Inakuaje maofisini huku msomi ana Masters ila hajui kuandikia mradi

Inakuaje maofisini huku msomi ana Masters ila hajui kuandikia mradi

We unasema AI ilhali mtu hata laptop hana,alipo hapo ana top up ,ukicheki posho kwa mbinde zote anakaba mkurugenzi anasafir peke yake,na cycle yake anayoitaka,sasa ubunifu utoke wap ikiwa mpaka sasa hiv kuna sehem wanahaingaika kufundishq mifumo hatarishi ili mrad wavipanguse vifungu ,siwez kuwa na idea ilihali nimechoka sana mpaka nikutanishe mwez kipengele
Akirudi ripot anawapa muandae yaani watu wanapenda pesa rahisi, nimefanya kazi Taasisi yaani management wanashindwa kuandika proposal ya kuomba pesa ya overtime .
 
Inashangaza unakuta mfanyakazi mwenzako kasoma Sawa ana master ila kuandika kuomba hela za miradi Kwa ma donors wetu hawezi sijui niseme hana idea wakati kila kitu kipo Google ni yeye kusuka tu wazo la hela ya kawaida wazungu Wana hela kibao hakuna PA kuzipeleka ziko hewani.

Mtu kijana under 40 msomi wa level ya master unabaki kugombania hela za per diem za ndani nako ni pesa madafu tu nini tofauti yako na uliowazidi shule?

Wewe ulipaswa uwe unaandika lipitishwe bora likataliwe ila upewe sababu utarekebishwa andika andika andika tena lazima ipo siku litatiki uka coordinate Michongo. Hela za mabadiliko ya tabia ya nchi zipo kama zote mamifuko yanatoa.

Mavyeti kibao unabaki kutumia Google ku watch nonsense everyday.
Mkuu unashangaa hilo. Mwezi mmoja uliopita nilikuwa pale costech kuna mwajiriwa hajui kuhamisha vitu from email to flash na wakati kaajrii kitengo cha data.
Nilibaki nashangaa
 
Uandishi wa miradi hauathiri chochote utekelezaji wake. Mana kama ilimake sense mpaka pesa ikatoka ujue tayari mradi ulikuwa tentative.. kufeli kwa mradi kunawez kuchagizwa na quality ya wafanyakazi. Mana hiyo ni case nyingine serious kwenye ufanikishaji

Mradi unaweza kuwa tentative kwa Donor na akaubali na bado ukaja kubuma kwa maana hautekelezeki, haupimiki kimatokeo mkuu. Kuna miradi mingi donors huwa wanaikatisha katikati au mnatekeleza awamu, mnaandika report na pesa haitoki tena na mnaambiwa wazi.

Mfano mzuri ni REA Mradi wao wa Nishati mbadala kutumia umeme wa Jua kutengeneza Min Grids za umeme kwa vijiji vilivyo visiwani ambavyo havifikiwi kimiundombinu, Ulikuwa Funded na European Union. Mwisho wa siku ulikuwa na uhalisia lakini haukutekelezeka na fedha za awamu zilitumika.
 
Kugombea vi per diem vya safar za uongo na kweli imekua ugonjwa.mtu anaandika phd kabisa anaskikizia dojezo litiki avute perdiem,unakuta mtu phd mzima badala ya kufo cus vip aandike maandiko kama yote magrant yamejaa huko yeye kutwa kusafiri,sehem za kuachia tu subordinate wako waende wakupe taarifa hapana yeye kutwa kucha barabaran anaubgqnisha vikao tu,unakuta katoka cha Morogoro kashajopigia pande juu kwa juu huyooo arusha,hajakaa sawa dar kikao hajapumua mwanza,hajaila posho ya moro mara dodom .

Nimewah kuuona phd kaja kukagua kaz yan hana point anabubuja tu,bora ma instructor sa Vyuo wale wanapambana,nenda pale dodma au UD wanapata sana grants za research ila maofisin asee msiba, unapokuwa mfano ni kiongzoi lets say shirika au unit baki tulia tandika maandiko tupia mabalozini huko subordinates wako wanakuwa bizr na activities, phd wa vyuo angalau wana pata grant za research ila hawa wa mofisin asee mtihan.
ukitaka kujua ilivyo ngumu angalia ma PhD waliopo bungeni
 
Mradi unaweza kuwa tentative kwa Donor na akaubali na bado ukaja kubuma kwa maana hautekelezeki, haupimiki kimatokeo mkuu. Kuna miradi mingi donors huwa wanaikatisha katikati au mnatekeleza awamu, mnaandika report na pesa haitoki tena na mnaambiwa wazi.

Mfano mzuri ni REA Mradi wao wa Nishati mbadala kutumia umeme wa Jua kutengeneza Min Grids za umeme kwa vijiji vilivyo visiwani ambavyo havifikiwi kimiundombinu, Ulikuwa Funded na European Union. Mwisho wa siku ulikuwa na uhalisia lakini haukutekelezeka na fedha za awamu zilitumika.
Chukua mfano mwingine wa Dege Eco Village, wakati wanaufanyia Appraisal naamini ilionekana kweli ni mradi mzuri ila mwisho wa siku ukawa Ghost, wa kuleta hasara, hautekelezeki kwa contest na mazingira yetu.
Unataka kuzungumzia HCD au? Human centered design haijamaliza kila kitu.. kutekelezrka kwa mradi kunahitaji pia uvumilivu wa kuruhus tamaduni za watu wale kupokea kwa Kasi ndogo. Hii ni kesi ya Social initiatives sio kwa business kama estates za dege. Kwa nn wa dege ulibuma? Wapi panafanana na huo wa rea na wapi panayofautiana kati ya hiyo miwili kwa observation yako?
 
