Inakuaje maofisini huku msomi ana Masters ila hajui kuandikia mradi

Akirudi ripot anawapa muandae yaani watu wanapenda pesa rahisi, nimefanya kazi Taasisi yaani management wanashindwa kuandika proposal ya kuomba pesa ya overtime .
 
Mkuu unashangaa hilo. Mwezi mmoja uliopita nilikuwa pale costech kuna mwajiriwa hajui kuhamisha vitu from email to flash na wakati kaajrii kitengo cha data.
Nilibaki nashangaa
 

Mradi unaweza kuwa tentative kwa Donor na akaubali na bado ukaja kubuma kwa maana hautekelezeki, haupimiki kimatokeo mkuu. Kuna miradi mingi donors huwa wanaikatisha katikati au mnatekeleza awamu, mnaandika report na pesa haitoki tena na mnaambiwa wazi.

Mfano mzuri ni REA Mradi wao wa Nishati mbadala kutumia umeme wa Jua kutengeneza Min Grids za umeme kwa vijiji vilivyo visiwani ambavyo havifikiwi kimiundombinu, Ulikuwa Funded na European Union. Mwisho wa siku ulikuwa na uhalisia lakini haukutekelezeka na fedha za awamu zilitumika.
 
ukitaka kujua ilivyo ngumu angalia ma PhD waliopo bungeni
 
Unataka kuzungumzia HCD au? Human centered design haijamaliza kila kitu.. kutekelezrka kwa mradi kunahitaji pia uvumilivu wa kuruhus tamaduni za watu wale kupokea kwa Kasi ndogo. Hii ni kesi ya Social initiatives sio kwa business kama estates za dege. Kwa nn wa dege ulibuma? Wapi panafanana na huo wa rea na wapi panayofautiana kati ya hiyo miwili kwa observation yako?
 
Nchi hii kamwe haitaendelea!
 
Huko nje kuna watu wanamapesa mengi mengi sana, kazi yako wewe ni KUJIELEZA TU (kuandika Proposal).
 
Mtu ukimsimamisha tu kwenye mkutano wa kijiji anaongea kwa kutetemeka na lugha ni Kiswahili huyu mtu kwa kutumia English anaweza kuongea mbele ya wazungu akaeleweka
Tatizo elimu ina mtiririko wa kukutaka ukariri na ufaulu ila si kuelewa,unaweza ukawa shuhuda lecture anataka utoe definition kama alivyoiandika,ila ukiandika kitu kinachofanana na chake na asielewe huna bahati
Sijui ata niishauri kitu gani hii serikali
 
Kwamba hajui kusima na kuandika? Au ulitaka aandike kama wewe ulivyokaririshwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…