Inakuaje maofisini huku msomi ana Masters ila hajui kuandikia mradi

Hahahaha upate ufadhili wa billion 100 sio mchezo unajua. Ni ishu nzito sana ila mpunga ukitoka ni kujipigia tu.
B 100 huko sio mchezo ila me naisemea tu ile ya million 200-300..
Unahakikisha kweli awamu ya kwanza wadau unawakazia wawe serious na mpango kazi wao ama katiba yao ili matokeo yatokee yaonekane wasiingie tamaa. Kikubwa ni ushirikishwaji partner wote na hasa viongozi wa maeneo husika ukandaa training za kutosha.. Wazungu wanapenda sana mradi uweze kuacha awareness zaidi. Mission ikiwa accomplished nyie kupewa hela za awamu ya pili ni rahisi vielelezo vikiwa vipo mfano hata wakikagua wakakuta vifaa ulivyotaka vipo na matokeo yapo hela ni nyingi tu labda changamoto zipogi kwenye mawizara huko wakatae kulipitisha andiko nako sio rahisi kama mradi una Make sense na mnagawana cake vizuri na wanaserikali wenzako na private sectors.
 
Hii nzuri naona sheta amepitia njia hii na kashtoboa freshi.
 
Uandishi wa Habari na proposal ya mradi unalinganisha yaani mtalaam Kwa mfano wa metereology unataka ulinganishe andiko lake na mwandishi wa Habari.
Ndugu wewe mgeni wa nchi hii na ma-masters' holders?!
Kwa kifupi wenye masters stahiki sijui kama wanafika asilimia thelathini.
Karibu asilimia sabini wana 'janja janja masters', masters za magumashi, masters za rushwa!
Watapata wapi huo uwezo wa kuandaa andiko la mradi husika kwa ufasaha?
 
Na byie mliopo kwenye ofis za umma tena mujitqhid sana .mkuu wa taasis akae chin aandike mirad mana ni Phd sio kutwa kuwasha gari kulalaallia barabaran,mana gari inakua mpaka na mswaki kwa safari,tuna mashirikiano na nchi zote duniani ni kias cha kuandika tu,wale us embasy wanatoaga mpaka na theme na format na area of study uliza sasa nan kaandika,
 
Huyo atakuwa na shida zake, or angalia masters ya kitu gani. Angeomba msaada. Sio mastars wote hawawez omba hela za mradi, wapo majembe hadi diploma yanaandika mkeka unaeleweka. Na ni suala lanuzoefu, huko alipotoka alikuwa ana andika au ana andikiwa?
 
Kama utafuatilia sana kazini watu wengi wanachoka wakifanya kazi kuanzia miaka 5 na kundelea , hapo wanaanza kutafuta vyeti vya masters na kuendelea ili wapate vyeo na pesa rahisi.

Ofisi nyingi sana bado senior na managers wanasumbua subordinates kuwaandalia mambo yao kibao , kiufupi wanakosa exposure kazi inabaki kugombania safari...Ukiona taasisi kubwa haina maslahi basi tambua uongozi wa hapo ni ovyo kabisa.

Katika kila mwaka wa fedha kama hivi kuelekea mwezi wa sabab, basi taasisi zinaandaa report zao kama proposal katika operations zao pamoja na kuomba pesa. wengi kati ya zile Taasisi za ovyo wanashindwa kabisa kupeleka ripot mwishoe wanabaki duni.

Zipo Taasisi wanaomba posho za field watu kwa wafanyakazi wao wanaenda mpaka nje na kuandika ripot binafsi , nyongeza za per diem na posho mbalimbali, hata kuendesha mifumo binafsi ya ulipaji ndani ya Taasisi achana na hawa wanaoutumia check number wamejishindwa kabisa kuanzia uongozi...Uelewa wa kufanya mambo ndio unaona baadhi ya Taasisi hazina watu makini wa kubuni uendeshaji na maslahi.

