faida kubwa zaidi kushinda wote na makampuni yamemwona diamond
 
Diamond ndo msanii anae wainspire wasanii wote wa bongo fleva ukiacha wakongwe alianza kutengeneza video za bei kali ile namba one alisema ametumia mil.26 wasanii wenzake walimcheka na kusema ana penda sifa lakini leo hao hao wanatoa mamilioni kushoot videos wakati mwenzao yupo mbali.
Diamond alienda nigeria kutafuta network akazamia hadi harusi ya Psquare hadi humu JF zikaanzishwa thread jamaa anajipendekeza wakati hawamjui wenzake wakawa wanamcheka dogo akapata network akatoboa nigeria, wenzakr leo wamegeuza maneno anawabania network, wanaangaika na collabo za nje mwenzao yuko mbali anapiga show zinazoeleweka nje.
Diamond ameanzisha lebo yake anasimamia wasanii wake tayari ni big bland. Anaelekea kuwa don jazzy wa bongo.
Hawa wasanii wengine mpaka wafike alipo diamond watasubiri sana maana sio wabunifu na waoga.
Sasahivi diamond hata akishoot video ya mil 60 akifanya show yake moja tayari pesa imerudi hawa wengine wanapata hasara wanafanya video za gharama show zao bei chee

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo maana hatufanikiwi mana hatutaki kuwa source ya mafanikio ya fulani. Mpe mtu nafasi...mjenge afu useme hana uwezo. Wenzetu wanaendelea sababu wanakuza watu.......sidhani kama kuna wasanii hawana juhudi binafsi...
Hakuna kitu kama hicho kwenye biashara. Labda niseme hivi. Kinachowavutia kwa Diamond sio mituzo mingi aliyonayo bali alivyoji-brand mwenyewe as real super star! But look... pamoja na u-superstar wake huo bado ni mtu anaye - interact sana, tena sana na fans wake kwenye social media. Hayo mambo mawili ndiyo wanayataka kampuni ktk kutangaza bidhaa zao. Na hayo mambo huitaji Vodacom au Coca-Cola kuku-empower bali ni msanii mwenye! Btw, sio jukumu lao!

Chukulia mfano wa Le Mutuz! Watu wanamkejeli kila leo lakini deal za matangazo anazipata sana hata kama co za makampuni makubwa. Why anapata? Coz' the guy knows how to interact with online community... that's it-- ndicho kampuni kinatafuta and you don't need to be empowered!
 



Ukitaka kujua madudu ya Domo tizama sura ya Mama yake tu, yule Mama anaruka na sahani usiku, si Muha yule. Wewe jiulize, Domo ana muziki gani wa kuwazidi vijana kama Barnaba, Amini, kina Aslay na wengineo? Ndiyo maana watu wanasema chini chini kuwa Domo anamezeshwa kizizi na Mamaye.
 
Unaonaje ukianzisha kampuni yako ukachukua hao top 3...usilazimishe kisichowezekana kwenye biashara nani alikuambia kuna top 3...? Biashara inaangalia nani atakupa faida kubwa zaidi kushinda wote na makampuni yamemwona diamond
Inawezekana sana kama mkishirikisha akili zenu kwa ufasaha.......tatizo ubongo ume stuck kwa jina moja tu diamond........ .
 
Makampuni hayana kazi ya kumnyanyua mtu...makampuni yana angalia nani atatupa pesa zaidi
 
Kitu ambacho sitaki kuamini ni kwamba wasanii wengine hawayafanyi kama anayoyafanya diamond...... Kama hilo swala uliloliyolea mfano. Ni kweli wengine hawafanyi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…