Mkuu ni kweli hali ya uwezo wa baadhi ya watumishi wa Umma inasikitisha na kukatisha tamaa.

Ingawa siungi mkono google search, Tafsiri ya ulichoandika ni kuwa weledi wa watumishi wa Umma upo chini.
Nakubaliana nawe, kuna viashiria vingi vinavyoonyesha kuwa baadhi ya watumishi wa umma hawana weledi stahili kwenye utendaji, uongozi na nafasi za kisiasa. Udhaifu unaonekana katika maamuzi, ubunifu, na utekelezaji wa sera.

Zamani ilikuwa vigumu kwa mtu anayefanya kazi kufaulu na kupata shahada au stashaha. wengi walikuwa wana discontinue au wanafaulu kwa tabu sana kutokana na utu uzima au uwezo wao kuwa mdogo. Lakini kwa sasa ni rahisi zaidi kwa watumishi kufaulu vyuo vikuu kuliko watoto wanaotoka A'level directly. Hii inatokana na ukweli kuwa sasa kuna njia mbadala nyingi za kufaulu vyuoni kuliko jitihada na uwezo wa mwanafunzi. Ukiwa na ushawishi, ni rahisi kupata B, M hadi PhD wewe tu na mbinu zako. Hivyo undeperomance kwa graduate wa sasa siyo kitu cha kushangaza.

Katika Ofisi fulani kuna mtaalamu ana MBA na CPA lakini anakodi watu wamwandikie riport na majibu ya CAG. Kuna mtu ni wakili aliyesajiriwa lakini hawezi draft mkataba. Kuna mtu ni Katibo Mkuuu lakini hawezi kutafsiri ripoti ya andiko la mradi. Unakuta watu wamevaa suti zimewakaa wanakula uapisho, unajua yes sasa taasisi itafufuka, akifika ofisini utatamani aliyetumbuliwa arudishwe!

Yaani huwa inashangaza kumkuta Katibo mkuuu, wakurugenzi na wasomi wanapambana ili kupiga pesa za posho za safari au ku overestamate bajeti kwa dhumuni ya kuiibia serikali. Watu kama utani wanakutana baa kujadili namna ya kuandaa dokezo la kupiga pesa, na kweli mchongo unafanikiwa, lakini haohao hawawezi kuandaa dokezo la maana la mradi. Mbaya zaidi, ikitokea kuna mtu ana upeo mkubwa na uwezo wa kutoa solutions za changamoto, atachukiwa na kupigwa vita kuanzia waziri, katibu, mkuu wa taasisi na benefiries wa udhaifu, mwishowe utengenezewa zengwe ili aonekane hajui kitu. watu wanapenda ku maintain status Quo ili waendele kupiga fedha za umma.

Ili kuishi katika mazingira ya sasa baadhi ya wasomi wameamua kujifyatua tu ili mambo yaende na wattoto wapate mlo.

Mungu atusaidie
Nchi hii kamwe haitaendelea!
 
Mwaka 2016 nilibahatika kuhudhurua annual technical meeting ya NGO moja hv ambayo ilikuwa imefadhiliwa mradi wake na UNEP kuhusu mambo ya climate change, wale jamaa walikuwa wametengewa bilioni 100 kwa miaka mitatu. Ndani ya mwaka mmoja walikuwa wametumia 38 bilioni. Kwa ufupi mradi ulikuwa uwe wa serikali, ila naona ile NGO ndio ilikuwa inaishirikisha serikali coz fund zilipitia kwao. Jamaa walikuwa wanajiandalia tu study tour mara sijui Moroco sijui Indonesia na per diem za kufa mtu. Ukitumia akili hela za mabeberu zipo hazina matumizi.
Huko nje kuna watu wanamapesa mengi mengi sana, kazi yako wewe ni KUJIELEZA TU (kuandika Proposal).
 
Mtu ukimsimamisha tu kwenye mkutano wa kijiji anaongea kwa kutetemeka na lugha ni Kiswahili huyu mtu kwa kutumia English anaweza kuongea mbele ya wazungu akaeleweka
Tatizo elimu ina mtiririko wa kukutaka ukariri na ufaulu ila si kuelewa,unaweza ukawa shuhuda lecture anataka utoe definition kama alivyoiandika,ila ukiandika kitu kinachofanana na chake na asielewe huna bahati
Sijui ata niishauri kitu gani hii serikali
 
Inashangaza unakuta mfanyakazi mwenzako kasoma Sawa ana master ila kuandika kuomba hela za miradi Kwa ma donors wetu hawezi sijui niseme hana idea wakati kila kitu kipo Google ni yeye kusuka tu wazo la hela ya kawaida wazungu Wana hela kibao hakuna PA kuzipeleka ziko hewani.

Mtu kijana under 40 msomi wa level ya master unabaki kugombania hela za per diem za ndani nako ni pesa madafu tu nini tofauti yako na uliowazidi shule?

Wewe ulipaswa uwe unaandika lipitishwe bora likataliwe ila upewe sababu utarekebishwa andika andika andika tena lazima ipo siku litatiki uka coordinate Michongo. Hela za mabadiliko ya tabia ya nchi zipo kama zote mamifuko yanatoa.

Mavyeti kibao unabaki kutumia Google ku watch nonsense everyday.
Kwamba hajui kusima na kuandika? Au ulitaka aandike kama wewe ulivyokaririshwa?
 
Back
Top Bottom