Zipo Taasisi hapa bongo zimeomba pesa za kufundisha watu mifumo ya AI , tena wana hoja za maana ila nyingine mpaka sasa hata e-office hamna . Tatizo la kukosa exposure ni baya sana watu wanapenda pesa rahisi bila ya kuhangaisha akili.​
 
Wakuu hao ni watu wa siasa . Yye akishapata per diem na safari za uhakika basi hana mpango wa kuandika miradi ya maana.
 

SASA SI UNGEMWAMBIA HUKO OFISINI? AU UNAAMINI ANA ID HUKU? MKIZIMANA PESA HUKO MNAKUJA KUCHAMBANA JF. BURE KABISA NINYI MADOGO.
 
wakenya elimu yao ipo juu by far kulinganisha na sisi. Ni vigumu kwa mtanzania kushindana na mkenya kiweledi ndio maana kwenye ajira za kimataifa wanatuacha. sisi level zetu ni Malawi, Comoro, Msumbiji, Burundi na somalia
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Jololo muongo muongo sana humu namfaham kwao mtwara pale nalindele. Msimsikilize sana ila mradi kuandika sio poa! Ujipange hasa
 
Achana na li mradi lote, we mwambie mtu yupo taasisi nyeti aandike "Concept note" yaani aweke tuu wazo la mradi kwenye maandishi. Utaona anavyohangaika. Tuna safari ndefu sana hii nchi. 😁
Kinachosumbua kwenye conceptional ni uniqueness/modus operandi. Mana hatujitaji tena kuwa na mawazo yaleyale.. miradi ya matengezo, ya biashara au social initiatives yanahitaji vichwa vya aina tofautitofauti.

Mtoa mada naye hili sijui kama analijua au la
 
Uandishi wa miradi hauathiri chochote utekelezaji wake. Mana kama ilimake sense mpaka pesa ikatoka ujue tayari mradi ulikuwa tentative.. kufeli kwa mradi kunawez kuchagizwa na quality ya wafanyakazi. Mana hiyo ni case nyingine serious kwenye ufanikishaji
 
Oya uyo msomi kwan yupo umu??
 
Mnasemea kule jalalani Kwa Paramagagagagaga.......m.............b......a sina Budi.

Vyuo vyetu hakuna kitu.
Ukiwa na hela yako unatoka na cheti kizuriiiiiiiiiii.
Mademu,ukiwa mkali unatoka na cheti kizuriiiiii bila hata kujisomea.




Ila ni Tz pekee,elimu inayopimwa kwenye kalatasi na sio kichwani.


Msukuma Kasheku ana akili zaidi ya wasomi wetu PhD holders 90 wa tzs🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wasomi wa Tanzania ni wa vyeti Sio utendaji
 
DU? Hao ndio wanatuharibia jina na kufanya tuchunguzwe sana kabla ya kufadhiliwa miradi....
Mradi unatakiwa ufanyike kwa ufanisi wa 90 to 98%; ukitaka kula hela; andika mradi kwa gharama za Ulaya halafu utekeleze kwa gharama za kitanzania ili hela Ibaki nyingi ....hao wanao kwenda kufanya vikao Malta sijui Dubai.....eti ili hela iishe sikubaliani nao kabisa kwani wafadhili wakiwa makini wanaona ni ubadhirifu wa hela za mradi.
Fanya study tour za kueleweka sio unatoka nchi masikini unaenda kulala 5star hotel wakati wafadhili wenyewe wanalala 3star hotel

Wangejustify kwa kuwa na timu kubwa ya watu wa kusaidia nk nk nk
Natamani sana watu wapate hela ila natamani pia watu watekeleze walicho ombea fedha na sio kuandika miradi ya kitapeli.....
 
We unasema AI ilhali mtu hata laptop hana,alipo hapo ana top up ,ukicheki posho kwa mbinde zote anakaba mkurugenzi anasafir peke yake,na cycle yake anayoitaka,sasa ubunifu utoke wap ikiwa mpaka sasa hiv kuna sehem wanahaingaika kufundishq mifumo hatarishi ili mrad wavipanguse vifungu ,siwez kuwa na idea ilihali nimechoka sana mpaka nikutanishe mwez kipengele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…